KWAHERI DEBORA JOHN SAID, KAZI YA MUNGU ULIIFANYA NA MATUNDA YANASTAWI.

Mchungaji na mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania Debora Said amekuwa dunia tangia mwaka 1972 na mwaka huu wa 2014 Juni Mungu amemchukua kwa mapenzi mema. Mch.Debora Said amefanya kazi yake akiwa duniani, amewaleta watu wengi kwa Yesu kwa njia ya uimbaji na uchungaji wake, ameisaidia familia yake mbali na huduma yake ya uimbaji na uchungaji.

Katika sherehe hii ya kumuaga Mch. Debora Said kulikuwa na waimbaji weng0i sana, baadhi yao ni Upendo Nkone, Victor Aron, Joshua Makondeko, Chidumule, Neema Gasper, Madam Ruti, Lungu la Yesu, Addo November, Christina Matai, Miriam Lukindo, Chriss, Martha Mwaipaja, Kyambiki, Petro, Apostle Gideon Mutalemwa, Upendo Kilahiro, na wengine wengi sana.
Askofu John Said mume wa marehemu Mch. Debora Said
Siku hii ilikuwa ni siku ya furaha na shangwe kwa kumuaga mtumishi wa Mungu Debora Said, waimbaji waliweza kuimba kwa furaha na bila kuonyesha huzuni. Lakini haikuishia hapobali watu wengine walionekana wakitoa machozi na kulia kwa sauti, na hii inaonysha ni jinsi gani Mchungaji  Debora Said alikuwa mchango mkubwa Tanzania na Afrika nzima.
Katika sherehe hii kulihudhuriwa na wachungaji wengi sana kwaajili ya kumuaga mpendwa wetu Mch. Debora Said. Wachungaji waliweza kutoa maneno machache kukuhisiana na msiba huu na wengine walionekana wakishindwa kujikaza na badala yake machozi yakiwatoka.
Rulea Sanga aliyekaa na shart nyeusi akitafakari
Tunamshukuru sana Mungu kwa kumpa ujasiri mume wake na marehemu Askofu John Said, alionekana ni mtu mwenye ujasiri kwa sura na akiwa na matumaini ya kwamba mke wake ametwaliwa na Mungu wetu wa mbinguni. Kibinadamu inaumiza sana kuona yule uliyekuwa unamtegemea kimawazo ametoweka duniani. Hakika huu ni wakati mugumu sana kwa Askofu John Said na kanisa lake zima kwa maana wameondokewa na mtu ambaye alikuwa kama nguzo ya kanisa.

Kwa wasiojua, ni kwamba marehemu Mchungaji Debora Saidi alikuwa ni mwimbaji, Mchungaji na pia mwanamichezo (netball). Kutoakana na taarifa tulizopata msibani ni kwamba alijituma sana katika ujuenzi wa kanisa lao na pia alikuwa muhimizaji mkubwa katika swala zima la michezo.
Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Addo November aliwaomba waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania waache tabia ya kujiona mastaa na kujitenga na wengine wakati wa raha na shida. Alisema anayeweza kukuweka wewe kuonekana staa ni Yesu Kristo tu na sio mwanadamu, Mungu anaweza kukushusha na kumuinua mtu mwingine kwa kazi yake. Pia aliwataka wasijifananishe na watu wa Bongo Fleva kwani wao ustaa mara nyingi wanategemea votes za mashabiki na asilimia kubwa hawategemea kutoka kwa Yesu Kristo. Rais aliwashukuru waimbakji wote kwa usirikiano wao katika zoezi zima la kumuaga mtumishi wa Mungu Mch. Debora Saidi.

Mch mama Fednandes wa kanisa la AGAPE alitoa ofa ya kurusha matukio ya msiba huu wote katika kipindi cha FIRE katika television cha ATN  na pia ameandaa tamasha kubwa la waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania hapo kanisani kwake.

