NILITAKA KUUAWA JINA LA YESU LIKANISAIDIA

WATSON NA ROSE GOODMAN Baada ya kuchukua mke wangu na jamii kwa imani kurudi Afrika kwa kazi ya KRISTO, niliamka usiku mmoja na pepo mbaya wa kutisha juu yangu .Nilimsukuma goti langu kwa goti lake ili nione kama ni kweli, alinisukuma goti langu ghafla kwa nguvu nyingi na akanijia kwa haraka zaidi kuelekea shingo yangu aninyonge. Nilikuwa na wakati wa kutamka maneno 3 tu, "YESU NISAIDIE" Mara moja akatoweka na katika miaka 35 tangu hapo sijawahi kurudiwa na jambo hilo,kuna nguvu za kushangaza katika jina la YESU KRISTO juu ya shetani na mapepo wote. Liitie jina la YESU KRISTO kwa wokovu na ukombozi wa jambo lolote {Warumi 10:13}. Mwanamke mmoja alimwambia mke wangu pamoja nami kwamba alipokua chuoni kijana mmoja alimchukua kwa matembezi njia ya reli. katika mahali fulani alijaribu kumuuua akitaka ionekane kuwa ameuawa na gari moshi.Dada huyu alipomwamuru katika jina la YESU akawa hana nguvu juu yake kwa nguvu za KRISTO alimlazimisha atembee mbele yake kurudi chuoni. Mwanamke mwingine akamwambia mke wangu pamoja nami kwamba katika siku zake za ujana pasipo busara aliwakaribisha nyumbani kwake kundi la waaguzi. Baada ya hayo pepo wachafu walianza kusogeza vifaa vya nyumbani huku na huku nyumbani kwake . katika hali ya kukosa tumaini aliwafukuza toka nyumbani kwake katika jina la YESU. alipotaja jina la YESU hali ikawa shwari na yeye akajitoa kabisa kwa YESU KRISTO tangu siku hiyo. Biblia katika Wafilipi 2:9-10 inasema "Kwa hiyo tena MUNGU alimwazimisha mno ,akamkirimia jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la YESU kila goti lipigwe la vyitu vya mbinguni na vya duniani na vya chini ya nchi" hivyo jina la YESU ni msaada kwa kila hitaji la mwanadamu na ndilo jina pekee la kusambaratisha nguvu za giza zinazosumbua wanadamu.na katika katika Yohana 14:13 YESU mwenyewe anasema "NANYI MKINIOMBA LOLOTE KWA JINA LANGU HILO NITALIFANYA ILI BABA ATUKUZWE NDANI YA MWANA". Usihurumie vau kusikitikia shetani na mapepo. Kusudi lao ni kukupata wewe uwe upande wao badala ya kuwa upande wa MUNGU.Mzee mkristo akiwa amepatwa na unyonge wa mwili na wasiwasi akilini alinieleza mambo ambayo shetani alikua akimwambia alikuwa anafikiria "kumjaribu shetani kama anaweza" Nilimwonyesha kwamba shetani shetani ni hodari wa kudanganya watu na huwezi kuamini neno analosema . Nikamkemea shetani katika jina kuu la YESU KRISTO . mtu huyo akasema 'ninashukuru umekuja usiku huu" Alionekana mwenye amani ya KRISTO majuma matatu yaliyofuata kabla ya kufa hivyo shetani alitaka asiende uzimani ndio maana alianza kumdanganya. =By WATSON GOODMAN=.MUNGU AKUBARIKI SANA NDUGU POPOTE ULIPO NA KUMPA YESU KRISTO MAISHA YAKO LIWE NDIO JAMBO LA MSINGI NA LA MAANA ZAIDI KWAKO KWANI ULIMWENGUNI TUNAPITA TU ILA HERI MALENGO YETU YAWE NI UZIMA WA MILELE AMBAO UPO KATIKA YESU KRISTO PEKEE {YOHANA 14:6}
KATIKA PICHA NI WATSON & ROSE GOODMAN WAKATI WA KUFUNGA NDOA MWAKA 1946

Comments