MPANGO WA MUNGU NA AGIZO LA MUNGU KWA MME KATIKA FAMILIA

Mume ni KIONGOZI. Uongozi usio wa mabavu bali uliotawaliwa na UPENDO.

1. KIONGOZI: Waefeso 5:23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama KRISTO naye ni kichwa cha Kanisa, naye ni mwokozi wa mwili.

i) MUNGU amempa wajibu mume wa kuwa kiongozi
ii) Mume ndiye anayehusika kuwa na kauli ya mwisho katika maamuzi
iii) Mume awe mwajibikaji na kusimama katika zamu yake ipasavyo, na siyo kuwa na kiburi
iv) Mume aonyeshe uongozi wake akifuta kielelezo cha KRISTO.

2.UPENDO: Waefeso 5: 25 Enyi waume, wapendeni wake zenu kama KRISTO naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake.

i) Upendo wa mume kwa mkewe ufuate kielelezo cha KRISTO
ii) Upendo wa kujitoa, upendo wa agape
iii) Mume anatakiwa ampende mke wake kana anavyojipenda mwenyewe. Waefeso 5:28-30.

Upendo wa mume kwa mkewe unaonekana katika mambo yafuatayo:

1. Mume ni mtunzaji wa familia.
Mwanzo 1:27-28, Mwanzo 3:17-19, 1Timotheo 5:8, 2Wathesalonike 3:6-10.

2.Mume ni mchungaji wa familia.
a. Mume anawajibika kuiongoza familia yake kiroho
b. Mme ana ushawishi mkubwa katika familia
c. Mume anawajibika kwa lolote litakalotokea katika familia yake

3. Mume ni mlinzi wa familia
a. Kimwili
b. Kisaikolojia
c. Kifalsafa      d. Kiroho



Comments