Maombi
ni neno ambalo limetumika sana katika Biblia. Mara nyingi maombi
yanafanyika makanisani, kwenye mikutano mbalimbali ya injili, katika
vikundi mbalimbali, na hata kwa mtu binafsi. Maombi yana umuhimu mkubwa
sana katika huduma. Na yakipata nafasi mafanikio makubwa yanakuwepo.
Maombi ya mtu binafsi nayo pia ni muhimu sana. Mimi mwenyewe nimeona
maombi yakifanya mambo mengi makubwa sana katika maisha yangu.
Yote ambayo Mungu ameyafanya na anaendelea kuyafanya katika maisha
yangu hata sasa yamenifanya mimi binafsi kusikia msukumo mkubwa na wa
kipekee sana moyoni mwangu wa kutaka kujua zaidi na zaidi kuhusu maombi.
Hili ni jambo kubwa sana na linatufaa sisi sote ambalo Mungu mwenyewe
ameliweka ili tupate nafasi ya kuwasiliana naye. Mungu ameiweka njia hii
ya maombi ili apate kutusikiliza wakati tunapozungumza naye. |
|
Comments