PICHA ZA HARUSI ZA AMOSI. YESU NI MWANAUME ANABADILISHA. HUYU NI MUISLAM ALIYEOKOKA ALIKUWA SHOGA, JINA AUNT ASU, KAKUTANA NA MWANAUME WA WANAUME YESU KAMBADILISHA SASA ANAMTUMIKIA MUNGU, AMESHAREKODI CD YAKE.

 Amosi akiwa na mkewe baada ya kufunga harusi.
 Mungu anaendelea kuonyesha uwezo wake wa kubadilisha maisha ya wanadamu, zaidi upendo wake kwa wanadamu kuonyesha kuwa hana upendeleo hata kama mtu ni mwovu namna gani basi yeye bado yeye anampenda tu, kwani yeye hakuja kwa waliowazima maana hawahitaji dakitari bali wale waliopotea, walio kwenye vifungo vya shetani na kuwahamishia katika pendo lake na kuwapa maisha ya heshima yenye furaha na upendo. hii inamhusu sana aunt Asu ambaye hapo mwazo alikuwa shoga
wa kutupwa ameshaolewa mara nyingi na kuachwa, na si hivyo tu bali aliishi maisha ya kudhalilika ya kuvyaa mavazi ya kike na kujipodoa. lakini upendo wake Mungu na neema ya kristo ikamwangazia na kupata neema hii ya wokovu na kuamua kuokoka.







 Msajili wa ndoa hiyo mch D. Kanemba na mapaparazi nao walikuwepo



 Kwa kweli Yesu anabadilisha kabisa na kumfanya mtu kuwa kiumbe kipya huyu sasa tena siyo Aunt Asu kama wengi walivyozoea kumwona sasa ni Mtumishi wa Mungu ambaye kwa sasa amejikita katika kumtumikia Mungu kwa sasa amesharekodi albamu yake ya nyimbo za injili, na amesha anza kurekodi na dvd muda si mrefu itaingia katika soko la muziki wa injili, kati ya nyimbo ameimba kuna unaoelezea maisha yake wakati anatumikishwa na shetani lakini sasa kabadilika.

Hicho ni cheti kuonyesha ndoa hii ni halali



Hili tukio la kihistoria lilifanyika katika kanisa la TAG Magomeni tar 13-04-2014 Amosi alipofunga pingu za maisha na kudhihilishia uma kuwa sasa yeye kabadilishwa na yesu na sasa ana maisha mapya.










Asante za nguvu kwa Martin Malecela

 Kama hukuona habari za Amosi baada tu ya kuacha ushoga FUNGUA HAPA        na pia kama Hukuiona habari ambapo huyu jamaa alikuwa anamvisha pete ya uchumba FUNGUA HAPA
 

Comments