SABABU ZA KUFELI NA KUSHINDWA




SABABU ZA KUFELI NA KUSHINDWA (FACTORS OF FAILURE):                                        Kwanini watu wa Mungu wanafeli au wanashindwa au wanakwama? Hili ni swali la muhimu sana ambalo linaweza kuwa kama funguo ya dhahadu katika mlango wa mafanikio a maisha yetu. Kama tukilifungua swali hili vizuri, tutaweza kupata majibu ya matatizo mengi katika maisha yetu sisi watoto wa Mungu. Kulingana na ukweli (Neno la Mungu – Biblia) sisi wana wa Mungu ni “washindi” na zaidi ya washindi, katika mambo yote (Warumi 8:37; 1Wakorintho 15:57). Kulingana na Ukweli wa Neno la Mungu, watu wa Mungu tumeshabarikiwa na kukabidhiwa vitu vyote tunavyohitaji kwa ajili ya maisha yetu yote ya mwilini na rohoni (Efe 1:3; 2Pet 13-4). Kama ni ushindi juu ya dhambi na dunia, uwezo huo tumeshapewa na Bwana. Mtu wa Mungu akikumbwa na tamaa za dunia hii, ina maana kwamba, yeye mwenyewe ameruhusu au amekubali kumtii shetani kuliko Mungu (Wagalatia 1:3-4; 1Yohana 2:15-17). Kama ni ushindi dhidi ya nguvu za giza, mapepo na wachawi; Mungu amekwishatupa uwezo huo wa kuwashinda watenda kazi wote wa ibilisi shetani (Wakolosai 1:13; Luka 10:19) Kama ni ushindi katika afya, tumepewa na tumeponywa tangu damu ya Yesu ilipomwagika msalabani kwa ajili yetu, na kwa kupigwa kwake sisi tulikwishaponywa tayari (1Petro 2:24; Mathayo 8:17). Kama ni jambo la uchimu na utajiri, watu wa Mungu tulkwishafanywa matajiri na Kristo, kwa kifo chake. Yeye alichukua umaskini wetu akatupa utajiri wake (2Wakorintho 8:9; 2Wakorintho 9:11). Kama ni suala la akili an hekima, watu wa Mungu tumekwishapewa uwezo mkubwa wa kiakili na fikra, kwa Roho Mtakatifu wa Mungu anayeishi ndani yetu. Sisi wana wa Mungu tuna akili na ufahamu wa kiungu. (Isaya 11:2; Zaburi 111:10; Matendo 6:8-10; 2Timotheo 2:7) Kama ni baraka katika mikono yetu, tumekwishapewa na Mungu kwa ajili ya shughuli zetu (Kumbukumbu 28:1-8; Zaburi 1:1-3) Kama ni ulinzi juu yetu na nyumba zetu na mali zetu, Bwana amekwisha waagiza malaika zake watuzunguke kwa panga za moto, farasi, magari ya moto (kufanya ukuta mzito wa moto) kutuzunguka (Zaburi 34:7; 2Wafalme 6:15-17; Zaburi 121:1-8; Zaburi 91;1-11-12). SABABU ZA KUFELI NA KUSHINDWA Kila kitu ambacho watu wa Mungu tunachohitaji katika maisha yetu yote ya mwilini an rohoni, tumekwisha kupewa na Baba yetu aliye mbinguni, ili tuweze kuishi maisha ya ushindi katika kila eneo linalotuhusu au linalotuzunguka. Kama ukweli ndio huu basi, kwanini watu wa Mungu wengine wana maisha ya kushindwa na kufeli? Kwanini watu wa Mungu wengine wanaishi maisha ya kuhangaika na kukosa? Ni lazima kuna sababu. 