MGANGA WA KIENYEJI ALINILISHA KIDUDE{sehemu ya 3}

MORASI KACHILA BAADA YA KUOKOKA
Si ninyi mlionichagua mimi ,bali ni mimi niliyewachagua  ninyi ; nami nikawaweka  mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lolote mmwombalo BABA kwa jina langu awapeni {YHANA 16:16}
{msichana Morasi kachila anaendelea kusimulia yaliyotokea katika maisha yake,baada ya kutuambia aliyofanyiwa na mganga wa kienyeji,alivyosafiri kutoka kigoma hadi zanzibar,walivyomtesa majini kule zanzibar, alivyookoka na jinsi alivyofunguliwa.Leo anaendelea na sehemu ya mwisho jinsi alivyochukuliwa mbinguni na alivorudi na majukumu aliyopewa kule mbinguni. lakini nimemuuliza aelezee kidogo kuhusu kile kidude kilienda wapi baada ya kutoka tumboni? huyu hapa anaendelea} baada ya maombi ya muda mrefu wa wale watumishi wa MUNGU na kufanikiwa kutoka kwa kile kidude saa 10 alfajiri kilipotoka kilidondoka na zikasikika sauti zikisema kwamba ngoja tu tutoke na huku zikisikika kelele kama za mtu anayalia kwa uchungu sana baada ya kushambuliawa na kilipodondoka chini  na kuungua na moto. Baada ya kupona kutoka katika janga hilo lililosababishwa na mganga wa kienyeji nikawa mzima kabisa na kiukweli asingelikua BWANA YESU ningekua nimeshakufa. hata kwa hili napenda kuwaambia na wengine kwamba hakuna msaada wowote kwa mganga wa kienyeji. Na kama unaumwa au una matatizo nenda hospital na pia nenda kwenye maombezi hakika utapona kwa muda mfupi sana  hata wewe mwenyewe utashangaa. Baada kupona kabisa niliishi kwa amani na hakuna tatizo lolote hadi sana lakini napenda kukushuhudia jambo moja baada kufunguliwa kutoka nguvu za giza nilipigiwa simu kutoka nyumbani kuwa yule wifi mchawi alikua mgonjwa sana nadhani itakua kwa sababu ya  moto ule niliouona pale kanisani siku ile alipokuja kuroga na wenzake majini wakateketea. na baada ya wiki 2 tukiwa kwenye maombi usiku maana nilijiunga na kundi la maombi kanisani,nilijikuta nanena kwa lugha  na nilipozidi kunena huku na wenzangu wakiendelea na maombi niliona na  mbingu zinafunguka na malaika wawili walinichukua na kwenda sehemu nzuri hata haielezeki kwa uzuri wake na kule mimi sikufahamu ni wapi ila yule malaika akaniambia kuwa ni mbinguni na haikuchukua hata muda mrefu kufika huko ni sekunde chache tu na tulipofika tulikua malaika wengi hata kuwahesabu huwezi maana ni wengi sana na katikati yao kulikua na mwanga mkali sana na ikasikika sauti ikisema mleteni nikapelekwa  pale na alikuwa ni BWANA YESU na tulipokaribia hata mimi nilikua nimeshabadirika na kung'aa sana tofauti na ninavyojifahamu. nikiwa pale mbele ya BWANA YESU nilipewa tunda zuri sana ili nile lakini nikajikuta nasema '' MUNGU wangu hili tunda sitashiba'' BWNA YESU akaniambia kula na nilipokula tu kidogo nikashiba yaani hata robo ya lile tunda sikumaliza nikaanza kujiuliza hivi mimi nikikua nasema nini?. Baada ya pale kwa pembeni niliona kioo kikubwa sana na ni kaanza kuangalia, nikama mtu anaangalia TV nikaonyeshwa maisha yangu yote tangu nazaliwa hadi muda huu na nikaona jinsi wifi alivyonyofoa miguu yangu na kuniwekea ya bandia ili nisitoroke mbele zake na pia jinsi alivyochukua unywele wangu na kuuweka chini ya kitanda chake ambako kuna shima kubwa na huko ndani ya shimo ndiko anakotunzia mali zake za kichawi na pia jinsi anavyoweza kuingia huko ndani ya shimo na kupitia hukohuko ili kwenda kuzimu, nia niliona jinsi alivyochukua nyayo za miguu yangu, mkoja wangu,kinyesi,na nguo yangu moja na kuvipeleka kuzimu.pia jinsi alivyokua na kioo ambacho kina antena na antena hiyo ni ile nywele yangu na hiyo inamwezesha kuniona wakati wowote na pia kunisikiliza ninachoongea wakati wowote hadi vitu hivi vyote vikateketeza kwa moto wa maombi ya wale wanakanisa.. Baada ya kuonyeshwa hayoyote na mengine mengi tu hata siwezi kuyasema nikamailza