KANUNI 12 YA KUIMARISHA MUDA WA THAMANI NA MWENZI WAKO

Na Mchungaji na Mwalimu Peter Mitimingi, Mkurugenzi wa Huduma ya The Voice of Hope Ministry(VHM)

1. Hakikisha kwamba unarudi nyumbani mapema katika muda mzuri baada ya kazi zako za siku.

2. Ukifika nyumbani usifikie kwenye Tv, magazeti, Kompyuta au mambo yako binafsi.

3. Jambo la kwaza liwe kukaa na mwenzi wako na kupata taarifa kwa kifupi ya mambo yaliyojili wakati ulipokuwa haupo.

4. Usipeleke cheo chako nyumbani au kazi zako za ofisi au biashara zako nyumbani kwa mkeo au watoto.

5. Mtazame mwenzi wako wakati mnapozungumza usiangalie pembeni au kwenye simu au Tv au kwingineko.

6. Usimsikilize wakati huo huo unafanya jambo linguine labda unapika au unafua au unachambua mchele au unasoma magazeti nk.

7. Sikiliza kwa hisia na uonyeshe kwamba hisia zako zipo pamoja naye. UUnge mkono kwa kuitikia, au kuonyesha mshangao, au kwa kucheka nk.

8. Usiwe mwingi wa kuzungumza bali utumie muda mwingi kisikiliza (hasa kwa wanaume). Zingatia kanuni ya kusikiliza. Wanaume huongea maneno 6,000 kwa siku na wanawake huongea maneno 24,000 kwa siku.

9. Tengenezeni utaratibu wa kutoka nje pamoja (Outing) sehemu za tofauti na zile mlizo zizoea. Mtoe mkeo au mumeo na watoto outing mara moja moja.

10. Mnapotembea muongozane pamoja. Msiachane au mmoja natangulia na mwingine anafuatia nyuma hiyo inaleta picha mbaya kusomeka kwa watu na huwa ni dalili za kuanza kutengana kwa siku za usoni.

11. Mle chakula kwa pamoja sio kila mtu kula kwa wakati wake. Kuna nguvu sana kwa wanandoa kula chakula pamoja.

12. Muwe na wakati wa maongezi na ibada pamoja kama mke na mume na watoto pia.

Comments