MGANGA ALINILISHA KIDUDE NA IKASABABISHA NIWE NALALA NA MAJINI{sehemu ya 2}

MORASI KACHILA
{Msichana Morasi kachila anaendelea kusimulia yaliyomtokea katika maisha yake kabla hajaokoka}
Tukiwa shambani na mama siku moja kabla ya kusafiri kuelekea zanzibar niliishiwa nguvu na nyoka mkubwa sana mweusi alianza kunizonga na nikashindwa kupiga kelele, Mama aliyekua mbali kidogo na mimi hakuwa anajua mwanzo hadi kama baada ya dk 5 na alipogeuka alinikuta kwenye hali hiyo. Mama akaanza kupiga kelele huku akiomba na kukemea kwa jina la YESU mimi nikujua kilichokua kinaendelea hadi nilipokuja kupata fahamu baada kama ya dk 40,Nilipopata fahamu nilikuta nimezungukwa na baba na mama huku mama akilia na ndipo mama alivyoniambia kwamba ile nyoka ilibadilika na kuwa mtu mzee mwanaume akiwa uchi na mama alipozidi kuomba yule mzee alitoweka ila ikasikika sauti ikisema hata aende wapi lazima tu tutamuua kwani ana alama yetu na watu wetu wanaishi ndani yake hivyo tunamuona massa 24 kila siku. siku hiyo sikulala kwa amani na nilikua kama mgonjwa. Kesho yake tulianza safari ya kuelekea Dar es salaam hatimaye zanzibar tulisafiri mimi pamoja na mjomba. safarini tulisafiri salama tu japokua mwili wangu ulikua na uchovu sana tulifika Dar es salaam kesho yake na baadae tukalala Dar na siku ya pili yake tukaanza safari kuelekea zanzibar tukiwa kwenye boti nilianza kuhisi kutapika kwani ilikua ni mara yangu ya kwanza kusafiri baharini baadae nilianza kupoteza fahamu  na sikujua kinachoendelea hadi tulipokaribia kufika zanzibar kwani safari ile ni kama masaa 2 tu. Baada ya kuzinduka mjomba akaniambia kuwa nilipandwa na uchizi nakawa kama mwehu na ilikua kidigo tu nijitupe baharini ila kaka mmoja mwanajeshi akanidaka na muda huo wote nilikua naongea lugha isiyofahamika, Tulifanikiwa kufika salama nna maisha yaliendelea japokua kwangu ilikuwa tatizo kubwa kwani usiku majini walikua wanakuja wengi sio kama kule kijijini kwetu kigoma,hapa zanzibar kwani huku majini mengi yalikuwa yanakuja kila siku tena mengine yanakuja kama mwanaumke na akifika ananinyoshea kidole tumboni kwangu na kile kidude kinatoka kisha anabadirika na kuwa mwanaume na kuniingilia. Haya yote nilifanya siri sikutaka mjomba ajue wala mtu yeyote kwani nilikuwa nimechoka sana kusumbuliwa na uchawi na majini. Niliendelea kusali huku nikiwa na siri yangu moyoni kwamba kila siku majini yanakuja na kunifanya vibaya hadi siku moja nikiwa kwenye ibada wakati wa maombezi mhubiri akiombea watu ndipo nilianguka ghafla nikiwa nje ya kanisa kwani nilikua naogopa kuwepo wakati wa maombezi nisije nikaanguka lakini siku hiyo nikiwa hukohuko nje nilianguka na nikaja kuchukuliwa kupelekwa ndani  ya kanisa nikaombewe siku hiyo niliombewa lakini kile kidude hakikutoka kwani wakiomba kilikua tu kinasogea kutoka tumboni na kukaribia mdomoni lakini kuna nguvu fulani ya uchawi ilikua inarudisha baada ya hapo nilipata unafuu kidogo lakini akili ya kuwambiwa watumishi wa MUNGU ili wanisaidie sikuwa nayo. kesho yake usiku nikiwa nimelala walikuja wachawi na majini pamoja na wifi wakaniambia wanashukuru kwa maana hata mimi mwenyewe napenda kufa kwani kitendo cha kukubali kuombewa wakati wao wana vitu vyangu vingi tu na huwa wananiona muda wote na chochote ninachofanya,  baada ya pale waninipiga na kunitisha sana na kuniambia