BWANA aliniambia kuwa wanadamu nimewaumba ili mniabudu hivyo nenda kawambie wanadamu kwamba ni wakati wa kuacha njia zao mbaya na wanirudie mimi pia aliniambia kuwa nikamwambie baba yangu aache pombe na na dhambi nyingine zote na ampe yeye BWNA YESU maisha yake yote naye atamsamehe na kumpa uzima wa milele pia aliniambia kuwa niache dhambi ya kiburi kwani ndio dhambi inayonisumbua sana na nidumu katika utakatifu pia nimtumikie yeye katika uimbaji na pia niombe sana kwa ajili ya baba yangu ambaye naye miguu yake ilinyofolewa na wachawi na ndo maana hata sasa ni kilema na kweli mimi baba yangu ni kilema wa miguu kwani imepinda hivyo hutembea kwa taabu hivyo nimwombee sana na nifunfe siku tatu na niwashirikishe wanamaombi wa kanisani kufunga siku tatu kwa ajili ya baba yangu.Baada ya hapo aliniambia niwambie wanadamu kwamba ni wakati wa kuacha dhambi na kumpa yeye BWANA YESU maisha yao tena nisema wala nisinyamaze.Baadae nilionyesha kwenye kile kioo jinsi baba yangu alivyonyofolewa miguu na jinsi anavyoteswa na wachawi hivyo nimwombee sana na baadae kidogo nikaonyeshwa wachungaji wa zanzibar wakiwa sehemu kweye jengo moja wakiomba na nje ya hiyo nyumba kuna jitu jeusi sana kubwa  nikaambia niwaombee sana watumishi wake na baadae wachungaji wale waliomba na lile jitu likalipuka. Baada ya ale niionyeshwa mambo mengi sana na nikaambiwa muda wangu wa kurudi duniani umefika nikamwomba BWANA nibaki huko milele akaniambia kuwa nikamilishe kwanza ile kazi aliyonipa huku duniani na akaniambia nimekupa ROHO MTAKATIFU akusaidie katika yote na kweli nikaona ni kweli nimepewa ROHO MTAKATIFU. Baada ya pale malaika akanichukua nikajikuta niko kanisani huku wanamaombi wakiendelea na maombi ni kama ilikua imepita saa moja na nusu tangu niondoke niliona kama niko kwenye giza sana huku duniani maana mahali nilipokua ni pazuri ajabu na panang'aa sana . Nikawasimulia wenzangu na wao wakamshukuru MUNGU. ndugu hakika hapa duniani sisi ni wapitaji tu na kama tukiokoka kwa kumanisha basi wenyeji wetu ni mbinguni sina maneno mengi ya kukuambia hata unielewe ila neno hili moja weka moyoni mwako kwamba ''Baada ya kifo ni hukumu" hivyo heri kuokoka leo na kuna sehemu mbili tu za kwenda baada ya kufa, kama unadhambi unaenda kuzimu kama sehemu ya mangojezi ya siku ile ya kuu na ya kutisha yaani siku ya mwisho na pia kama umeokoka unaenda mbinguni moja kwa moja na huko ni furaha ya milele kwani nimewaona mwenywe wale watakatifu waliofariki zamani pia kumbuka kama ukienda kuzima ni mateso yasiyoelezeka na hakuna anayeweza kukuondoa huko kwani jarada lako linakuwa limefungwa.na hakuna hata mmoja aliyeombewa atoke kuzimu akatoka hata hawa wanaofanya misa za wafu au kuombea wafu hawa wanajifurahisha tu na kufanya machukizo ya kuwafanya watu watende dhambi ili wakifa waombewe kitu ambacho sio kweli na hiyo inakuwa ibada ya sanamu.Hata sijui niseme neno gani unielewe ila okoka ndugu. na tambua kuwa hakuna mwokozi mwingine yeyote ila ni BWANA YESU na hayo niliambiwa na BWANA mwenyewe tena mbele za malaika wasio na idadi katika kiti cha enzi cha mbinguni. {ndugu uliyesoma ujumbe huu wa kweli najua kuna kitu umejifunza na huu ni ukweli mtupu kwani hata mimi mkurugenzi wa maisha ya ushindi nilikuwepo katika maombezi ya morasi na hata alipochukuliwa mbinguni nilikuwepo siku hiyo kwenye maombi. tuiishi lakini tukifahamu kwamba tuanatakiwa kumpa YESU maisha yetu. MUNGU BABA akubariki sana popote pale ulipo AMEN.}
Si ninyi mlionichagua mimi ,bali ni mimi niliyewachagua  ninyi ; nami nikawaweka  mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lolote mmwombalo BABA kwa jina langu awapeni {YHANA 16:16}
kama una habari ya kweli au ushuhuda wa kweli tutumie kwa email mabula1986@gmail.com au mabula 86@yahoo.com au mabula86@facebook.com .

Comments