HAWA WALIFUNGWA KWA AJILI YA YESU LAKINI HAWAKUMWACHA YESU




PASTOR BEHNAM IRANI AKIINGIZWA MAHAKAMA YA 26 REVOLUTIONARY COURT AMBAPO ALIFUNGWA KWA KUONEWA KWA SABABU YA KUMTANGAZA YESU.

ALIREZA SEYYEDIAN BAADA YA KUTOKA GEREZANI

Kama watu wa MUNGU tuliompa BWANA YESU maisha yetu wakati mwingine tunaweza kupita kwenye vikwazo vingi na wakati mwingine kuonewa na wenye mamlaka kisa tu tunamtangaza YESU kwa mataifa yote.Lakini licha ya hayo yote kama kweli unaujua uzuri wa BWANA YESU huwezi kurudi nyuma na kuwa mpagani eti tu kwa sababu ya kukwazwa. Bwana Alireza Seyyedian miaka 37, Amekua mkristo tangu 2006 na  decenber 2011 alifunga miezi 6 kwa kosa la kuwambia watu waache dhambi na wampe YESU maisha yako.Nudgu Behnam Irani miaka 41 ameokoka tangu 1992 na amekuwa Mchungaji tangu 2002 lakini katika huduma yake ya injili amefungwa zaidi ya mara 2 bila kosa lolote. hii ni mifano michache tu ya wakristo wengi wanaonyanyaswa kote ulimwenguni kwa sababu tu ya kumtangaza BWANA YESU kwa mataifa yote ili wanadamu wapate bure uzima wa milele ulio katika YESU KRISTO pekeyake, kumbuka Yohana 14:6 Biblia inasema  {YESU akasema, Mimi ndimi njia ,na ukweli na uzima; mtu haji kwa BABA ila kwa njia ya mimi} pia Matendo 4:12 {Wala hakuna wokovu kwa mwingine awaye yote, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo} ndugu bila YESU hutaingia katika uzima wa milele hivyo ni wakati wa kumpa yeye maisha yako, Licha ya kanisa kuwa katika kipindi kigumu ambapo lakini injili inahubiriwa kila sehemu na watu maelfu wanaokoka.

PASTOR BEHNAM IRANI
KUOKOKA WANAOKOKA WATU WA AINA ZOTE KWANI MUNHU NI WA WOTE WENYE MWILI

Comments