MWANZO WA HUDUMA YA MCHUNGAJI STEVEN MWAKATWILA



Mwl Mwakatwila 1
Mimi Steven Gwasa Anthony Mwakatwila pamoja na Mke wangu Beth Tunamshukuru sana Bwana Yesu Kristo aliyetuokoa na kutupa nafasi ya kuwa Watoto wake na pia kutuita ili tupate kumtumikia katia maisha yetu aliyotupatia kuishi hapa Duniani, Bwana Yesu Kristo aliniokoa tarehe 19-11-1995, jioni katika mkutano wa injili uliofanyika katika viwanja vya ccm Tukuyu, Mkutano huo uliandaliwa na watu wa Tukuyu Christian Fellowship, Mtumishi wa Mungu Mmanyi toka Dar es salaam alihudumu katika mkutano huo wa Injii, Mke wangu Beth pia amempokea Bwana Yesu Kristo, alimpokea mwaka 1997, Katika semina iliyofanika mjini Tukuyu,na mtumishi C.Mwakasege toka Arusha alihudumu katika semina hiyo.

Mimi ni mfanyakazi katika Shirika liitwalo  Here’s Life Tanzania, nikiwa Msimamizi wa Kanda ya Nyanda za juu kusini Magharibi,  Makao yetu yapo Mjini Mbeya, Baba yangu ni askari mstaafu wa jeshi la Mageleza anaitwa Anthony Gwasa. Mwakatwila yeye aliokoka mika ya sitini, Mama yangu anaitwa Lideya Mwakibete, pia amempokea Yesu kamaBwana na Mwokozi wa maisha yake, tupo sita katika Familia ya Mzee Mwakatwila, nikwa motto wa tatu na mzaliwa wa kwanza wa kiume,nina dada zangu waili wa kwanza anaitwa Sara,wa pili ni Upendo, na nina wadogo zangu wa kiume wawili nao ni Daved, na Geofrey, wa Mwisho kwa sasa ni marehemu aliitwa Neema, Mke  wangu anatokea katika familia ya Mzee Seth M wang’onda, Baba pia ni mstaafu kutoka shirika la mapato TRA.
Mimi na mke wangu tunamshukuru Mungu aliyetuupa watoto Watatu, Mtoto wetu wa Kwanza anaitwa, Birgita, wa pili Daniel, na watatu ni Priska

Huduma yetu

Baada ya kumpokea Bwana Yesu Kristo, Mungu aliweka ndani yangu wito wa kumtumikia, na ninamshukuru kwa kunipa ofisi ya Ualimu ndani yangu, na kuniambiwa wazi kuwa anataka Nifundishe Watoto wake na watu wake, na tulianza utumishi huo rasmi  mwaka   2006, baada yakupitishwa na Bwana katika maandalio  mbalimbali,   ya kiutumishi, Mwaka huo nikiwa Lilongwe Malawi kikazi ndipo Bwana aliposema nami kuwa sasa  “Lundi Tanzania kwa kazi ninayotaka uifanye nayo ni ya kufundisha Watoto wake yaani Kanisa lake, na Watu wake pia kuwaombea  watu na nchi yetu” ni kweli Toke wakati huo nilipoludi tu nchini kila kitu kilibadilika,  na ndipo Mimi na mke wangu tulpoanza kazi hii ya kufundisha neno la Mungu atupalo kulifundisha kwa wakati, na Mungu ameweka kitu ndani yetu nacho ni  kuwahudumia Watoto wake yaani watu waliomwamini Yesu waliopo mahali popote pale, tunafanya kazi mahali popote pale tupatapo mialiko ya kufundisha neno lake bila kujari dhehebu gani ilimladi tumepata kibari kutoka kwa Bwana wa huduma hii Yesu Kristo.
 ''Hata nitakapokuja ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha…. ''(1Timotheo 4:11)
BethTulianza kufanya huduma hii kwa kufundisha watu wawili tena wa familia moja, baadaye wakaongezeka kuwa thelathini, mpaka hii leo tunafundisha maelfu ya watu katika nchi hii ya Tanzania, tumepata mialiko mingi kwa kufundisha katika makusanyiko kwenye mashule  ya sekondari, vyuo mbalimbali, kambi za vijana, Pia semina za Watumishi wa Mungu Wachungaji, Wainjilisti Waombaji na hata katika madhehebu mbalimbali. mwaka 2006 tulianza kufanya huduma ya kufundisha kwa kushirikiana na Wapendwa kutoka madhehebu mbalimbali, walijikusanya kama kamati na kuandaa semina mjini mbeya, na kukodi ukumbi wa St Marys,na watu wasiozidi, 50 walihudhuria semina hiyo , na Bwana alitupa somo lenye kichwa KUWEKWA HURU, hapoa ndipo ulikuwa mwanzo wa huduma hii kuenea sehemu mbalimbali, mwaka 2007 kamati hiyo iliandaa tena semina  na kukodi tena ukumbi  wa Uhasibu mjii mbeya, watu wapatao mia 200, wakiudhuria, na hapo Bwana alianza kufungua milango ya kwenda mikoa mbalimbali ya nchi hii kufundisha semina za neno la Bwana,  mwaka 2008, kamati hiyo iliandaa tena semina Mbeya mjini na safari hii tulifanyia kwenye viwanja vya Chuo Cha Otu mjini Mbeya.

