WAKRISTO WANA HAKI JA KUCHIJA KWA MUJIBU WA MAFUNDISHO YA KIISLAMU.

Je! Wakristo wana haki ya kuchinja kwa mujibu wa mafundisho ya kiislamu? . Jibu ni ndio, kwa mujibu wa Qur-an 5:5 nainukuu. Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha waliopewa kitabu kabla yenu ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao. Mwisho wa kunukuu. Mahali popote katika Qur-an inapotaja waliopewa kitabu, wanakusudiwa ni Wayahudi na Manasara yaani Wakristo, hili halina ubishi kwa msomi yeyote wa Qur-an.
Pengine kuna madai ya uongo kusema waolipewa kitabu sio Wakristo wa sasa ni wale wa zamani, hii hoja sio ya kweli kwa wapenda haki na utii wa maneno ya Mungu. Katika Qur-an takatifu ya Kiswahili, iliyo tafsiriwa na Kadhi na shekhe Abdulla Saleh Farisy chapa na 7. 2004. Ufafanuzi katika hiyo sura ya 5:5 surat maidah. Nanukuu. Chakula cha kuchinja hakiwi halali kwa Waislamu ila kichinjwe na (a) Mwislamu au na (b) Myahudi au (c) Mnasara (Mkrito) kwa sharti ile ya kuchinja sio kuwanyonga. Mwisho wa kunukuu.
Katika kitabu cha waislamu kiitwacho “Halali na haramu katika uislamu” kilichoandikwa na Ustadh Yusuf al-Qaradhawi. Ukurasa wa 67. Nanukuu. Na ikadhaniwa kuwa baadhi ya Waislamu wata- wachukulia Wayahudi na Manasara (Wakristo) kama wenye kuabudu sanamu na mizimu, Mwenyezi Mungu alitoa ruhusa ya kula chakula chao na kuoa wanawake wao ili kuwatofautisha na washirikina, akasema Mola mtukufu. Mwisho wa kunukuu.

Comments