MAISHA YA USHINDI NI NINI?

Tumia Dakika Moja Kuubadili Ulimwengu OMBA KWA AJILI YA MATAIFA AMBAYO KANISA LINAPITA KATIKA WAKATI MGUMU MFANO Ombea taifa la Liberia. Idadi ya watu: 3,000,000. Asilimia 37% ni Wakristo. Ni taifa lililoharibiwa na vita. Waamini wengi ama wamekufa au wameikimbia nchi. Ni kazi ngumu kuijenga upya. 1. Maisha Ya Ushindi Ni Nini? Katika Yn 10:10 Yesu anatumia neno zoe kwa lugha yake mwenyewe, akimaanisha uzIma. Mara nyingi watu hudhani kwamba uzima hupimwa kwa kuzingatia wingi wa mali tulizonazo, lakini Yesu hakubaliani na hilo (Lk 12:15). Zoe ni maisha Yesu aliyoishi; maisha ya Mungu mwenyewe, uzima wa milele, uzima tele, uzima halisi na wa kweli; maisha motomoto na ya kiutendaji, ufuasi na utii kwa Mungu, yaliyobarikiwa sasa, na kudumu milele. Mpango Wa Mungu Kwa Ajili Yako Ni Zoe Pia Warumi 8:29, 30 inasema ~ Anavifanya vitu vyote vitende kazi kwa mpango na makusudi yake, kwa manufaa yako. Alikujua wewe kabla ya nyakati kuanza. Alikuita. Alikufanya mwenye haki, akazichukua dhambi zako. Anajishughulisha sana kukufanya wewe ufanane na Yesu. Ameshakutukuza tayari, na kwa imani utukufu ni hatima yako ya uhakika. 2. Je, Ina Maana Gani Kufanana Na Yesu? Mungu anaposema anatufanya tufanane na Mwanaye, hana maana ya kufanana kwa sura ya nje bali kwa ndani, yaani maisha maadilifu. Mungu anawachukua watoto wake katika safari ya marejesho (Mwa 1:26) akitubadilisha kidogo kidogo tuendelee kufanana na Mwana wake Yesu, tukishiriki utakatifu wake, mawazo yake, asili yake na hata ubora wa maadili yake. Tunataka kufanana na Yesu, lakini wakati mwingine tunafanya kosa la kujaribu kumsaidia Mungu kwa kujitahidi sisi wenyewe kuwa wema, au kwa kuzitii sheria za dini zetu. Tunafanya kila jitihada ya kibinadamu na baadaye tunakata tama kwa sababu hatufanikiwi. Mara tunagundua mgongano mkubwa ndani mwetu baina ya pande mbili zenye asili tofauti zinazopingana; asili yetu ya zamani ya dhambi, na asili yetu mpya ya upendo wa Mungu. Mioyo yetu ina shauku kubwa ya kutenda yale yanayompendeza Mungu, lakini mara kwa mara tumekuwa tukitenda kinyume chake (Gal 5:17-21) (Rum 7:15-25). 3. Je, Tunawezaje Kuachilia Uzima Wa Mungu? a. Chagua Kuenenda Kwa Roho Ni afadhali umruhusu Roho Mtakatifu atawale maisha yako kila siku kuliko kujaribu kuishi kwa kufuata sheria (Gal 5:1; 16:18). Mwache Roho Mtakatifu alete ndani mwako tunda la Roho, yaani upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, na kiasi (Gal 5:22, 23). Mabawa Mawili Ya Njiwa Wa Mungu Watu hufukuzia sana karama za Roho Mtakatifu lakini tunda la Roho pia ni muhimu sana kwa sababu ni tabia ya Yesu. Unapoona tunda unakuwa na uthibitisho wa uhakika ya kwamba Mungu anatenda kazi ndani yako ili kukufanya ufanane na Yesu zaidi na zaidi. Tunda la maisha yaliyobadilishwa ni ushuhuda mzuri pia. Roho Mtakatifu hupanda mbegu za tunda ndani ya mioyo yetu, lakini ni lazima tuiruhusu mbegu ikue na kutusababishia sisi maisha yanayofanana na ya Yesu ili watu wote waweze kuona. Kwa mtu kuwa na ujuzi wa matumizi