MAMBO MUHIMU WAKATI WA JARIBU


Mtu aliyejeruhiwa moyo wake



Ndugu zangu wakati mwingine wanadamu huwa tunapitia mazingira magumu sana katika maisha na hiyo husababishwa na tunaoishi nao au wakati mwingine sisi wenyewe ndio tunasababisha hayo magumu, pia Biblia inasema kwamba majaribu hayana budi kuja pia hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea.hivyo majaribu hayakwepeki japokua mengine huja kwa sababu ya sisi kutokua na maombi kumbuka neno la BWANA YESU aliposema kwamba ''OMBENI ILI MSIINGIE MAJARIBUNI'' Muhimu wakati wa jaribu kwa wewe mtoto wa MUNGU
1; Acha kulalamika na kunung'unika; ndugu kumbuka kulalamika na kunung'unika hakuwezi kupunguza maumivu au kuondoa hilo jaribu badala ya kulalamika na kunung'ika oma MUNGU

2;Jihadhari kubeba makwazo; kubeba makwazo huongeza tatizo badala ya kupunguza hivyo hakuna haja ya kubeba makwazo hii inaweza kukufanya uingie dhambini
3;Kili ushindi kila wakati; Biblia inatuambia kuwa ''mwenye imani ataishi kwa imani '' hivyo ushindi wako upo tu
MUNGU BABA akubariki sana somo hili litaendelea
Ubarikiwe.
By Peter M Mabula.
Mabula1986@gmail.com
0714252292

YESU ndie msaada wetu kwani hakuna mwokozi mwingine yeyote zaidi yake {MATENDO 4:12}

Comments