Kamati ilitafuta miti na kuomba maturubai na kuezeka na kukodi viti pia walikubaliana kutengeneza jukwaa la chuma, walifanikiwa kutengeneza jukwaa hilo, tulikuwa na huduma nzuri sana, Bwana aliokoa watu wengi sana, na kuwaponya na kuwa fungua, na kuwafundisha, Mwaka 2009, tulianza kutengeneza darasa linalo hamishika, na kuwa na semina ambayo ilikuwa na watu wengi sana tulitengeneza hema la watu takribani 2,000 wakae lakini watu walikuja zaidi, na mwaka huu, 2010 tumekuwa na semina nyingi tokea mwanzoni mwa mwaka, na tuliendelea kuongeza darasa hilo na ili lifikie watu elfu tatu, lakini baada ya semina ya mwezi wa 7 mwaka huu wa 2010 , tumegundua kuwa tunahitaji sasa darasa lisilo pungua watu 5,000 hayo ndio mafanikio ya utumishi huu ambao Mungu ametupa, mwaka 2008, Mungu alitupa nafasi ya kuweka msomo kwa njia ya ledio, na pia kwanjia ya iitwayo Mbeya TV, tumekuwa na vipindi kila siku ya jumanne saa tatu mpaka saa nne katika ledio Bomba fm, pia mwaka 2010,tumekuwa na vipindi kwenye ledio Baraka fm, Ledio hizo zinafikia mikoa takribani nane na nchi mbili za Malawi na Zambi, kila wiki tumekuwa na semina hizo, na vipindi hivyo vyote tunanunua. Tunahitaji maombi yako sana.

Malengo yetu ni kuufikisha ujumbe wa neno la Bwana kwa kila mtu mahali popote pale Duniani. Nakukaribisha sana karibu tushirikiane katika utumishi huu kwa kutuombea kutushauri, na hata kwa hali na mali. ninamwamini Mungu kuwa Roho Mtakatifu atakufundisha, pia usisite kuwashiriksha watu wengine kile Mungu amekufundisha,pia utakapo pata nafasi kutushirikisha mahitaji yako ili tukuombee usisite kuwasiliana nasi, nasi tunakuahidi tutakuombea kwa Bwana na tunamuamini sana Yesu atakuhudumia, ikiwa pia unahitaji kuokoka usisite mpe Yesu maisha yako, na anza kutendea kazi mambo yale Bwana .

Bwana akubariki sana

Wako: Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila

Comments