JINSI YA KUIFAHAMU MIUJIZA YA MUNGU

Ili kuifahamu na kuipambanua miujiza ya mashetani.itakuwa vema kujifunza alama zitakazotuwezesha kuifahamu miujiza ya Mungu.Tukiweza kufahamu namna ya kupambanua miujiza ya Mungu,itakuwa ni rahisi kufahamu kinyume chake,na kuifahamu miujiza ya mashetani.ZIKO ALAMA KUMI (10) za kutuwezesha kuifahamu miujiza ya Mungu.Alama zote hizi,lazima zionekane katika huduma yoyote inayotumiwa na Mungu kufanya miujiza.Tukiziona alama zote hizi kumi katika huduma yoyote ya miujiza,tujue huduma hiyo niya Mungu,na hatupaswi kusema mtu huyo wa Mungu anatumia roho chafu au anatoa pepo kwa Beelzebuli,mkuu wa pepo.Alama hizi kumi ni hizi zifuatazo:-
1.      .Mtu anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, lazima mwenyewe awe ameamini na kuokolewa; akikiri mwenyewe wokovu ulio katika Kristo Yesu, na kuushuhudia ishara au miujiza ya Mungu, hufuatana nao WAAMINIO tu, au waliookolewa (MARKO 16:17).Mtu yeyote ambaye hajaokoka, hawezi kufanya miujiza inayotokana na Mungu.Miujiza anayoifanya mtu yeyote ambaye hajaokoka, ni miujiza ya shetani.
2.     .Huma yoyote ya miujiza ya Mungu, lazima iambatane na Biblia au Neno la Mungu, kwa kuwa Neno la  Mungu ndiyo dawa ya ugonjwa na tena ndilo linalofanya miujiza(ZABURI 107:20; MITHALI  4:20-22; YOHANA  6:63). Mtu anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, ataiamini Biblia na kuifanya kuwa msingi wa utendaji wake wote. Huduma yoyote ya miujiza isiyoambatana Biblia, inatokana na Shetani.
3.      Huduma yoyote ya miujiza inayotokana na Mungu, LAZIMA iambatane na KUHUBIRI NA KUFUNDISHA Neno la Mungu. Mtu yeyote anayedai kwamba yeye hakupewa kuhubiri Neno, ila amepewa karama ya kutenda miujiza tu, huyo anatumiwa na Shetani (LUKA  4:18; 5:17; 9; 8:1-2; MATHAYO  10:7-8). Huduma yoyote ya miujiza ya Mungu, lazima iambatane kuhubiri kwamba watu watubu dhambi zao na kuziacha, na kuokolewa. Kinyume cha hapo, ni huduma ya Shetani (MARKO  4:6;12-13).
4.      Miujiza yoyote ya Mungu, LAZIMA ifanyike kwa jina la YESU (LUKA 10:17; MATENDO 4:30; MARKO 16:17; MATENDO 3:6;  4:10;  3;13,  16, 16:18).
5.      Miujiza yoyote ya Mungu, hutumika kuwaleta watu kwa Bwana Yesu na kuwafanya wawe wanafunzi wa Yesu, na kuwafundisha kudumu katika kanisa linalohubiri wokovu (MATENDO 5:12, 14; 2:41-43;  6:7-8; 8:5-8, 12). Miujiza isiyo na lengo hili ni miujiza ya Shetani.
6.      Mtu yeyote anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, lazima afanye huduma yake kwa kushirikiana na makanisa yanayohubiri wokovu, ili apate kutoa ripoti ya huduma yake inavyokwenda na kuwajibika (MATENDO 14:27; 21:17-19; 1WAKORINTHO 14:29).
7.      Miujiza ya Mungu, hutusogeza katika kumtumikia Yesu Kristo na kushika maagizo yake, na kutufanya kuwa watakatifu kama yeye alivyo mtakatifu. Miujiza yoyote inayoambatana na maagizo yoyote yaliyo kinyume na Neno la Mungu, kama kutumia sanamu za watakatifu, kufukiza uvumba, kutumia rozari au maji ya Baraka, kuzuru makaburi, kuwaomba wafu tuwaombee n.k; haitokani na Mungu (KUMBUKUMBU 13:1-4).Mafundisho ya mtu anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, hutufundisha kuwa watakatifu, na kuwa mbali na mapenzi ya Mataifa. Wote waliotumiwa sana na Mungu kufanya miujiza kama Paulo, Petro, Yakobo na Yohana, walifundisha hivyo (WARUMI 12:1-2; 1YOHANA 2:15-17; 1 PETRO 1:14-16; 2:12; 4:2-3; YAKOBO 4:4; 1 WAKORINTHO 4:3-4).
8.     Miujiza ya Mungu hutolewa bure, hainunuliwi (MATHAYO 10:8; 2 WAFALME 5:14-16; DANIELI 5:16-17; 1 WAFALME 13:6-8; MATENDO 8:18-20). Namna yoyote ya kuomba hela ili kununua muujiza ni kinyume na mpango wa Mungu .Hata kama tutaona wakiuza vitambaa,leso na sabuni zilizoombewa ili zitusaidie, hatuna budi kujua mapanzi ya Mungu kwa watumishi wake ni kutoa huduma ya maombezi bure. Huduma yoyote inayochangisha mchango au kiingilio kwa ajili ya semina ya Neno la Mungu hiyo siyo huduma ya kimungu, ni huduma ya Shetani. Mungu anataka injili iwafikie watu wote.Mfano 1 wa huduma ya shetani ni huduma ya babu wa Loliondo. Bila kutoa sh: 500  usingeweza  kupata msaada.Pia miujiza ya Mungu inatokana na Neno la Mungu kama tulivyoona hapo juu. Miujiza ya Mungu inakuwa na lengo la kuwaleta watu kwa Yesu.Watu wanaokuja kutafuta msaada kwa Yesu sharti waongozwe kutubu dhambi zao
kwanza ili kuwapatanisha na Mungu kwa ajili ya kufungua mlangio wa Miujiza yao.
9.       Miujiza ya Mungu humtukuza mwana wa , Yesu kristo (YOHANA 11:4), wale wanaotumiwa na Mungu kufanya miujiza ya Mungu hubaki wanadamu na wao kukiri hivyo, na kumpa Mungu utukufu(MATENDO 14:8-18). Tunapomuona  mtu akichukua utukufu kana kwa mba yeye ndiye anayetenda miujiza ndipo tunatambua kuwa huyo si mtumishi wa Mungu.
10.      Maisha ya mtu anyetumiwa na Mungu kufanya miujiza yanapaswa kuwa sawasawa na Neno la Mungu. Watu wanaotumiwa na Shetani kufanya miujiza, huambatana na dhambi NNE zinazoonekana upesi-uzinzi au uasherati (1 WAKORINTHO 6:15-17), maneno ya kihuni (YAKOBO 3:10-12), maisha yaliyo sawa na mataifa katika kuvaa na kutenda (WARUMI 12:2;  1 PETRO 2:12; YAKOBO 4:4), maisha yasiyo na uaminifu katika masuala ya fedha na kusema uongo (NEHEMIA 7:2)

Comments