HATARI YA MAISHA. KUONGEZEKA NA KUYATUMAINIA MAARIFA YA KIDUNIA.

Vicent Mwengo
HATARI YA MAISHA.
KUONGEZEKA NA KUYATUMAINIA MAARIFA YA KIDUNIA.

Kwa maana rahisi ya neno maarifa au hekima ni ufahamu/uwezo wa kutambua jambo na kukabiliana na jambo hilo. Ninapozungumzia habari za hekima au maarifa ni namna watu wanavyokabiliana na maisha, lakini sasa shughuli zako za kila siku ndizo zinakufanya usiweze kuzikumbuka habari za Mungu? Liko tatizo la watu kumsahau Mungu kwa sababu ya shughuli zao cha kiuchumi, watu kujiongezea na kujivuna mali zao ambazo wanaamini ndio msaada wao maishani lakini wanasahau kama uhai walionao ni neema tu. Watu ambao wamekuwa na elimu ya darasani ndio wamekuwa na mioyo migumu tangu enzi za Yesu lakini kwa kipindi hichi tatizo hili limeongezeka kwa kasi, watu wanajivunia elimu zao; fanya uchunguzi utagundua wasomi ndio wanaoongoza kwa zinaa, dhuluma, uongo, wizi na mengine mengi yaliyo maovu. Naomba ujiulize mimi na wewe tuko kwenye kundi lipi. Nikwambie tu hivi; hapana!! Tusikubali, pamoja na mambo yote tumtangulize Mungu. Jifunze kupitia hadithi chache toka kwenye kitabu kitakatifu.
Luka 12:13-21
Mathaayo 6:19-21
Muhubiri 6:1-7 kaa chini zisome kwa makini utaelewa.

NB: MKUMBUKE MUNGU, MHESHIMU MUNGU KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YAKE. (soma Biblia utayakuta maagizo).MUNGU akubariki sana by  Vicent Mwengo

Comments