HISTORIA YA ASKOFU MOSES KULOLA





ASKOFU MKUU MOSES KULOLA

Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule  ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.
Alimwoa Elizabeth na wamezaa  watoto10 ambapo saba bado hai.alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa.
Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.
Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.
Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzishaa makanisa Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuan makanisa yapatayo 4000 katika nchi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo
Askofu Moses Kulola anayeongoza makanisa elfu nne, Askofu Msaidizi wake ni Mwaisabila.
Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo yasiyopungua 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake. Nampenda sana Askofu Moses Kulola maana anafanya kazi ya MUNGU kwa moyo na kwa mujibu wa kitabu cha historia yake Askofu Kulola amezunguka Tanzania nzima tena wakati mwingine kwa kutembea kwa miguu na kwenye mazingira magumu sana kiasi kwamba ni wito mkuu wa MUNGU mkuu alionao Askofu Kulola na kwa miaka zaidi ya 60 amekuwa akihubiri neno la MUNGU na hadi sasa MUNGU anamtumia sana, katika mkutano uliopita wa askofu Kulola pale viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam maelfu ya watu walihidhulia na wengi sana kufunguliwa na injili anayohubiri askofu Kulola ni injili iliyonyooka na akiwataka wanadamu kumpa YESU KRISTO maisha yao ili wapate uzima wa milele bure.MUNGU ambariki sana mtumishi wake huyu ni mfano hai kwa watumishi wa MUNGU wa sasa
ASKOFU MOSES KULOLA AKIWA NA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI FAUSTINE MUNISHI NA EMMANUEL MWASOTA NA HAPA ILIKUWA NI MWANZONI MWA MIAKA YA 1970
ASKOFU MKUU MOSES KULOLA AKISHIKANA MIKONO NA MCHUNGAJI DANIEL KULOLA AMBAYE PIA NI MCHUNGAJI PIA DANIEL NI MTOTO WA ASKOFU KULOLA

Comments

Anonymous said…
Bwana apewe sifa,asante kwa kuanza kutoa history kidokido unajuwa ktk 1996-2000 nilipata mzigo wa ku-documentary Kulola baada ya kuokoka nikaona kwanini mhubiri mkubwa kama huyu haambatani na media team.Matendo yote hayo yalokuwa akiyafanya ROHO Mtak.kupitia yeye-maana YESU aliagiza hubirini ufalme wa Mungu umekaribia -pozeni wagonjwa ,toeni pepo nk No records....!!!iliniuma sana.Nikarekodi mesage chache 1996-2000.Haya uliyoandika yamo tena analia kabisa-injli ya kusini lindi-mtwara.ukiona hii dvd utalia nawewe kwa wito huo...hata muda huu teyari niasikia kulia ndani yangu-Ubarikiwe wanahabari wa injili wanatakiwa
Peter Mabula said…
amen sana mtumishi wa MUNGU na kwa kweli haya niliyoandika ni moja tu katika 100 maana MUNGU amemtumia sana mtumishi wake tena hata katika mazingira magumu lakini bado MUNGU wa Moses Kulola alikuwa pamoja na mtumishi wake kwa injili ya zaidi ya miaka 60 na hadi sasa injili hii inasonga mbele. hakika utukufu ni kwa BWANA YESU