NILINUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUBADILI DINI

ESTER
Naitwa Ester Mahamud japokuwa zamani kabla sijaokoka niliitwa Aisha mahamud nina miaka 21 nimzaliwa wa moshi mkoa wa kilimanjaro,Ninaishi Dar es salaam napenda kuwashuhudia jinsi nilivyotaka kuuawa na mama yangu mzazi kwa kushirikiana na ndugu pamoja na majirani. Mama na baba walitengana nikiwa mtoto mdogo na mimi na mama tukaenda kuishi Zanzibar na baada ya kufika huko mama aliolewa na mwanaume mwingine na maisha yaliendelea kama kawaida.Nikiwa na miaka 15 nilianza kuumwa kichwa na kupagawana na  mapepo hali hii iliendelea kwa muda mrefu na mama alinipeleka kwa waganga wengi wa kienyeji lakini sikupona .Hali hiyo ilinisumbua sana kwani wakati mwingine nimevaa vizuri lakini nikipagawa tu nakujakujikuta nimechafuka sana pia nilikua nasumbuliwa na ndoto za kutisha mara kwa mara. Mwaka 2008 tulipanga safari ya kwenda kilimanjaro na tulilala Dar es salaam kwa kaka na siku hiyo nimelala chumba cha jirani kulikua radio inaongea na ilikuwa WAPO FM na wakati mhubiri wa kwenye radio anamalizia kufundisha alisema yeyote aliyeko majumbani anayeumwa chochote au kusumbuliwa na chochote aweke mkono kifuani na yeye ataomba niliweka mikono yangu kifuani na wakati mchungaji huyo anaomba nilihisi kuna vitu vinatoka mwilini mwangu na baada ya maombezi hayo kwa njia ya radio nilijihisi kuwa mzima japokuwa mimi sikuwa mkristo ila nilitaka tu kupona. Baada ya hapo nililala na kuamka salama na kesho yake tulienda moshi na baada ya wiki3 tulirudi na kulala hapohapo kwa kaka kwani tusingeweza kupitiliza zanzibar moja kwa moja. Pia kumbuka nikiwa kilimanjaro siku moja majini walikuja na kunionya juu ya kujihusisha na ukristo kwani nikiendelea wataniua na kesho yake nikiwa hukohuko moshi nilijisikia wa tofauti kama nataka kufamiwa na majini na hiyo nilijua kwa sababu ya kuvamiwa na majini kwa muda mrefu sana hadi nikajua ishara zao kama wakitaka kunivamia na baada ya kuhisi hivyo nilianza kuomba kwa dini yangu sala zote lakini hali ndio ilizidi na wao majini walianza kunicheka lakini hata sijui nilikumbukaje yale maneno ya yule mhubiri radioni nikajikuta natamka  ''kwa jina la YESU'' wale majini walipiga kelele na kusema wanaungua na kuniambia nisitaje hilo jina tena kwani ndo jina pekee ambalo ni kikwazo kwao. Baada ya kufika kwa kaka tukiwa safarini kurudi nyumbani Zanzibar usiku ule kulikua na hali sio ya kawaida kwani niliweza kuwaona majini na wachawi live na nikaogopa sana ila nikajua kwamba yule YESU wa wakristo ndie kiboko ya wachawi na majini wote lakini siku hiyo hata sijui walinifanya nini kwani hata kutamka nilishindwa na kile chumba ambacho siku ile ya kwanza walifungulia RADIO WAPO siku hiyo haikuwa hivyo na nililala na watoto wa kaka ambao hawakujua chochote kilichokuwa kinaendelea ila walikua tu wanakoroma kiukweli siku hiyo sikulala kabisa ila usiku wa manane kwenye chumba kile jirani nilisikia mtu anaomba na kukemea nguvu zote za giza zilizopo maeneo hayo walikua na mke na mme na waliendelea kuomba na mimi kwa sababu nikuwa na uwezo wa kuwaona majini na wachawi nishuhudia moto ukishuka kutoka mbinguni na kuwateketeza wale majini. Baada ya muda pakawa shwari na muda huo huo baada ya hari kuwa shwari mama alipiga simu na kuanza kuongea kwa hasira kwamba kwanini nashiriki kuwaharibu wenzake? nilimuuliza kivipi alisema kwa sababu namtaja YESU wakati mimi sio mkristo kiukweli