MAMLAKA YA YESU KRISTO NI KUU SANA


WATU WALIOJITOKEZA KUOKOKA KATIKA MKUTANO WA INJILI ULIOENDESHWA NA MCHUNGAJI AMOS LUKANULA HUKO MWAKAJE ZANZIBAR
Watu wengi hawamjui YESU na wengine husema yeye ni mwanadamu tu aliyepata kuishi duniani na ukiwauliza wakuonyeshe mwanzo wa YESU hakuna  sehemu watakapokuonyeshe iwe ndani ya BIBLIA ambalo ni neno pekee la MUNGU aliye hai au hata kwenye kitabu kingine chochote watakachokuambia tu ni kwamba kwa duniani alizaliwa na bikra Mariamu  kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU lakini alitoka mbinguni na ili tumfahamu vizuri BWANA YESU lazima tusome Biblia kwani katika Mika 5:2{yesu KRISTO yupo tangu milele iliyopita hivyo hana mwanzo wala mwisho } na katika Tito 2:13 [ YESU KRISTO ni MUNGU MKUU}  pia katika Isaya 9:6{YESU KRISTO ni  mshauri wa ajabu,MUNGU nmwenye nguvu,BABA wa milele na  mfalme wa amani.YESU KRISTO ni sauti ya MUNGU na mamlaka yake ni ya milele na utawala wake ni wa milele na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa. Waebrania 1:1-2 Biblia inasema ''MUNGU ... mwisho wa siku hizi amesema na sisi  katika mwana aliyemweka kuwa mrithi wa yote tena kwa yeye aliufanya ulimwengu''.Na alipokuja duniani alidhihirisha mamlaka yake na hadi Biblia inasema miujiza aliyoitenda YESU duniani ingeandikwa yote isengetosha nafasi ya kuandika na kayika Marko 1;22 Biblia inasema ''Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri wala si kama waandishi'' na Yohana 5:27 inasema ''Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni mwana wa Adamu''.  Ndugu yangu kumbuka kuwa kuna MUNGU mmoja tu aliye wa kweli na anapatikana katika KRISTO YESU pekee Biblia inasema hivi katika 1Korintho 8:6 ''lakini kwetu sisi MUNGU ni mmoja tu aliye BABA, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja YESU KRISTO ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo na sisi kwa yeye huyo'' pia katika 1 Petro 3:22 Biblia inasema ''Naye yupo mkono wa kuume wa MUNGU amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake'' je katika uzima wa milele itakuaje? katika uzima wa milele MUNGU BABA atakuwa yote katika wote.MUNGU akubariki sana na kama hujamchagua BWANA YESU awe BWANA na mwokozi wako na hatimaye uurithi uzima wa milele nafasi hiyo ni sasa tafuta kanisa la kiroho na waeleze watakusaidia pia kumbuka kuwa BWANA YESU alikufa msalabani ili mimi na wewe tupate uzima wa milele bure kabisa kupitia kumwamini na kumpa yeye maisha yetu na Biblia katika Warumi 14:9 inasema ''Maana KRISTO alikufa akawa hai tena kwa sababu hii awamiliki waliokufa na walio hai pia''  na ndio maana aliwambia mitume katika Mathayo 28:18  ''YESU akaja kwao, akasema nao akawaambia. NIMEPEWA MAMLAKA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI''.ubarikiwe sana ndugu
KUWA NA YESU NI KUWA NA UZIMA WA MILELE
USINIPITE BWANA YESU NA UNAPOZURU WENGINE NA BWANA USINIPITE
TUNAOKOLEWA KWA NEEMA YA MUNGU
YESU NI MAMBO YOTE
MTUMANIE BWANA YESU SIKU ZOTE

Comments