KATIKA KUISHI MAISHA YA KIMUNGU YAKO MAMBO NI LAZIMA KUYAACHA.





BWANA YESU APEWE SIFA…
Wapendwa wa Mungu nami niwaletee maneno ya MUNGU.
Kwenye maisha ya kawaida ya mtu yeyote kitu ambacho
humfanya ajisikie furaha sana ni uhuru wa mawazo na matendo, kwa hayo huamini nafsi yake imeridhika kwayo.
Katika uhuru huo mtu anakuwa anawaza pia hasa matendo ambayo ndiyo huonekana kwa wanadamu huyatenda pia. Mtu huyo huyatenda na huwa haijalishi kama yanawaudhi wengine au hapana lakini ili mradi huufurahisha moyo wake basi huyatenda tu. Uhuru huu mtu huwa nao tu kwa sababu hakuna jambo au mtu yeyote ambaye anaweza kuingilia au kuupunguza uhuru huo. Cha ajabu ni kwamba upo wakati uhuru kwa mtu hubadilika, hupungua na kuanza kufanya kwa misingi ya mamlaka nje ya kichwa au mawazo yake. Ni wakati huu ambapo mtu hupata shida kwa sababu amebadilishiwa utaratibu wake wa kuishi iwe kwa kutaka au kulazimishwa lakini baada ya muda huwa ni maisha yake ya kawaida kwani huyazoea.

Fikiria mtu anapokuwa chini ya mamlaka fulani hususani za utumishi (kuwa chini ya bosi). Yako mambo ambayo kwa mazoea yako ulikuwa unayatenda kwani ulikuwa ni uhuru wako lakini kwa sababu sasa uko chini ya mamlaka ya mtu huyaachakuyatenda kwani mamlaka hayo haiyapendi au ina utaratibu wake. Fikiria ulikuwa umezoea kuvaa viatu vya wazi/sandles na pensi, baadhi ya misuko kwa wadada, nguo fupi na zinazoonesha maungo ya ndani lakini ukifika kwa bosi anakwambia style hiyo hatuitaki vaa hivi na uonekane hivi la sivyo huna kazi. Kwasababu ya kuhitaji kazi mtu huyo hubadilika na kufuata utaratibu huo wa kazini na kuacha maisha yake ya kawaida,

Pia yamkini kwa sababu mtu huyo alizoea kuamka saa tatu pindi hana kazi baada ya kupata kazi hulazimika kuamka saa 12 au saa 1 ili kuwahi kazini aendane na masharti na taratibu za kazi.(hiyo ni baadhi ya mifano tu) katika maisha ya kimwili ya kila siku.

Vivyo hivyo maisha ya kimungu yana sheria taratibu, na masharti yake pia. Unapoanza maisha ya kimungu ni lazima yako matendo na mwenendo wa fikra zako kubadilika pia. Mpaka unamtafuta mungu maana yake umetambua dhambi za maisha yako ndio maana ukazikimbia, mmhh haiishii hapo, inapasa kukimbiambali zaidi ktk na kuyaacha mazoea yako ili kishi maisha yenye msingi wa kimungu na kumpendeza mungu na watu pia. Tunapoamua kumtumikia bosi wetu mungu ambapo malipo yetu ni kufika mbinguni ni lazima tuache baadhi ya mazoea yetu mabaya. (flp 1:27)

Soma filp 3;1-10
Nizingatie filp 3:7 lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya kristo.
Hapa Paulo alikuwa akiwahadithia wafilipi habari za nyakati zake kabla ya kumpokea kristo kwamba aliyatenda kwani yaliufurahisha moyo wake, lkn baada ya kumpokea kristo sasa anachukua gharama ya kuyaacha.
Katika mengi unayoyajua kwa uzoefu wako wa maisha mimi nitazungumzia jambo moja tu

MAVAZI.
Suala la mavazi sijui kama watu huwa wanalizingatia hussani wale wenye jukumu la kuhubiri au kufundisha neon la Mungu. Elewa vizuri dhana hii, “Mungu anaangalia moyo wako lakini wanadamu wanaangalia matendo yako, wakiyaona mazuri huamini lakini wakiyaona mabaya hawana haja na Mungu wako”

Angalia habari hizi, watu Fulani wakajisemea; aaahh kwa jinsi alivyo huyu hata mimi leo nikiokoka siwezi kuvaa hivi.

Mahala Fulani watu wakishuhudiwa ibada ya nyumba kwa nyumba walisema; aaa aaahhhh azungumze huyu lkn huyu sisi hatutaki atushuhudie kwani naye anahitaji kushuhudiwa (mavazi yake yalikuwa mabaya)

Mhubiri akihubiri na hereni zake ndefu sana na madoido mengi, mshirika mmoja akaulizwa umeelewa somo la leo? Alichosema aah hivi zile herein zinauzwa shilingi ngapi? Na zinapatikana wapi kwani makubwa!!!

Mhubiri mmoja akiwa madhabahuni akidhani watu walikuwa wanasikiliza neon kwa makini kumbe watu walikuwa wanatafakari hivi kile kikofia alichovaa kinauzwa shilingi ngapi kwani kina mbwembwe kwelikweli.
(hiyo ni baadhi ya matukio niliyowahi kupata kuyasikia au kuyaona kwenye huduma mbalimbali)

Haijalishi kama wewe ni muhubiri, mwalimu au muumini wa kawaida je unajiwekaje kimavazi mpaka wengine waseme hakika huyu amebadilika.

MWISHO NIMALIZIE,
TAFAKARI, JIPIME MWENYEWE KAMA MTU WA MUNGU NA MAISHA YAKO YAWAFUNDISHE WENGINE.

Comments