AFYA YA BAHATI BUKUKU YAZIDI KUIMARIKA NA WALA HAJAVUNJIKA MGONGO

Hali ya mwimbaji wa nyimbo za injili Bahati Bukuku inazidi kuimarika na kuendelea vizuri kama GK ilivyomshuhudia akiwa nyumbani kwake Tabata, akiwa mwenye furaha kuwaona watu mbalimbali wakiwemo waimbaji wenzake ambao wameenda kumjulia hali.
Bahati Bukuku akiwa amekaa nyumbani kwake

Bukuku ambaye kwa sasa anaendelea kuutibu mgongo ambao umepata maumivu na wala haujavunjika kama taarifa nyingine zilivyosambazwa.. Pia GK ilimshuhudia akiwa amekaa na marafiki zake huku akiendelea kumshukuru Mungu aliyewaepusha  na ajali hiyo.

Bukuku anasema kama sio Mungu kuingilia kati basi sasa hivi ingekuwa habari nyingine, kwani mara baada ya lori kuwagonga alijaribu kutoka katika gari alilokuwemo lakini alishangaa anashindwa kuamka ndipo alipogundua kuwa ameumia mgongo lkn kwa sasa hali yake inaendelea vyema. Pia dereva wa gari hilo Edson Mwakabungu ambaye aliumia mguu anaendelea vizuri pamoja na kijana Frank ambaye alipata jeraha dogo kichwani naye anaendelea vyema.

Zifuatazo ni picha zikimuonyesha Bahati Bukuku akiwa na ndugu na marafiki mbalimbali waliofika nyumbani kwake kumjulia hali.
Jennifer Mgendi akizungumza na Bahati

Ambwene Mwasonge akimjulia hali

Gospel Kitaa (GK) ikijadili jambo na Bahati

Irene Mwamfupe (kushoto) pamoja na Ikupa Njela (kulia) wakiwa pamoja na rafiki yao Bahati


Edson Mwakabungu ambaye alikuwa dereva na kuumia mguu katika ajali hiyo akiwapasha kilichojiri marafiki zake

Edson Mwasambwite (kulia) akiwa na Aliko nao walifika kumjulia hali
Ambwene Mwasongwe akisalimia ndugu mbalimbali waliofika

Emanuel Mgogo (mwenye shati jekundu) aliyeimba wimbo unaoitwa Msikilize Mungu akizungumza na Edson
  
MAOMBI YAKAMIMINWA
 


Gospel Kitaa tunamwamini Mungu ambaye ameanzisha kufanya uponyaji kwao, ndiye atayekamilisha. Endelea kuwakumbuka katika maombi kwani Mungu anasikia na anajibu.

Comments