ya karama za Roho Mtakatifu peke yake haituhakikishii kwamba mtu huyo ni mwadilifu na kwamba anaishi maisha matakatifu. Kila mara tafuta tunda. b. Chagua Kuyafisha Maisha Ya Kale Soma orodha iliyoko katika Gal 5:19 ili upate picha ya mtu anayeishi maisha ya peke yake. Hiyo asili mbaya na ya zamani imetujia kutoka kwa mtu wa kwanza Adamu, ambaye alimwasi Mungu na kuambatana na uongo wa Shetani. Mungu alimwacha Adamu na roho yake ambayo ndiyo iliyomjua Mungu ikafa ndani yake; akawa amebakiwa na mwili na nafsi peke yake. Kutokea hapo, matakwa ya mwanadamu yakatawala maisha yake. Sasa anataka njia zake mwenyewe, na si za Mungu. Ni hiyo asili mbaya na ya zamani anayozungumzia Paulo akisema kwamba tunapaswa kuisulibisha, yaani, kuifisha (Gal 5:24). Je, Unaweza Kujisulibisha Mwenyewe? Jaribu! Simama, na ujifanye kama una msalaba, nyundo na misumari kwa ajili ya mikono na miguu yako. Sawa, huwezi kujisulibisha! Hata ungejitahidi namna gani huwezi kamwe kuifisha asili yako mbaya na ya kale. Lakini kuna habari njema. Yesu Amefanya Kwa Niaba Yako Unalopaswa kufanya ni kupokea mauti yale na maisha mapya kwa imani. Fanya hivi: Ukisoma kitabu cha Warumi mlango wa 1 hadi wa 5 utagundua kwamba Mungu amemweka mwanadamu kwenye kona. Mwanadamu ni mwenye dhambi asiyekuwa na msaada wo wote na hawezi kujiokoa mwenyewe mpaka atakapogundua kwamba Yesu alimfia. Hilo humfanya mwanadamu awe na amani na Mungu. Ukiendelea kusoma Warumi mlango wa 5 hadi wa 7 mstari wa 25 utagundua kwamba mwamini huyu asiye na msaada anawekwa kwenye kona nyingine ya kukata tamaa na analia kuomba msaada (Rum 7:24). Kupatikana kwa jibu kunamletea mtu huyu amani. Jibu Ni Nini? Linapatikana kwa kuamini (Rum 6:1-14). Utu wetu wa kale ulikufa mara moja tu pale Msalabani pamoja na Kristo (ms 6). Utu wetu wa kale uliofishwa, pia ulizikwa pamoja na Yesu (ms 4, 5). Sisi tumeunganishwa na Yesu katika ufufuo wake, maisha yake mapya, zoe yetu. Tahadhari; utu wetu wa kale hautulii tu kaburini bila kufurukuta. Unapaswa kuvumilia katika ukweli huo ili kuachilia ushindi kamili (Rum 6:4, 5, 8, 10). Kila siku jihesabu kuwa mfu kwa habari ya dhambi. Kila siku jihesabu kuwa hai kwa Mungu na uutoe mwili wako autumie (ms 11). Kwa imani achilia uzima wa Kristo na kutawala katika uzima huo kama Paulo alivyofanya. Soma shuhuda zake katika maandiko yafuatayo: (Gal 2:20) (Kol 1:29) (Efe 3:20) (Flp 2:13) (Rum 5:17). Warumi 8 ni aya tukufu inayohusu maisha yanayoongozwa na Roho. Soma jinsi waamini wanavyotupilia mbali laana na sheria ya dhambi na mauti; na kuingia kwenye sheria ya Roho wa uzima, yaani zoe, maisha ya ushindi. c. Hatimaye, Nenda Sawasawa Na Roho Katika Gal 5:25 Paulo anasema kwamba kwa kuwa sasa tunao uzima wa kweli na halisi kwa uweza wa Roho, tunapaswa kutembea naye katika hatua zinazofanana kama askari, tupate kustawi, na kuona mambo yakibadilika na kuwa mema. Lakini Paulo anatahadharisha kwamba katika maisha haya yenye kuongozwa na Roho hapakosekani majaribu; kwahiyo tuwe macho (Gal 5:26 - 6:2).

Comments