KWELI KUHUSU MCH JOSEPHAT GWAJIMA

Pastor Josephat Gwajima


"Siku moja nilialikwa kuhudhulia kwenye maombi, pamoja na watu wengine walikuwepo maaskofu mbalimbali, nikiwa kijana nikamsikia askofu mmoja mzee akiomba. Nami nikavutiwa sana kujua anaomba nini, ikanibidi kuacha kuomba ili nisikie, yule askofu alikuwa akisema, "Mungu naomba unisamehe kwasababu sikuutumia ujana wangu vizuri kukutumikia wewe, naomba uniwezeshe nikutumikie katika uzee wangu"

Hapo hapo, nilishtuka alafu nami niakaanza kuomba maneno haya, "Mungu naomba nikifika uzee wangu, nisiombe maombi ambayo anaomba askofu huyu"

Toka siku hiyo, nikaamua kumtumikia Mungu kwa bidii zote, biblia inasema, Ufunuo 14:13 "Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao." Mbunguni hawaangalii ulipewa nini bali, ulifanya nini ulipokuwa duniani. Matendo yako ndio yatakayofuatana nawe. Kama hukutenda chochote kumtumikia Bwana Yesu, ni sawa na bure.

Jifunze kumtumikia Mungu hungali kijana."

- Pastor Josephat Gwajima

Comments