KIPINDI CHA KUPELEKA MWILI WA MAREHEMU MCH. DEBORA SAID KANISANI








Wa pili kutoka kushoto ni Askofu John Said mume wa Marehemu Mch. Debora Said akijianda kuingia Kanisani




WAIMBAJI WAKISHREKEA SIKU YA PEKEE YA KUMUAGA MWIMBAJI MWEZAO MCH. DEBORA SAID
 Tumaini Njole akimsindikiza rafiki yake Mch. Debora Saidi
Edson Mwasabwite akisema bye bye Debora Said huku akiimba wimbo wa Ni kwa Neema tu
MC Joshua Makondeko
Kwaya ya kanisa la Maisha ya Ushindi kwa Askofu John Said

Waimbaji kutoka Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) wakiimba wimbo maalum wa kumuaga mpendwa wao marehemu Debora Saidi

Edson Mwasabwite

Apostle Gideon Mutalemwa

 Christina Matai hakuweza kujizuia, alijishtukia analia wakati waimbaji wenzake wakiimba. Hii inaonyesha ni jinsi gani alipigwa na kifo cha marehemu Mch. Debora Said

 Sifa John
Kutoka kulia ni Victor Aron
Upendo Kihariro

Lungu la Yesu




Mchunga Anton Lusekelo (Mzee wa Upako)
Mchungaji Anton Lusekelo "Mzee wa Upako" (aliyekaa)
 Mwimbaji wa nyimbo za injili Petro aliyevalia koti la draft
 wa kwanza kutoka kwenye nguzo ya kanisa ni mume wa Upendo Kilahiro
wa pili kutoka kushoto mstari wa kwanza ni mwimbaji Orida Njole


Mume wa Martha Mwaipaja (kulia) akiwa na mke wa Mtume Fidnandes wa ATN



Mchungaji Harisi Kapiga

MATUKIO MBALIMBALI YAKIENDELEA NJE YA KANISA WAKATI SHEREHE IKIENDELEA KANISANI



 Victor Aron (mwenye tshirt nyeusi akiwa na baadhi ya marafiki wakibadilishana mawazo
 Baadhi ya waimbaji walioamua kupiga picha ya kumbukumbu


 MC Joshua Makondeko mwenye kitamba cha bendera ya taifa akiwaelekeza wenzake ratiba ya waimbaji
 Miriam Lukindo (kushoto.gauni nyeusi) na kulia ni Tumaini Njole
Mwimbaji wa Gospel Tanzania Furaha Isaya (kulia)

 Gideon Mutalemwa akichukua namba za simu kutoka kwa mtumishi wa Mungu Datson

 Sarah Mvungi akifanya mawasilia

KIPINDI CHA KUOMBEA CHAKULA


 Upendo Kilahiro (wa pili kutoka kulia) akiongea na rafiki yake





KIPINDI CHA KUTAMBULISHA WACHUNGAJI NA WAGENI MBALIMBALI




 Wachungaji, mitume na viongozi mbalimbali (waliosimama)
Waliosimama ni wake wa wachungaji
"Nyamayao" wa tatu kutoka kushoto
 Bloga na mtangazaji wa WAPO REDIO Silas Mbise akifanya kazi ya Mungu

 Mchungaji Mama Finandesi wa ATN akisema jambo
Askofu John Said akiwa na mwanae

 Rais wa Chama Cha Muziki Tanzania (CHAMUITA) Addo November akiwashukuru waimbaji kwa kujitolea kufika katika msiba huu. Pia aliweza kusema waimbaji waache kujiita mastaa kwa anayekupa ustaa ni Yesu Kristo na sio mtu mwingine. Leo unaweza kuonekana unang'aa lakini kesho Mungu akamuinua mtu mwingine.

ASKOFU JOHN SAID AKIWA AMEMKARIBISHA MAMA HUYU KUSEMA JAMBO KUHUSIANA NA KIFO CHA MKE WAKE
Mama huyu alionekana kulia wakati wote hata ulipofika wakati wa kula chakula bado alionekana kulia huku akila chakula. Mama huyu alishikwa na uchungu mkubwa kwa kutwaliwa kwa marehemu Debora Said
 Kulia ni Askofu John Said
Askofu  John Said


 KIPINDI CHA KUOMBEA WATU WALIOWEZA KUOKOKA SIKU YA MAZISHI YA MCH. DEBORA SAID



Comments