JE NIOMBEJE ILI MUNGU AJIBU MAOMBI YANGU

  • NAHARIBU KILA HILA ZA SHETANI NA NASAMBARATISHA VIKAO VYOTE VYA UCHAWI VILIVYOKAA KWA AJILI YANGU KATIKA JINA LA YESU.{KUOMBA KWA MAMLAKA NA KUOMBA KWA IMANI HUKU UKIWA MTAKATIFU KUNA USHINDI MKUBWA}
    MKIOMBA LOLOTE KWA JINA LANGU HILO NITALIFANYA {YOHANA 14:14}
    TUKIFANYA KAZI TUTAFANYA LAKINI TUKIOMBA MUNGU ANAFANYA KAZI KWA AJILI YETU HIVYO MAOMBI NI MUHIMU SANA KATIKA MAISHA YA WAKRISTO

    {Nngeomba uniandikie sara ambayo ntaitumia wakati wa usiku na asubuhi kaz njema.} hili ni swali lililo ulizwa na ndugu mmoja katika page yetu ya www.facebook.com/maishaYaUshindi.

  • asante sana kaka kwa kile ulichoniomba nikuandikie sara ya kuomba usiku au mchana.Kaka maombi halisi ambayo MUNGU anataka si yale ya kukariri bali MUNGU anataka uombe kana kwamba unamwomba rafiki yako ila katika maombi yako muda wote nakuomba zingatia yafuatayo. 1.katika maombi yako anza na kumshukuru MUNGU kwa ulinzi wake kwako .                                                                                                     2.tubu kwa MUNGU hata kama hujui kama umetenda dhambi yeyote maana sisi wanadamu wakati mwingine huwa tunatenda dhambi pasipo kujua hivyo tubu kwanza maana Biblia inasema maombi ya mtu mwenye dhambi MUNGU hayajibu hivyo kama unataka MUNGU ajibu maombi lazima utubu kwanza  .                                                                            3.omba chochote kwa MUNGU na yeye atakujibu .                             4.baada ya maombi yako yoyote shukuru kwa MUNGU kwani hata huo muda wa kuomba MUNGU ndio aliyekupa. ukiomba kwa kuzingatia hivyo vipengere MUNGU lazima atakujibu maombi yako lakini lazima licha ya kufanya yote hayo lazima uwe umeshampa YESU maisha yako kwanza. kaka zingatia tu hivyo vipengere 4 yaani kushukuru,kutubu ,kupeleka mahitaji yako kwa MUNGU na kushukuru. pia kumbuka maombi yako yote omba katika jina la YESU na hitimisha katika jina la YESU. ni hayo tu kaka ubarikiwe sana na nakutakia siku njema na ukizingatia hayo lazima utaona matokeo na lazima pia uombe kwa imani pia soma mistari hii katika Biblia ili ikusaidie katika maombi yako; YOHANA 14:14, ZABURI 136:1-26,WAEBRANIA 11:1 NA WAEBRANIA 11:6.AMEN. Ubarikiwe sana ndugu na pia katika maombi kuna aina nyingi za maombi kama Maombi ya vita na maombi ya kusihi na hayo unaweza kuomba huku umefunga au hata hujafunga ila katika maombi hayo yote husika na hivyo vipengere 4 hapo juu.

    KUNA NGUVU KATIKA MAOMBI YA KUHAMISHA MILIMA YA MATATIZO,MAGONJWA NA KILA AINA YA UONEVU WA SHETANI HIVYO OMBA KATIKA JINA LA YESU NA UTAONA MAJIBU
    TUKIOMBA SAWA SAWA NA NENO LAKE YEYE NI MWAMINIFU NA WA HAKI LAZIMA ATAJIBU MAOMBI YETU

Comments