MASUMBUKO WALIYOYAPITIA MASHUJAA WA IMANI WA ZAMANI NDIYO TUNAYOPITIA SISI KATIKA KANISA LA LEO.

Natafakari Wakristo walio katika nchi za vita kama Syria, au wakristo walio katika nchi zinazouchukuia ukristo , wanaopitia mambo yakushtua Imani yao katikati ya vita na mateso. 

Wengi wao iliwabidi watoroke kuokoa maisha yao, wakiacha nyuma nyumba zao, kazi na Kanisa. Ili wanusurike, inawabidi wakimbie maeneo mengine ambayo pia hayana urafiki na Wakristo. 

Hawa waumini kutoka katika nchi kama hizi  hawana kazi wala makao, hawana pa kutorokea. Lazima waombe kila siku kupata chakula. 

Wengi wameuawa. Hata hivyo, wanaendelea kuubiri Injili katika nchi hizi za ukimbizi pale wametorokea kwa sababu ya vita.

Wapo watu wa MUNGU ambao huwaza  ''Majaribu  yamekuja kwetu , kwetu sisi, majaribu makali yamekuwa nasi kwa miaka mingi sasa.”

 Wameona taabu kwa muda mrefu sana, wameelewa maaan ya kuishindania  Imani. Kama Mtume Petro au Mtume Paulo, wametengwa Kuubiri na nguvu, wakilionya Kanisa la KRISTO.

Mimi naamini kwa kweli, wengi wetu tuko katika majaribu makali kutoka kwa adui, tunastahimili majaribu. Je wewe? 

Kama hujapatwa na jaribu la Imani? Ninakusihi: shukuru MUNGU. Lakini, nyenyekea, usiwahi kujisifu kuwa Imani yako ni ya nguvu kuliko wengine.

Shetani hungojea mpaka pale anayejaribiwa amevunjika moyo, na kuisha nguvu. Yeye hungoja mpaka pale maombi yana kaa kana kwamba hayajibiwi – pale matumaini yamekwisha kabisa, pale ambapo mbinu zetu zimekwisha. Hilo ndilo lilimtendekea Mtume Petro, alipomuona BWANA wake akiteswa mbele ya kikao cha Mafarisayo. 

Iilimtendekea Ayubu, aliye lazimika kuwaza alipo poteza kila kitu cha muhimu kwake.

Maswali yanapochipuka akilini mwa anaye pitia majaribu – “MUNGU, ukowapi?
 Kwanini maombi yangu hayajibiwi?” – papo ndipo Shetani huchagua kupanda Uongo wake: “MUNGU amekuacha. Amejitenga nawe. Hakusikii.”

Kumbe MUNGU hajakuacha – na hatawahi kukuacha. Kwa kweli, sasa hivi anakuambia hivi: “nimekuhakikishia sitakuacha kamwe. Sasa basi, simama, enenda ukalishe kondoo wangu. 
 Chunga mbinu za Shetani kinyume nawe, tazama, niko nawe, hata mpaka mwisho wa Dunia.” Amina!

MUNGU akubariki sana.

Comments