RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU MBALIMBALI YA DINI YA KIKRISTO IKULU

Raisi Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi wa madhehebu ya kikristo dini Ikulu Dar es salaam jana, Rais amekuwa na mazungumzo na viongozi hao wa kiroho ikiwa ni katika jitihada zake za kutafuta muafaka na amani ya Taifa letu, hii inatokana na hali ambayo imeanza kujitokeza kwa baadhi ya watu wachache kuanza kujenga chuki zinazotoka na tofauti zao za imani.

kazi yetu yetu sisi ni kuomba kwa Bwna wetu ili amani ipatikane, tunaamini kile ambacho kimezungumzwa na Rais na viongozi hao wa makanisa, kinakwenda kuzaa matunda mema tena yenye faida kwa watu wa Dini zote na kwa manufaa ya taifa letu la Tanzani
Viongozi wa madhehebu ya Kikristo wametoa wito wa kuwataka waumini wote kote nchini, kulinda amani na umoja uliopo ili Taifa lisije likaingia katika mgawanyika wa kidini na hatimaye Taifa kugawanyika na kuingia katika mgogolo na ugomvi wa kidini. wito huo umetolewa jana na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo mara baada ya kikao cha pamoja na Rais Kikwete Ikulu jana

viongozi hao wa kiroho, walifika Ikulu wakiongozwa na Askofu T. Ngalalekumtwe, ambaye ni mwenyekiti wa baraza la maaskofu Tanzania (TEC), Viongozi wengine waliokuwepo ni kutoka PCT. CCT, SDA, Viongozi hao wamemweleza Rais Kikwete kwamba wanaunga mkono jitihada zake ambazo anazifanya za kutafuta muafaka na amani ya nchi yetu, viongozi hao kabla ya mazungumzo yao, walitoa tamko lao mbele ya Rais, tamko ambalo ndilo lilikuwa mwongozo wa mazungumzo yao hiyo jana

kabla ya kikao hicho cha jana, Rais Kikwete siku chache zilizo pita aliwahi kukutana na viongozi wa dini ya kiaslamu, na baada ya kikao cha jana, Rais atakutana na viongozi wote wa Kikristo na Kiislam kwaajili ya kuhakikisha amani na umoja unadumu katika Taifa la Tanzania

Tunamshukuru sana Rais kwa hatua hii na tunazidi kumwombea ili Mungu ampe hekima na afya njema kwa ajili ya kuliongoza Taifa ambalo amekabidhiwa kuliongoza.
Mungu ibariki Tanzania

Comments