MAJINA YA MUNGU YANAVYOWEZA KUTENDA KAZI NDANI YA MAISHA YETU

Kwani wakati nikiwa na uhitaji / shida na kimbilia kuita Jehovah-Jireh yaani Mungu anayetoa kadri ya uhitaji wangu. Ukisoma Wafilipi 4:19 Paulo anawaandikia watakatifu wa Kristo Yesu walioko Filipi akiwashukuru kwa wao kumpelea msaada wa vitu mbalimbali na kuwaambia kuwa Mungu ambaye yeye ni mtoaji / mgawaji wa vitu atawapatia yale yaliyo hitaji la mioyo yao.
Hivyo basi ukiwa na shida ukiwa na uhitaji ndani ya maisha yako basi ujue kuwa yuko Mungu ambaye yeye anaoutoshelevu wote ambaye amekamilika katika kila nyanja ni mimi na wewe kujitoa kwa kuliita tu hili jina lake katika maombi yetu nae anafanya /anatugawia.
Nikipatwa na mashambulizi ya magonjwa yaletwao na yule mwovu naiita jina la Jehova Rafa yaani Mungu mponyaji. Soma 2korintho 4:7-17 magonjwa yanaletwa na hofu, uchungu kutokusamehe haya yote kwa pamoja ndio yanayofanya miili yetu kuwa dhoofu Mtume Paulo anasema hivi ktk mstari 8-10 kuwa hata tukipwata na jambo gani miili yetu inatiwa nguvu kwani kwa kufa kwake Yesu Kristo pale msalabani ni ili miili yetu itiwe uzima, kwani aliyabeba madhaifu yetu yote na kwa kupigwa kwake sisi tumepona pia ukisoma kwenye mstari wa 16 tunaambiwa kuwa hatulegei kwa kuwa utu wetu wa nje unapochakaa utu wetu wa ndani unafanywa upya kwa hiyo tusichoke kumwiita Jehova Rafa maana yeye anaanza uponyaji wa ndani halafu anakuja nje na hii itakufanya kuwa kiumbe kipya kabisa.

Pale ninapokwa na mashaka / hofu kuu imenitawala ndani ya maisha yangu basi liko jina kuu niitalo Jehova Shalom yaani Mungu wa Amani. Soma Yohana 16:33 Bwana Yesu alikuja kuleta upatanisho kati yetu sisi na Mungu na pia kuleta amani kwani yeye ni mfalme wa amani ukiwa naye hakuna shaka ndani ya maisha yako japo Yesu anatumbia ktk mstari wa 33b kuwa hapa ulimwenguni dhiki zimo na zitatupata lakini tuwe imara tusikate tamaa kwani kama yeye ameushinda ulimwengu na sisi tutashinda vita. Alikuja ulimwenguni kuleta Amani.
Ninapokuwa mpweke sina mahali pa kukimbilia ninalo jina ninalokimbilia kuliita nalo ni Jehova Shama yaani Mungu ambaye yupo. Mungu yupo kila mahali, kila wakati, kila siku milele na milele hivyo hakuna haja ya kuwa mnyonge, mkiwa kwani yeye yupo na anasikia ukisema naye anakujibu, ukimtafuta unampata. Anakusubiri tu uliite jina lake naye anasema niko hapa anakupa pumziko la moyo la kweli upweke hautakuwepo tena. Mungu wetu yupo jana, leo, kesho hata milele.
Mungu wetu ni Mungu mkuu mwenye uweza wote mwenye upendo usiopimika anatujua sisi kabla hata ya misingi ya ulimwengu kuwepo alitujua hata kabla hatujazaliwa anajua kila jambo katika maisha yetu yeye anaona mwisho tangu mwanzo hivyo ni sisi kujifunza kuliita jina lake kila wakati kutokana na uhitaji wetu .
Ukisoma Ufunuo Wa Yohana 1:8 unasema hivii MIMI NI ALFA NA OMEGA, MWANZO NA MWISHO, ASEMA BWANA MUNGU, ALIYEKO NA ALIYEKUWAKO NA ATAKAYEKUJA , MWENYEZI.
Tujifunze kumtegemea Mungu katika mambo yetu yote, si wakati wa dhiki tu hata kwenye furaha.

Comments