UHURU KENYATTA AAPISHWA NA KUWA RAISI WA 4 WA KENYA

Rais  Uhuru Kenyatta akishikilia biblia na mkono wake wa kulia wakati akiapishwa kuwa rais wa nne  wa Jamhuri ya  Kenya katika uwanja wa  Kasarani Sports Center huko  Nairobi, Kenya akiangaliwa mke wake Margaret Uhuru kulia .
Rais Uhuru Kenyatta akishikilia BIBLIA TAKATIFU na mkono wake wa kulia wakati akiapishwa kuwa rais wa nne wa Jamhuri ya Kenya katika uwanja wa Kasarani Sports Center huko Nairobi, Kenya akiangaliwa mke wake Margaret Uhuru kulia .

Rais mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapishwa katika sherehe ambazo zilihudhuriwa na maelfu ya watu waliokuwa wakishangilia huku wakipunga bendera zao katika mji mkuu Nairobi.
Tukio hilo ni kilele cha uchaguzi wa Machi 4 uliofanyika kwa amani ambapo Kenyata alimshinda Waziri Mkuu anayaeondoka madarakani Raila Odinga . Rais huyo ameahidi kufanya kazi kuboresha maisha ya Wakenya wote.

Viongozi wengine  wengi barani Afrika walihudhuria hafla hiyo, ikiwa ni pamoja viongozi wa mataifa ya nchi jirani za Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Baadhi ya mataifa ya magharibi yaliwakilishwa na mabalozi wao wakati wakijaribu kupunguza mawasiliano na rais huyo kutokana na kesi inayomkabili huko ICC.
Wakati wa hotuba katika sherehe za kuapishwa rais wa Uganda Yoweri Museveni aliwapongeza Wakenya kwa kumchagua Bw.Kenyatta na akikaidi  kile alichosema kuwa ni kurubuniwa na ICC.
Rais Kenyatta anakabiliwa na mashitaka ya uhalifu  dhidi ya ubinadamu  kwa shutuma za kusaidia ghasia za baada ya uchaguzi mapema 2008 ambazo zilipelekea vifo vya watu zaidi ya 1,100 na wengine 600,000 kupoteza makazi yao. Kesi yake itaanzwa kusikilizwa mwezi Julai.





Comments