1 KUTOKUJUA Mungu anasema watu wangu wanaangamia (wanateseka na kuhangaika) kwasababu ya kukosa maarifa (ufahamu na ujuzi wa mambo niliyokwisha watendea) … japo wana bidii nyingi lakini wana bidii bila maarifa (wanapoteza nguvu nyingi katika maisha) (Hosea 4:6; Warumi 10:2) Ndio maana Paulo alikuwa anawakazania sana wanafunzi wake ili wapate Roho ya hekima na ufunuo, ili wapate “Kujua“ mambo tuliyokwisha kupewa na Mungu kupitia Yesu Kristo. Alimwambia Timotheo hivi, yafahamu sana mambo haya… (2Tim 2:7). Ndugu yangu, mambo usiyoyajua, hutaweza kuyapata; hayatatendeka maishani mwako. Kujua ndio mwanzo, ndio ufunguo wa kuyafungulia ili yaweze kuja kwako. ndio maana tunaambiwa Neno la Kristo likae kwa wingi katika mioyo yetu, kwa hekima yote … kuyajua maandiko matakatifu kunatuhekimisha ili tupate ufahamu wa haki zet na baraka zetu (Wakolosai 3:16; 2Timotheo 3:15-17) Ukitaka ufahamu na ujuzi, soma kwa bidii Neno la Mungu. Pata maarifa. 2 KUONA VIBAYA Kutokujua kunasababisha kuona vibaya. mtu asiyejijua kuwa yeye ni shujaa, atajiona dhaifu. asiyejijua kuwa yeye ni mzima, ayajiona mgonjwa. asiyejijua kuwa yeye ni mbarikiwa, atajiona ni maskini. Soma vizuri habari ya wana wa Israeli kitabu cha Hesabu sura ya 13 na 14 yote, utaona jinsi wana wa Isreali walijiona wao ni kama panzi mbele ya wenyeji wa Kaanani. Hii ni kwasababu hawakujua vizuri na kwa uhalisi, uwezo wa Mungu aliye pamoja nao, japo waliyaona matendo yake ya ajabu. kutokujua kunasababisha kuona vibaya. Hii ndio sababu iliyomfanya Mtume Paulo atuombea Wakristo tupate kufunguliwa katika macho yetu ya ndani, ili tuweze kuona vizuri, mambo ya rohoni. tukiona vizuri, tutapata ufahamu sahihi wa jinsi tulivo rohoni na jinsi tunavyotakiwa kuwa katika mwili (Waefeso 1:15-19). Gideon alikuwa anajiona yeye ni dhaifu na muoga lakini Mungu akimuangalia anamuona yeye ni shujaa, na ndio maana Mungu alimwita “ewe shujaa” japo kuwa yeye Gideoni alikuwa katika maficho kwa hofu ya maadui. Soma vizuri habari hii katika (Waamuzi 6:11-14) Bwana akamwambia “enenda kwa nguvu zako”. Maana yake ni kwamba, kumbe Gideoni alikuwa na nguvu za kutosha ndani yake, lakini hakujua! Kutokujua kunaweza kukunyima kusonga mbele. kutokujua kulimfanya ajione mnyonge mbele ya maadui wao. Mungu akusaidie kujiona sawa sawa na yeye anavyokuona na sio kama unavyojiona wewe Kama utatumia mwanga wa manjano ndani ya nyumba yako, vitu vyote vitaonekana ni vya manjano. Kama ukitumia mwanga mwekundu, vitu vitaonekana ni vyekundu. Vivyo hivyo katika dunia, Yesu anasema kwamba yeye ndiye nuru (mwanga) wa ulimwengu (Yohana 1:7-9) Tukimtumia yeye kuangalia mambo yetu, yataonekana vizuri kuliko tunavyoyaona sasa. Yesu ni Neno (Yohana 1:1-4; Ufunuo 19:11-13). Tumia Neno la Mungu (mwanga bora na halisi) kutazamia maisha yako, utayaona kama Mungu anavyoyaona na si kama wewe unavyoyaona. Kwa Neno la Mungu, Hutajiona mgonjwa bali mzima; hutajiona maskini, bali tajiri; hutajiona dhaifu bali hodari. soma sana Neno la Mungu ubadilishe unavyojiona. Kuona sawa sawa kutakuokoa na jambo lifuatalo.

Comments