KUSAMEHE NI MUHIMU SANA ILI MUNGU AJIBU MAOMBI YAKO


MACJAY ZION
"Moyo wa kutosamehe,huleta madhara kukatika kwa ushirika kati yako na Mungu..Ushirika ni mawasiliano pande mbili,yaani kati ya mtu na Mungu,na Mungu na mtu,ivyo kwa sababu ya kuto kusamehe yale mawasiliano yako na Mungu yanakatika..Pia utendaji uliokuwepo Utaondoka.Hutaona nguvu za Mungu zikifanya kazi,hutaona upako wa Mungu,wala hutaona mafanikio ya MUNGU,wala utendaji wa Mungu katika Shughuli zako,ndoa yako,masomo yako wala chochote ufanyalo...Isaya 59:2"Lakini maovu yenu yamewafarakisha ninyi na Mungu wenu,na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone hata hataki kusikia" Kutokusamehe ni sawa na dhambi zote uzijuazo kama uzinzi,uögo,wizi na mengine Mengi,tumekua tunadhania kutokusamehe si dhambi lakini napenda ujue kuwa,MOYO WA KUTOKUSAMEHE NI DHAMBI KAMA DHAMBI NYINGINE,samehe kama BABA YAKO WA MBINGUNI ANAVYO SAMEHE,
1YOH 1:5-7 "Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake,na kuihubiri kwenu,ya kwamba Mungu ni Nuru,wala giza lolote hamna ndani yake,Tukisema ya kwamba twashirikiana naye,tena tukienenda gizani,twasema uongo,wala hatuifanyi iliyo kweli,bali tukienenda Nuruni,kama yeye alivyo katika Nuru,twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu,mwana wake,yatusafisha dhambi yote" Ndugu yangu mpendwa hauwezi kufanikiwa bila kusamehe,hauwezi ukaponywa bila kupokea na kusamehe rafiki na jamaa zako kwani hata Mungu husamehe kwanza na ndipo kukuponya Zaburi 103:3 "Akusamehe maovu yako yote{DHAMBI ZAKO ZOTE} na kisha akuponya magonjwa yako yote," haijalishi unaumwa nini Yesu kristo huponya,haijalishi vipimo vimesema nin,Yesu amesema ndiyo katika hali unayopitia yeye anakwenda kukuinua ,tazama amesema atafanya njia pasipo kuwa na njia,Amini Mungu amekuinua,amini amekuponya,amekubariki pale unapokwenda kusamehe Mungu aweke mkono wake katika Jina la Yesu kristo aliye hai. MUNGU awabariki sana. B y Macjay Zion

Comments