NA BARAKA HIZI ZOTE ZITAKUJIRIA NA KUKUPATA USIKIAPO SAUTI YA BWANA,MUNGU WAKO.(Kumb. 28 : 2 ) * Sehemu ya kwanza *


Mtumishi Gasper Madumla
Haleluya…
Jina la Bwana lipewe sifa…

Kati ya jambo la kushanga’za duniani ni hili, la mtu kuomba BARAKA.Hakuna andiko wala fundisho linalofundisha watu waombe Baraka.
Hivyo basi BARAKA HAZIOMBWI bali zinakujilia pale utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote ambayo Bwana akuagizayo.

Nasema utakaposikia maagizo ya Bwana KWA BIDII.
Maandiko matakatifu yako wazi kabisa ,na hapa tunasoma,
Kumb.28 :1-2 :
" Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako."

Kupitia andiko hilo ,tunaona maana halisi ya BARAKA,Kwamba,
Baraka ni :
01.Kusikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii,
02.kutunza kuyafanya maagizo yake yote akuagizayo leo,
03.Kutukuzwa juu ya mataifa yote ya duniani., na baraka hizi zote kukujiria

Sasa kupitia maana hiyo ya BARAKA,Kamwe huwezi kuomba BARAKA.
Kinachowafanya watu waombe BARAKA ni uvivu wa kushindwa kusoma maandiko matakatifu na kutomshirikisha roho Mtakatifu kwamba awafunulie wapate kuelewa.

Watu wengi tena Wakristo wa namna hiyo utawakuta wananga’nga’na wakitaka kubarikiwa pasipo kwanza kulishika neno la Bwana Mungu KWA BIDII,wala pasipo kuyatunza maagizo ya Bwana.Leo nataka nikujengee msingi wa somo hili,ili nitakapokuwa naendelea mbele iwe lahisi kwako kunielewa.

Haleluya…
Jina la Bwana libarikiwe…

Labda tuanze kuchambua maana ya Baraka kama ilivyo hapo juu,Kumbuka ninakuambia

BARAKA ni :
01.KUSIKIA SAUTI YA BWANA,MUNGU WAKO,KWA BIDII

Ukweli ni kwamba duniani zipo aina nyingi za sauti. Sauti hizi zote zinaweza kusikiwa kwa masikio yetu ya nyama.Sasa ishu kubwa sio kusikia sauti kama sauti tu,Bali ni sauti ipi uisikiayo,Je ni sauti ya Bwana ?
Au ni sauti za wataabishaji wa neno la Mungu?

• Neno linaposema “ UTAKAPOSIKIA SAUTI YA BWANA ” Inamaanisha Utakapoelewa kile ukisikiacho kutoka kwa Bwana.
• Ukiwa msikiaji wa neno la Mungu,Basi utakuwa ni mtendaji wa neno la Mungu.
Shida tuliyonayo sisi Wakristo ni kwamba sio WASIKIVU WA NENO LA MUNGU bali ni wasikilizaji tu,( Maana ya kusikiliza ni kule kunakohusisha na kutokuelewa kwa neno,Bali KUSIKIA ni kuelewa kwa neno)

Bwana anazungumza nasi kwa njia tofauti tofauti,maana Yeye ni MUNGU MKUU hatuwezi kuzungumza naye moja kwa moja,bali twazungumza naye kwa njia tofauti tofauti labda kwa kupitia kwa watu wake,Au Maono,Ndoto.N.K
Bidii inahitajika katika kusikia sauti ya Bwana.
Ikumbukwe kwamba Mambo ya Mungu yote yanahitaji BIDII,
Pasipo bidii hakuna kumuona Mungu.

Maana hata katika viwango vya utakatifu,Bidii yahitajika.Na ndio maana kwenda mbinguni si rahisi kama wengine wanavyodhani,Bali BIDII yahitajika.Baraka za Bwana haziji kwa kula na kulala,Bali kwa kutumia bidii kulisikia neno la Mungu. Labda nikupe mfano wa mtu aliyetumia gia hii ya BIDII katika kuomba kisha akapata mpenyo,na hapa tunaye ELIYA Tunasoma

Yakobo 5 : 17-18 :
“ Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba KWA BIDII mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake. ”

Eliya alikuwa hana tofauti na sisi wanadamu wa leo,katika hali ya mwili,Bali tofauti yake ni kwamba yeye aliomba kwa KWA BIDII,kisha BIDII alimsukuma apokee yale ayaombayo,tunaona alifanikiwa kuisimamisha mvua muda wa miaka mitatu na nusu.

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.
MR& MRS GASPER MADUMLA

Comments