HERI ZA MWAKA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MARAFIKI WA MAISHA YA USHINDI {2}

BWANA YESU asifiwe.
Tunaelekea kusherekea ukumbusho wa kuja kwa ukombozi duniani maana hakuna uzima popote ila ni kwa YESU KRISTO {Yohana 14:6,YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. }. 
 
=Ndio maana dunia nzima ni shangwe na furaha kwa tukio ambalo limetokea miaka zaidi ya 2000 iliyopita ambapo siku YESU anazaliwa malaika ambao ni jeshi la mbinguni walishangilia na kumsifu sana MUNGU
{Luka 2:8-14,Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Malaika wa BWANA akawatokea ghafula, utukufu wa BWANA ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo BWANA. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe.Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu MUNGU, na kusema,Atukuzwe MUNGU juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. }

Siku hiyo hiyo YESU mwanaume wa ajabu anazaliwa watu wenye heshima na watawala walimsujudia 
{Mathayo 2:11, Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. }

hao walijua kuwa aliyezaliwa ni MFALME wa wafalme na BWANA wa mabwana.

Pia YESU alizaliwa kwenye hori la ng'ombe ashilio la kwamba wanyama wapumzike maana hakuna tena sadaka ya kuteketezwa kama ilivyokuwa zamani maana YESU ni dhabihu idumuyo milele ili watu wasamehe dhambi zao na kuurithi uzima wa milele bure kupitia yeye {Waebrania 9:12-15, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake KRISTO, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa MUNGU kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu MUNGU aliye hai? Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele. }.

Tunasherekea christmas kwa kumwabudu MUNGU na kuonyesha upendo kwa wengine na kuhakisha kwamba YESU anatenda jambo jipya mioyoni mwetu ili tuzidi kuishi katika neema yake maana kwa ajili yake na kwa neema yake alituhamisha kutoka kwa shetani na sasa tuko huru mbali na kuonewa na wachawi na hata nguvu zozote za giza.

Nampenda YESU KRISTO maana ndiye pekee Mwokozi wa watu wote.
Ubarikiwe na nakutakia Sikukuu njema ya kuja kwa ukombozi duniani.


 HIZI HAPA NI BAADHI TU YA SALAMA ZA KUTAKIANA HERI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA KUTOKA KWA WATUMISHI WA MUNGU PAMOJA NA MARAFIKI NA WASOMAJI WA BLOG HII.
LUCAS MAGARE WA MWANZA NAWATAKIA HERI ZA CHRISTMAS NA MWAKA  MPYA ABDULAAZIZ ESIR AL TAMIMU ,AZORI MHOJA,BONIPHACE MAGARE,DANIEL MASHENENHE,GIRBERT HOAL,GODYFREY ISAAK,JACKOB MASHENENHE,JAMES MASANYIWA,JAPHARY MWAMBETE,JAPHET FUMBUKA,JOHN MASIGE,MAMA YUSUPH CATERING,MICHAEL MAGAMBE,MORANG`A JOSEPH,MOURICE NUHU,PAUL MICHAEL,PENDO LUCAS AMBAYE NI MKE WANGU,SHADRACK MASSOY, SOSPETER SIMON NDABAGOYE,VENANCE NUSDER PIANIST,VENANCE VICTOR,YUSUPH MHOJA,ZAKY MADDY,DANIEL MABINA PIA WEWE MWENYEWE USIJISAHAU.MUNGU awabariki sana na tusherekee kwa kutenda matendo mema
LUCAS MAGARE
MR & MRS LUCAS MAGARE

JUNIOR BARRY WA KIBOSHO KILIMANJARO NAWATAKIA HERI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA MARAFIKI ZANGU WOTE NA WAPENDA INJILI WOTE NA MUNGU AWABARIKI SANA NA TUSHEREKEE KAMA WATAKATIFU WA MUNGU TULIYE NA KRISTO YESU MIOYONI MWETU

Comments