DHAMBI YA KUZINI NI MAKOSA MAKUBWA.






BWANA YESU asifiwe ndugu yangu.


Karibu tujifunze ujumbe huu kuhusu  kuzini, jambo ambalo huwakosesha wengi sana.


-Kuzini ni kitendo cha kufanya mapenzi ambacho ni dhambi.

-Anayezini ni kahaba, mwasherati , Malaya, changudoa na mzinzi.

-Mzinzi ni mtu aliyeoa au kuolewa anapozini na mtu ambaye siye mkewe au mmewe.

-Mwasherati ni mtu Yule asiyeoa au kuolewa anapozini na mtu na mtu mwingine huo ndio uasherati.

-Kahaba ni mtu Yule anayezini na watu wengi au kujiuza kwa lengo la kujipatia kipato. 



1 Kor 6:18 (Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. ).


-Watu wengi kwa sababu ya uzinzi wao au uasherati wao huitwa viwembe.

Hii ni dhambi mbaya ana Kumb 5:18 MUNGU anasema ‘’ Wala Usizini’’

-Dhambi hii imewaharibia wengi uhusianao wao na MUNGU.

-Wengi wamekosa Baraka zao kwa sababu ya uzinzi.

-Wengi wamekufa kwa sababu ya kuzini.

-Wengi wako kuzimu sababu ya kuzini.

-Kuzini ni jambo baya sana.



                              VYANZO VYA UZINZI.




1.  Chanzo cha kwanza cha uzinzi ni TAMAA.



Kumb 5:21 ( Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu cho chote alicho nacho jirani yako. )

Usitamani mke wa jirani yako, tamaa hii ya wake za watu ni mbaya sana ni ni chanzo kikubwa cha uzinzi.

Yakobo 1:13-15 ( Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na MUNGU; maana MUNGU hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. ).

Tamaa ikiwa ndani yao inauwezo wa kunena na kuongea , pia shetani anaanza kukuhubiri juu ya kufanya uovu.
Tamaa inazaa dhambi, dhambi inazaa mauti.
Tamaa ndi mbaya sana.

Mathayo 5:27-32( Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini. )



2.  Chanzo cha tatu cha  uzinzi ni MAVAZI


                   1 Petro 3:1-5 ( Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;  wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.  Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;  bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za MUNGU.  Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini MUNGU, na kuwatii waume zao. ).
mavazi ya kujistiri ni muhimu sana.

                        Yeremia 31:22 (Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume. ).

Mwanamke anatakiwa amlinde mwanaume kwa kutovaa nguo za mitego. 

3. Chanzo cha 3 cha uzinzi ni KUKAA SEHEMU MOJA KWA MUDA MREFU MKIWA WAWILI TU WA JINSIA TOFAUTI.


Wagalatia 5:16  (Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. ).

Mithali 15:1-2 ( Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.  Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.).



4. Chanzo cha pili cha uzinzi ni UBINAFSI.


Ubinafsi humfanya mtu awe anataka kila msichana/ mvulana awe wake.

Ubinafsi humfanya mtu kujipendelea kila kitu na hivyo huwafanya wabinafsi wengi kujipendelea pia kutenda dhambi hii.

Unamuona msichana amejitunza na wewe moyoni mwako unawaza kwamba anatayemuona msichana huyu atafaidi sana na hiyo inakupelekea kutaka kumwoa kwanza wewe huyo msichana kabla hajaolewa na mtu sahihi. Na kama msichana huyo naye hana hofu ya MUNGU ndio kabisa wewe pamoja na ubinafsi wako mnazaa dhambi na dhambi hiyo inakuwa na madhara kwako na kumharibia maisha msichana wa watu.



5.Chanzo cha 5 cha uzinzi ni KUWA KATIKA ENEO AMBALO HUTAKIWI KUWA KWA WAKATI HUO.


      2 Samweli 11:1-12 (Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Daudi akampeleka Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote; wakawaangamiza wana wa Amoni, wakauhusuru Raba. Lakini Daudi mwenyewe akakaa Yerusalemu. Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.  Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?  Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake.  Yule mwanamke akachukua mimba; basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja-mzito.  Ndipo Daudi akapeleka kwa Yoabu, akisema, Unipelekee Uria, Mhiti. Naye Yoabu akampeleka Uria kwa Daudi.  Uria alipomwendea Daudi, Daudi alimwuliza habari za Yoabu, na habari za watu, na habari za vita.  Daudi akamwambia Uria, Haya, shuka nyumbani kwako, ukanawe miguu yako. Basi Uria akatoka katika nyumba ya mfalme, na tunu ya vyakula ikamfuata, iliyotoka kwa mfalme. Lakini Uria akalala mlangoni pa nyumba ya mfalme, pamoja na watumishi wote wa bwana wake, wala hakushuka nyumbani kwake. Watu walipomwambia Daudi ya kwamba, Uria hakushuka nyumbani kwake, Daudi akamwambia Uria, Je! Hukutoka safarini? Mbona hukushuka nyumbani kwako? Naye Uria akamwambia Daudi, Sanduku, na Israeli, na Yuda, wanakaa vibandani; na bwana wangu Yoabu, na watumishi wa bwana wangu, wamepiga kambi waziwazi uwandani; nami niende nyumbani kwangu, kula na kunywa, na kulala na mke wangu? Uishivyo, na kama roho yako iishivyo, mimi sitafanya jambo hili. Basi Daudi akamwambia Uria, Ngoja hapa leo tena, na kesho nitakuacha kwenda zako. Basi Uria akakaa Yerusalemu siku ile, na siku ya pili yake. )
Daudi alikaa katika eneo ambalo sio sahihi na ikapelekea uzinzi, hata leo wapo watu hukaa kwenye mitego ya watu wabaya na kupelekea uzinzi.
 

  Waefeso 5:15-17 (Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. ).



6. Chanzo cha 6 cha Uzinzi ni MAZUNGUMZO YASIYO NA KIASI.


Mazungumzo yasiyo na kiasi ni mabaya sana maana adui kidogo kidogo ataanza kuwawekea dhambi ndani ya mioyo yenu. Ndio maana unatakiwa kuwa na kiasi maana shetani yuko vitani ili akuangamize. Wengi wameongea hadi story nzuri zikaisha na kuanza kuongea pumba tu na kuwapelekea dhambi.





7. Chanzo cha 7 cha uzinzi ni KUIGA 


     Wadada wengi wamepata mimba na kuharibiwa mosomo yao kwa  kuiga kutoka kwa wenzao ambao shetani amewavaa na kufanya uovu huu.

Sio kila jambo ni la kuiga mengine ni mambo mabaya na ya kifo.



MUNGU anautazamaje uzinzi.




      1.Uzinzi ni ubaya mkubwa.





2.  Uzinzi ni jeraha la fedheha.

  (Mithali 6: 32-33 ( Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika. )



          EPUKA DHAMBI YA UZINZI.

1 Kor 6:9-10 ( Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. ).



Ufunuo 21 :8 (Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. ).




Mithali 1:28 -31 (Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione. Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha BWANA. Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote. Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe. ).





Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292
                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
 MUNGU Akubariki.

Comments