ASILI YA PASAKA.




BWANA YESU asifiwe.
BWANA AMEFUFUKA? AMEFUFUKA KWELI KWELI. AMEN.
karibu tujifunze kuhusu PASAKA.

-Pasaka ya Kiyahudi ni kati ya sikukuu muhimu zaidi za dini ya Uyahudi. Sikukuu hii inakumbuka kutoka kwa Wanaisraeli kutoka utumwa walimokuwemo huko Misri.

-Pasaka ya Kiyahudi ina uhusiano mkubwa na pasaka ya wakristo leo 

                                  JINA LA PASAKA

Jina la Pasaka limetokana na neno la Kiebrania lenye maana ya "kupita juu, kukaa juu ya (kama mlinzi)" katika kitabu cha Biblia cha Kutoka 12:23(
Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi. )  

Hapa imeandikwa ya kwamba MUNGU "atapita" juu ya milango ya nyumba za Wanaisraeli huko Misri katika usiku kabla ya kutoka kwao, na kuwaua wazaliwa wa kwanza wote wa wamisri.

Na Peter M Mabula
Katika Biblia, kitabu cha Kutoka, sura ya 12, kuna taarifa ya kutoka kwa Wayahudi katika Misri wakati wa Musa mnamo mwaka 1200 KK. Musa alitumwa na MUNGU kuwaondoa Wanaisraeli katika hali ya utumwa huko Misri na kuwaongoza kwenda nchi ya ahadi. Lakini mfalme wa Misri, Farao alikataa hivyo MUNGU alituma mapigo dhidi ya Misri ili Farao alazimishwe kukubali. Pigo la mwisho tena la kali mno lilikuwa kifo cha kila aliyezaliwa kama mtoto wa kiume wa kwanza katika Misri. Hapo Wanaisraeli waliambiwa kuchinja kondoo na kupaka damu milangoni kwao ili malaika akipita kuua watoto wa kwanza asiguse watoto wa Wanaisraeli. Baada ya pigo hili Farao alikubali Wanaisraeli watoke.

Tendo hili la kuwawekwa huru kwa waisraeli linakumbukwa na Wayahudi kote duniani kote kila mwaka. Na lina uhusiano mkubwa na Pasaka ya wakristo ambapo BWANA YESU alikufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu, hivyo anayempokea kama BWANA na Mwokozi wake hutengwa mbali na shetani na kufanyika mtoto wa MUNGU.Luka 24:1-8-Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari. Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, Wakaingia, wasiuone mwili wa BWANA YESU.  Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumeta-meta; nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, hao waliwaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu?  Hayupo hapa, amefufuka. Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa akaliko Galilaya, akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu. Wakayakumbuka maneno yake.''

Pasaka ya kwanza ilikuwa ni ukombozi kwa waisraeli kutoka utumwani misri na kwenda nchi ya ahadi yaani kaanani na Pasaka ya kwetu ni ukombozi kutoka utumwani kwa shetani na tunaingia katika ufalme wa Milele wa BWANA YESU.

 Je, ni kwa nini usiku huu ni wa tofauti na nyingine zote? Kutoka 12: 26 -27 Kisha itakuwa hapo watoto wenu watakapowauliza, N’nini maana yake utumishi huu kwenu? ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya PASAKA ya BWANA, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainama vichwa na kusujudia

                             Umuhimu wa Pasaka

Pasaka ni moja ya sikukuu kubwa sana kwa Wakristo. Pamoja na kuwa imeendelea kuchukuliwa kama tukio la kihistoria tu, bado dhana yake ya kuonyesha upendo wa MUNGU kwa wanadamu haitapotea. 


Ni upendo wa kutoa moja ya nafsi za MUNGU, iteswe, isulubiwe, ife na kisha ifufuke kudhihirisha utukufu wa MUNGU na upendo wake kwa wanadamu.

MUNGU awabariki sana na nawatakia PASAKA njema sana  na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.


                       MUNGU akubariki sana .

                        Ni mimi ndugu yako

                          Peter M Mabula

                    Maisha ya Ushindi Ministry.

                         +255714252292
BWANA YESU AMEFUFUKA?
AMEFUFUKA KWELI KWELI AMEN AMEN.

Comments