BAADHI YA NYWELE ZA BANDIA SIO NZURI



Nywele zinazovaliwa kila siku na kina dada na kina mama vina uhusiano mkubwa na maiti waliozikwa kisha watu kwenda kuchukua nywele zao makaburini au mahospitalini.
        kinachoshanga zaidi ni kwamba wengi wa wadada wanajua hili swala lakini wameweka urembo mbele na kutembea na maiti kichwani.
   kwa wanaume hebu jiulize inakuwa je unapenda mke mwenye nywele za maiti hali ukijua sio zake? Tuko katika wakati wa siku za mwisho na Biblia katika danieli 12:4 kwamba siku za mwisho maarifa yataonezeka na 2 Timotheo 3:1-5 inasema siku za mwisho kutakuwako na nyakati za hatari maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha,wenye kujisifu,wenye kiburi,wenye kutukana,,wasiotii wazazi wao,wasio na shukurani,wasio safi,wasiowapenda wa kwao,wasiotaka kufanya suluhu,,wasingiziaji,wasiojizuia,wakali,wasiopenda mema,wasaliti,wakaidi,,wenye kujifuna.,wapendao anasa kuliko kumpenda MUNGU,wenye mfano wa utauwa lakini wakikana nguvu zake hao nao ujiepushe nao. wakati huu ndio wakati wa haya yote na shetani naye akijua kuwa ana muda mchache tu anatafuta wanadamu wamkatane YESU ili waende nae motoni milele na yeye haji direct ila anatumia vitu ambavyo wanadamu wanavipenda sana mfano wanaovamiwa zaidi na mapepo ni wadada unadhani ni kwanini? mapepo huwekwa kwenye nywele bandia, kwenye pete, heleni, cheni,bangili, marashi/ perfume, mafuta na pia vipodozi mbalimbali. Lengo langu sio kukukataza kutumia vitu hivi ila nakuomba sana tena sana kuomba kwa ajili ya vitu hivi hasa pete na kuvunja maroho yote yaliyopandikizwa ndani yake na kuharibu kila kusudi la shetani ndani ya vitu hivi ndipo utumie. pia tambua kuwa mapepo yakiingia ndani yako kupitia vitu hivi yatasababisha ujitenge na MUNGU mfano ukiwa na mapepo hutapenda kwenda kuombewa ili yatoke labda kwa neeema ya MUNGU, pia yanaweza kuzalisha kiburi hata kwa wazazi wako au kusababisha kupenda sana mambo fulani ambayo ni dhambi mbele za MUNGU BABA ambayo wakati mwingine huwa hadi unasema kwamba nafanya jambo hili lakini sipendi, ni kweli hupendi lakini nguvu ya mapepo ndio inakulazimisha kufanya hivyo nenda kwenye maombezi ili ufunguliwe. ushauri wangu vunja roho ndani na vitu hivi kwa maombi kwa jina kuu la YESU KRISTO ndipo uvitumie pia kama hujampa YESU maisha yako fanya hivyo leo tafuta kanisa la kiroho na waeleze watakusaidia. MUNGU akubariki

Comments