MAMA RWAKATARE AFADHAISHWA NA MANENO YA KASHFA



 Mtumishi wa MUNGU mama Getrude Rwakatare akifundisha neno la MUNGU kanisani Mlima wa moto Assemblies of GOD, Mikocheni B jijini Dar es salaam
Mtumishi wa MUNGU mama Getrude Rwakatare wa mikocheni B Assemblies of GOD ameandika katika wall yake ya facebook akielezea kufadhaishwa kwake na tukio la mtu mmoja kuandika maneno ya kashfa zidi yake.''Wanangu, Jina la Bwana libarikiwe sana. Ningependa kumshukuru Mungu sana kwa mema yote aliyotutendea mpaka kuiona siku ya leo. Sifa, Utukufu,Shukrani na Heshima tumrudishie Mungu wetu aliye hai. Nimefadhaika sana Moyoni mwangu baada ya kuona mpendwa akiandika maneno ya kashfa juu yangu na kusema account hii ni feki, baada ya kupiga ile namba niliyoiweka kwa ajili ya maombi yenu na kupokea moja ya wanangu hapa nyumba. Nilifungua PAGE yangu ili niweze kuweka mafundisho kwa ajili yenu. Roho akanifunulia tena nikafungua hii account ili niweze kuwa karibu nanyi na kusikiliza shida zenu na kuzileta mbele za Bwana, kwani ndio kazi niliyoitiwa hapa duniani na pia ni baraka kwangu kama mtumishi ya kuwaombea watu wenye matatizo mbalimbali. Basi kulingana na hoja hiyo, wangapi wangependa niifunge account hii, ili nisiweze kuwa karibu nanyi na kusikia matatizo mengi, na ibaki PAGE tu. Wanangu ninawapenda sana, naomba mnisamehe sana kama nimefanya makosa kufungua account hii. Natumai ningepeda kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwenu. Jina la Bwana libarikiwe sana!

katika mojawapo ya ibada zenye nguvu ya MUNGU katika kanisa la Mlima wa moto, mikocheni B.

Comments