USHUHUDA,AMINI KATIKA JINA LA YESU





Baada ya kumaliza chuo cha utalii,nilitafuta kazi kwa shida sana,Arusha. Niliwajua wengi lakini hawakuweza kunisaidia.
Ipo siku sitosahau nikawa najiombea sana hadi usiku mnene,sikujijua au Mungu anakusudi gani nami. Nina shemeji yangu alikuwa meneja mwajiri katika kampuni ya Utalii,nilimwomba sana anisaidie,lakini kazi zilikuwepo,hakunisaidia. siku moja akanipigia simu,nikamfuata, akaniambia kuna kazi imepatikana,Bukoba utaweza kwenda,nikamjibu ndiyo,sikuwa na jinsi miaka 5 nipo mtaani,nasota. Akaniunganisha na huyo mwajiri,akanitumia nauli,nikaenda Bukoba. Nikapokelewa vizuri,nikapewa nyumba ina kila kitu. Nikapewa na cheo nikawa meneja. Sasa nilikuwa sijajitambua,wakati mwingine naona maono ya Mungu,napuuza,nikaanza kazi nilikuwa napata wageni wazungu,nafanya kazi,pesa ikanikolea,sikuacha kuomba,nikasahau nilipotoka nikaanza kunywa pombe,wasichana,lakini kila nikinywa,usiku nateswa kwenye ndoto naona majitu yananifuata,nanyongwa,wakati mwingine wananibeba kama kunipeleka sehemu inagiza,nalia kweli na uwanaume wangu,nashituka nabadilisha mwenendo,naacha pombe,nikiacha uovu nalala vizuri kumbe hayo yote ni Mungu alinipenda,wapo wengine wanakufa. Nikatubu nikarudi kundini,nikawa makini,jinsi nilivyokuwa nalewa bosi alinifurahia sana,alinipa hadi usafiri,niliposimama kimaombi,kila nikienda kazini ananilalamikia,mara anasema sifanyikazi nastarehe,nikawa nasonöneka,nikapata marafiki wa kanisa fulani,wana wazungu wakawa wananipa kazi,tajiri yangu alikuwa ana Hotel,siku moja wakanialika,mchungaji nikale pasaka,katika maongezi Bwana mmoja akaniuliza,hapo kwenu hamna kazi,nikamjibu hamna,akaniuliza kuna msanii alikuwa anaimba alikufa pale,wanavyodai alitolewa kafara. Wakaniambia uwe makini bana,dah! Nikashtuka na yale mauzauza niliyokuwa nayaona usiku. Nikatulia nikaanza kukesha,maombi. Bosi mkubwa hakuwepo,nikapigiwa simu anakuja,nikaenda kumpokea. Nikawa naye siku 3,ikawa jumapili siingii kazini,akanipigia simu,wewe umekuja kustarehe,au kufanya kazi,nikaenda kazini sikumjibu,navyokwambia nilikutana na barua jumatatu ofisini,ya kwamba nimeachishwa kazi. Nikapokea mshahara wangu nikarudi Arusha. Ndipo nilipoamini maneno ya wale wachungaji,kusimama na Mungu ikawa vita pale hadi nikafukuzwa kazi. Ushuhuda huu uwajenge,muwe mnamuuliza Mungu au kumshirikisha awape kazi,usikurupuke wengi wameajiriwa na makampuni,wamekuwa watumwa,hakuna wanachokifanya,baada ya hapo nilianza kujiajiri mambo hayaendi,kumbe Mungu ananiita,ipo siku nikachoka na tabu hizo,nikamwomba Mungu japo anionyeshe kazi nitakayokuifanya,kweli Mungu ni mwaminifu,niliota ndoto nawaombea watu vibaya mno,nilipoamka nililia sana,nikwamwambia Mungu umeniacha siku zote nateseka,kumbe ulinihitaji. Huenda ni wewe ndugu,usione unapita kwenye mapito sana,tuliza moyo wako,mwambie Mungu atakupa kazi yako,tunajipotezea muda kwa kuangalia matatizo yetu. Ukiwa na Mungu,aliyekuajiri ni mchawi au mshirikina,ataambiwa na bwana wake,nao watakutesa,pasipo wewe kujijua,utapata mshahara leo,pesa itaisha kesho,chuma ulete,tuombe sana Mungu.
Bwana Yesu atusaidie ahsanteni. Kwaherini Aminaa!.By David polle

Comments