sikumwelewa mama na nikawaza sana kwani hata nikiwa huko aliko yeye yaani zanzibar hakuwa ananijali na akaniambia  nijiepushe kuwa karibu na wakristo. Kulipokucha asubuhi niligundua kuwa yule aliyekuwa anaomba chumba cha pili ni mchungaji kijana ambaye amepanga kwenye nyumba hiyo na nilitamani kumshukuru kwa maombi yake yaliyonisaidia sana hata kama yeye hakujua kama ameniombea na mimi Na kiukweli muda wote nilikuwa nawaza mama kajuaje na kwanini hao majini ni wenzako. Kesho yake nilipanda bot na kurudi zanzibar, mama alinifokea sana na nilikaa kwenye ulinzi mkali sana na pia alitumia muda mwingi sana kuwasema vibaya wakristo pamoja na ukristo yeye pamoja na mmewe ambaye ni kiongozi wa dini. nilikaa kwa miezi kadhaa na hali yangu ya kupagawa na kumwa kichwa ilirudi na mama aliniambia kuwa hawezi kunipeleka tena kwa waganga kwani mganga wa mwisho alimwambia wameniwekea majini mengi mno hivyo kwenda kuongeza jini jingine hataki. kwa kusikia hivyo niliogopa sana na kulia sana huku naumwa. Baada ya muda walikuja vijana 2 wakristo wakishuhudia na mama aliwatukana sana lakini wakasema ubarikiwe mama nilitamani sana kuwafuata lakini nilishindwa. Baada ya muda nilipanga kutafuta kazi za ndani ili nipate nafasi ya kuombewa ili nipone kwani kama kwa maombezi ya radio nilipona kwa muda pia maombezi ya yule mchungaji kule Dar nilipona kwa muda mrefu na hadi mama akalalamika hivyo niliuaga mama na kwenda kutafuta kazi ya ndani na nikapata kazi hiyo kwa nyumba ya mkristo japokuwa walikuwa ni wakristo jina tu kwani sikuwaona kujihusisha na kanisani.Nikiwa pale niliwaona wale vijana wahubiri na kuwaomba namba zao za simu na baada ya hapo nilienda kanisani na niliombewa na kupona kabisa hakika hakuna kama YESU KRISTO na hatatokea kama yeye milele na tangu muda huo niliokoka hadi sasa naendelea na wokovu bila kuonewa na nguvu za giza hata siku moja hakika ukiokoka unakaa salama kabisa nje ya uonevu wowote wa wachawi. Baada ya kuokoka mama alifahamu na kuanza kunikusanyia watu ili waniue na alikuja hata nilipokuwa nakaaa na kumweleza mwenye nyumba na mwenye nyumba akanifukuza huku mama akinitafuta zaidi ya mara 4 kuniua lakini MUNGU BABA tu ndie aliniepusha na kifo. Pia mama aliniambia kuwa undugu kati ya mimi na yeye umekufa na yeye sio mama yangu tena hivyo nitafute mwingine. Niliishi kwa mmoja ya waumini wa kanisa lakini nikitafutwa kuuawa kwa sababu nimekubali kujiunga na ukristo. nilikaa zanzibar lakini nilipozidi sana kutafutwa ili niuawe maana nilikua nashinda ndani. Ndipo kanisa likanipa nauli na nikaja kuishi Dar es salaam ambako naishi hadi sasa huku nikiwa nimeokoka na namshukuru MUNGU BABA kwani kanibariki na kunipa mchumba na mwezi uliopita mama alikuja kuniomba msamaha na kuniambia kweli amehakikisha kuwa kuokoka ndio dini ya kweli kuliko zote tena akaniambia kuwa yeye ni mchawi na amejaribu zaidi ya mara 10 kuniua lakini aliwakuta malaika wakinilinda na ametumia wakuu wake wa uchawi zaidi ya watano lakini wameshindwa hivyo anaomba tu nimsamehe lakini yeye hawezi kuokoka kwa sasa labda baadae. SIKU ZOTE NINAOMBA NA NAAMINI IPO SIKU MUNGU ATAMWOKOA.MUNGU awabariki sana na kama hujaokoka ndugu tangu leo tambua kuwa hakuna jambo zuri kama kuokoka na mbinguni ni hakika pia jehanamu na hakika lakini kama tukimpa BWANA YESU maisha yetu hakika tuna uzima wa milele. Amen.

Comments

Unknown said…
DAAAAAAAAAAAAAAHHHH!!!! POLE SANA NDUGU YANGU MUNGU AKUPE NGUVU