NILIPEWA PESA KAMA ZAWADI IKAGEUKA NYOKA

STELLA HAROUN WA TATU KUTOKA  KULIA NYUMA YA MAMA MWENYE MTOTO
BWANA YESU asifiwe, naitwa Stella Haroun niko Tanga na nimeokoka na nampenda YESU. ilikua january 2012 nikiwa nyumbani likizo baada ya kutoka chuoni Tabora nilikukua nasoma . Nikiwa nyumbani jirani na nyumbani na nyumbani kulikua na nyumba ambayo ilikua haijaisha ila likizo hii nilikuta imeshaisha na kuna watu wanaishi humo mwanamke mwafrica na mwanaume mzungu na hawa walikua ni mke na mme. baada ya kukaa wiki moja yule dada mke wa mzungu alikua anakuja sana nyumbani kwetu kuongea na mama na kila akinikuta alisema kuwa amenipenda sana kwani mimi ni msichana mchangamfu na mpole na baada kama ya wiki moja nyingine nikiwa nimebakiza wiki mbili niondoke alikua ananiulizia sana habari za chuoni na pia akaniahidi kabla sijaenda chuoni nikachukue zawadi kwake kwani amenipenda sana.Sikuwa na hofu wala kuwaza lolote maana huyu ni mwanamke mwenzangu nilikubali kwa kusema nitaenda kuchukua hiyo zawadi na alifurahi sana nilipokubali kwenda kuchukua zawadi hata kama sikujua ni zawadi gani.niliendelea na maisha ya likizo kama kawaida hadi ilipobaki siku moja kuondoka kwenda chuoni Tabora ndipo mida kama ya saa 3 usiku alipiga simu na kuniambia nifate hiyo zawadi na kwa kuwa siku hiyo mchumba wangu alikua amekuja nilimwambia anisindikize tukaondoka pamoja na mdogo wangu wa mwisho.Tulipofika pale kwa mzungu alinipa Tsh.10000 na ilikua noti moja tu tukaondoka akinitakia safari njema maana kesho yake ningesafiri kwenda chuoni, Tulipoondoka pale mchumba wangu aliniomba ile pesa na kusema tuiombee kwanza kwani yeye moyoni mwake ilikuja ishara kama kuna hatari fulani muda huo itatokea maana tulikua tumeokoka wote mimi na mchumba wangu na familia yangu wote na akaikamata ile pesa na kusema kama kuna hila yeyote ya shetani au manuizo yeyote basi katika jina la YESU KRISTO yasifanikiwe. tulienda hadi nyumbani na pesa hiyo nikampa mama ili anitunzie mama akaikamata na muda huohuo ile noti ya shiling 10000 ikageuka nyoka na tukaanza kukemea na kuvunja hila hila za shetani yule nyoka akageuka na kuwa tena pesa  na tulipoomba muda mrefu kidogo akatoka nyoka mwenye rangi tofauti na yule wa kwanza na muda huo wote ili pesa ilikua chini huku sisi tukiomba pembeni baada ya yule nyoka kutoka mama alisema basi pesa hiyo tunaweza kuitumia, niliogopa na kuikataa lakini mama akasema tumeshaoomba kwa jina la YESU na hakuna uchawi wala ushetani wowote utakaompata yeyote kati yetu nilimwambia anibadilishie anipe ya kwake na yeye achukue ili akakubali na mimi kesho yake asubuhi nikasafiri lakini nilipouliza kuhusu ile pesa mama aliniambia ilitumika kama kawaida na hakukuwa na tatizo lolote. Nilijifunza sana kwa tukio hilo maana sio kila mtu ana nia njema na wewe na wapo watu wengi hata ufahamu wao umechukuliwa na wachawi ila hawafahamu chanzo cha tatizo na tibaya ya tatizo ambayo ni maombezi kwa jina YESU KRISTO.MUNGU awabariki sana na kumpa YESU KRISTO maisha itakuepusha na hila mbaya zote za shetani na mawakala wake maana hata huyu dada alikua na nia mbaya na mimi hata kama sikujua alikua na lengo gani .

Comments