NENO LA MUNGU, MAMLAKA YA MWISHO KWA MRISTO




Katika nchi, kisheria, katiba inaitwa sheria mama, Katika nchi, ni mamlaka ya juu zaidi naya mwisho kwa raia wote wa nchi. Nchi nzima wakati wote sharti iongozwe na katiba. Kwa mfano huu, kwetu wakristo, katika mambo ya ufalme wa Mungu Neno la Mungu ndilo sheria mama. Ni mamlaka ya juu zaidi naya mwisho kwa kila mkristo au yeyote  anayetaka kufanya mapenzi ya Mungu. Neno la Mungu ni mamlaka ya juu zaidi kuliko katiba za makanisa za kibinadamu au maelekezo ya kibinadamu yanayotokana na vikao vya viongozi wa dini walioko Ulaya au waliopo hapa nchini Tanzania. Siku ya mwisho tutahukumiwa sawasawa na Neno la Mungu na siyo maneno yoyote mengine (WARUMI 2;16). Hivyo Neno la Mungu ndiyo sheria mama katika mambo yote ya ufalme wa Mungu. Hukumu yote ya wanadamu wote itatolewa kwa  kuzingatia Neno la Mungu. Linasemaje.MUNGU awabariki sana

Comments