ILIKUWA NI PASAKA YA UKOMBOZI, KUFUNGULIWA NA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU KPC KAWE.

Ni saa ya ukombozi na kufunguliwa kwa jina kuu la YESU KRISTO.
Kama vile ambavyo mamilioni ya wakristo duniani walivyosherekea ukombozi wao kwa furaha na shangwe, Ndivyo ilivyokuwa pia katika kanisa la P A G kawe au maarufu kwa jina la Kawe Pentecostal Church(K P C) Ambalo liko chini ya mchungaji Elly Boto.

Katika ibada hiyo iliyojaa nguvu za MUNGU mhubiri alikuwa ni mchungaji Yona Gidasaida kutoka Manyara -Hanang  ambapo nguvu ya MUNGU ya hali ya juu sana ilishuka na BWANA YESU alifufua uzima ndani ya watu, wapo waliokuwa wameteswa na nguvu za giza lakini BWANA YESU alifufua uzima ndani yao, pia ibaada hiyo iliambatana na somo la ujazo wa nguvu za ROHO MTAKATIFU.

Akifundisha somo linaloitwa NJOONI MKATAZAME AMEFUFUKA.
Mchungaji Yona Gida alisema, '' Habari hii ya ufufuko ilikuwa habari njema kwa kila mwamini na BWANA YESU alithibitisha kufufuka kwake kwa kuwatokea watu zaidi ya 500 wakiwemo wanafunzi wake, pia BWANA YESU aliwaonyesha hata alama za misumari wanafunzi wake  ili kuthibitisha kufufuka kwake.''

Pia Mchungaji Yona alisema kwamba '' Jiwe lililokuwa kizuizi cha kuwazuia watu wasione kilichopo kaburini, liliondolewa na malaika, na kuwaambia NJOONI MKATAZAME HAYUPO KABURINI AMEFUFUKA KAMA ALIVYOSEMA.
Mtumishi wa MUNGU alisema wapo watu wengi leo  mawe yamewakalia katika maisha yao, kuna mawe yamekalia biashara zao, kuna mawe yamekalia ndoa zao na kuna mawe yamekalia wachumba zako lakini kwa Kumwamini BWANA YESU aliye fufuka kutoka katika wafu  na kumpokea kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yao, Mawe yote yataondoka. Akasema jiwe na litoke katika masomo yako, ndoa yako, uchumba wako na biashara yako kwa jina kuu  la YESU KRISTO aliye HAI.''
Mchungaji Yona  alitumia maandiko haya ili kuithibitisha ukweli wa MUNGU, Mathayo 28:1-8, Marko 16:1-8, Luka 24:49, 1 Korintho 10:11 na Yohana 7:37-39. 

Haya ni baadhi ya matukio katika Picha.

Wakati wa kumsifu BWANA YESU aliye hai.

Mtumishi wa MUNGU Pius Kapufu , kama kawaida akifanya kweli kwenye kinanda.

Praise and Worship team wakiwa kazini.



Wakati wa maombezi

Ndugu huyu anaitwa Yusufu Hussein amekuja kuokoka na kumpokea BWANA YESU baada ya kufanya uchawi na uganga wa kienyeji,. Nitakuletea ushuhuda wa ndugu huyu ambaye ilikuwa ni kawaida yake kuwalalia watu ambao hawana nguvu za MUNGU, atashuhudia mahali hapa siku chache zijazo maana ana ushuhuda mzito sana ambao aliusema kanisani baada ya maombezi , nimeongea nae na atatoa ushuhuda wake hapa. Usikose maana ni ajabu ya ajabu.


BWANA YESU akiwaweka huru watu

watu waliojitokeza kupokea nguvu za ROHO MTAKATIFU.



Mchungaji Yona Gida kutoka akifundisha katika ibada ya Pasaka kanisani KPC

Baadhi ya waimbaji wa K P C Choir baada ya ibada


Hata mimi ni mmoja wao.



Ni siku ya kufurahia ukombozi wetu, Hapa nikiwa na baadhi ya waimbaji wa kwaya yetu ya K P C Choir.

Comments