JE SHETANI ANA UHALALI KATIKA MAISHA YA WANADAMU?

wapendwa katika Bwana,kitu ambacho mwanadamu aliumbwa nacho ni nguvu ya kuamua.namaanisha hivi,unachokiamua aidha mfumo wa maisha yako unayoishi yatajulisha uko kwa Mungu au gizani.
Kwa watu wa Mungu huwa tumezungurushiwa uzio/boma{mhubiri 10:8}wigo wa ulinzi ambao haumruhusu Shetani maishani mwetu.Sasa jambo la kujua ni kwamba,Wigo huo haukuzuii kutoisikia sauti ya Shetani,utamsikia ila hawezi kukugusa.Sasa kinachotokea Shetani atatumia kufanya kila njia ili apate kiupenyo cha ule wigo aingie ndani yako..je wigo huu tunaubomoaje?..ni kwa kutokuwa mvumilivu,kutosamehe na kuruhusu hasira tena kwa kusikitisha mtu wa Mungu unakubali kukasirishwa na mtu asiyemjua Mungu.
NOTE:Shetani hutumia watu ambao hawana uzima ndani yao kama agenti wa kukuangusha.kuwa makini.
UHALAKI WA SHETANI KUKUTAWALA.
1.kwa kufanya dhambi za Amali.
amali(kwa hiari yako).yaani unajua unachokifanya i.e ulevi,uzinzi,matusi,uongo n.k.
2.Kwa njia ya ushirikina
3.Kwa kurithi mikoba.unaweza kurithishwa bila kujua,na hii hutokea kama hauna Yesu.
4.Roho ya kutosamehe.huu ni mlango ambao shetani anautumia sana.Filemoni 1:8-20,filemon mambo yake hayakwenda vizuri sababu hakumsamehe Onesmo.
5.Majanga mazito.mfano usaliti,kufiwa n.k
6.Maunganiko ya nafsi sio kwa utukufu wa Mungu.
mfano:maagano ya damu,uzinzi(1kor 6:16-18)unakuwa nafsi moja ya uzinzi.
7.Kuathiriwa na tabia mbaya(being adicted)mfano:Ulevi,ulafi wa kula na uongozi na ulev wa picha chafu za ngono..
Mungu atusaidie tusimane imara tusimruhusu shetani.MUNGU awabariki sana.by RAPHAEL MBOGO

RAPHAEL MBOGO
maombezi huondoa nguvu zote za giza na kumwacha mtu huru



Comments