TABIA ZA MAPEPO NA MAJINI YANAPOMTOKA MTU





Luka 11:23 - 28
“Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutawanya. Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema, Nitairudia nyumba yangu niliyotoka. Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ikawa alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia, Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya. Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.”

Wapendwa Tusimame ndo mana Tunapewa/kuwekewa madarasa ya kukua Kiroho, ile ni kama mwanajeshi yuko kambini/depo akijifunza mbinu za kivita hata kujitambua na kuwa mkakamavu. Kwa hiyo kuombewa na kutoka kwa Mapepo/majini si tuishie hapo tuu, kujiami zaidi ni vyema.

Hii ni vita kama uonavyo katika neno hilo kwa ajili yetu kutufunza madhara yake wanapofanikiwa kuingia tena kwa mtu

Comments