MAANA YA KANISA

WATU WAKIWA KWENYE SEMINA YA NENO LA MUNGU HUKO MWAKAJE ZANZIBAR



Kanisa maana yake ni nini?
Neno kanisa linatokana na neno la asili katika lugha ya kiyunani linaloitwa “ECLESIA” lenye maana “walioitwa na kutoka miongoni mwao”. Kanisa linafananishwa na wana wa Israeli walioitwa na kutoka katika utumwa wa Farao kule Misri na kuanza kwenda Kanaan kupitia jangwani.. Walipokuwa jangwani waliitwa kanisa la jangwani (MATENDO 7:38). Kwa msingi huu kanisa leo ni wale wote walioitwa na kutoka katika utumwa wa dhambi.Kama vile wana wa Israeli walivyokuwa watumwa wa Farao vivyo hivyo na watenda dhambi ni watumwa wa Shetani. Watu wote wote waliookoka kwa kutoka katika utumwa wa Shetani koye duniani bila kujali dhehebu lake la dini , wote kwa pamoja wanaitwa kanisa. Watu wote ambao majina yao yamefutwa katika kitabu cha hukumu yakaandikwa katika kitabu cha uzima mbinguni hao ndiyo kanisa.. Hilo kanisa ndilo linatajwa kwamba litanyakuliwa kama tukio la kwanza katika matukio ya mwisho ambayo hayako mbali sasa.MUNGU awabariki sana

YESU ANAOKOA WATU WA AINA ZOTE
YESU ANAOKOA
BIBLIA TAKATIFU NDILO NENO HAI LA MUNGU

Comments