NTEZE JOHN LUNGU AOKOKA, KWA SASA NI MCHUNGAJI MAREKANI

MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Nteze John Lungu sasa amekuwa Mchungaji wa kanisa moja la kilokole nchini Marekani, imeelezwa.
Rafiki mmoja wa karibu Nteze, ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Nteze aliyewika Pamba FC ya Mwanza na Simba SC ya Dar es Salaam, kwa sasa amekuwa mtumishi wa Mungu baada ya kustaafu soka
.

Mtumishi wa Bwana; Mchungaji Nteze John Lungu (watatu toka kushoyo) aliyekuwa mchezaji wa timu ya Pamba ya Mwanza na Simba Sports Club ya Dar es Salaam pamoja na Watanzania wa Seattle, ndugu, jamaa na marafiki kwa pamoja wakiwa kwenye makaburi ya Holy Rood kwenye safari ya mwisho ya mpendwa wao Flora Ndimbo Glimsdale aliyefariki tarehe 12/30/2013, huko Seattle Washington State na kuzikwa Jumatatu Jan 6, 2014/


Nteze alianza kuichezea timu ya  Pamba FC mwaka 1990 na mwaka 1994 akasajiliwa Simba SC hadi alipokwenda Afrika Kusini na Marekani kucheza soka ya kulipwa.
Nteze alirejea Simba SC mwaka 2002 na baada ya hapoalistafu na kwenda kuishi Marekani.
Nteze ni kati ya wachezji wachache waliopata mafanikio wakiwa na klabu na timu za taifa pia.


Nteze John wa pili kushoto baada ya Joseph Kaniki akitambulishwa kwa mgeni rasmi na Nahodha wa Simba SC,Suleiman Matola mwaka 2002 kabla ya mechi dhidi ya Moro United Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kwani pamoja na kushinda mataji mawili ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, sasa Kombe la Kagame akiwa na Simba SC mwaka 1995 na 2002, pia alishinda Kombe la CECAFA Challenge mwaka 1994 akiwa na timu ya Bara, Kilimanjaro Stars nchini Kenya na Kombe la CECAFA Castle mwaka 2001 mjini Mwanza akiwa na Taifa Stars.
 
CHANZO BIN ZUBEIRY
.

Comments