siku sio nyingi nitakutana wa wadogo zangu pamoja na dada yangu na kaka yangu waliokwisha kufa zamani na kusema kuwa yeye wifi amewafanya misukule, Kesho yake usiku alikuja tena wifi na baba mmoja na visichana 2 pamoja na wavulala wawili na alipofika tu wifi akawambia wale wasichana na wavulala  wanitese kiukweli mateso niliyopata siku hiyo MUNGU ndo anajua na walinitesa sana na nilipowaangalia kwa makini niliwafahamu ni ndugu zangu wa baba mmoja na mama mmoja waliokwishafariki niliwaita majina lakini waliendelea kunitesa na kuniambia kuwa mimi hawanifahamu na nilipowaita majina ndipo walipozidi sana kunitesa. Kesho yake niliamka nikiwa hoi na uso umevimba sana mke wa mjomba aliponiuliza nilimdanganya tu na siku hiyo jioni nilikwenda kanisani kwenye uimbaji kwani nilijiunga na kwaya ya vijana kanisani. nikiwa kanisani nilishindwa kuimba na kiongozi wa kwaya akaniambia nipumzike pembeni wao wakiendelea na uimbaji wakati wanamaliza kuimba walianza kuabudu kwa ajili ya kuomba na kuondoka pale kanisani ndipo nilianguka tena na kuanza kuombewa waliniombea kutoka saa 12 joni hadi saa 4 usiku na kile kidude kikawa kinataka tu kutoka lakini hakitoki. Ilipofika saa 4 usiku walianza kuniuliza kwa kina kwamba kuna kitu gani tumboni ambacho niliwahi kulishwa? Nikawambia ukweli na wakati huo huo nikaanza kuwaona wachawi wengi sana pamoja na wifi wakisema leo ndo tumekuja kukuchukua kwani siku ya kikao chao imefika,Niliogopa sana japokuwa walikua mbali sana na kanisa kwani kanisani tulipokuwa tulikuwa tumezungukwa na moto japokuwa haya yote niliyekuwa nayaona ni mimi tu.nilimwita mchungaji pembeni na kumweleza yote akaniambia hao uliowaona leo hautawaona tena maana ni zamu ya MUNGU BABA kunitendea muujiza. Walianza kuomba na huku mimi naitwa na wale ndugu zangu marehemu tena wakilia na kujifanya wapole sana siku hiyo kumbe lengo lao nitoke nje wanikamate na kuniua kwani huko nje ule moto uliolizunguka kanisa haukuwepo.Nilijikuta nashawishika kwenda nje na kila nilipotaka kwenda nje wanamaombi walinizuia huku wakiendelea kuomba. Nilipoteza fahamu na nilikukuja kuzinduka saa 10 alfajiri huku wakiendelea tu kuniombea na muda huo nazinduka nilikuta nimetapika sana na maombi yaliendelea kidogo ndipo kile kidude kilitoka tumboni mwangu huku nakisikia na kilipotoka nilijiona wa tofauti sana. Namshukuru sana MUNGU BABA kwa neema na uzima alionipa.na kiukweli hakuna msaada kwa waganga wa kienyeji hata mmoja ila msaada pekee ni kwa BWANA YESU na mimi ningepona mapema sana  ila kuficha siri nilikosea sana.Baada ya pale kesho yake wale wachawi walikuja wengine wakiwa vilema na kusema nimesababisha kambi yao kuchomwa moto na majini wote kufa na pia wengi wao wamekufa nilikemea muda uleule na sikuwaona tena. Baada ya siku 3 nilijazwa ROHO MTAKATIFU na  ninaendelea na wokovu hadi sana nakuomba tu ndugu endelea kuniombea na tuombeane ili tufike uzima wa milele pamoja na BWANA YESU. {ndugu mwana maisha ya ushindi sehemu ya mwisho Morasi atasimulia jinsi alivyochukuliwa mbinguni na jinsi alivyoonesha mambo mbalimbali na pia alivyoambiwa kuhusu baba yake na ndugu zake  na aliambiwa aache dhambi za kiburi pia alivyoambiwa afanye kazi ya MUNGU. kwani alipata neema ya kumwona BWANA YESU katika utukufu wake hii itaendelea siku ya jumatatu. ubarikiwe sana ]

Comments