JOSEPHAT MWINGIRA: JINSI NILIVYOTOKEWA NA BWANA YESU: AKIWA MBINGUNI MWINGIRA ANAONYESHWA JINSI MAPEPO YANAVYOFANYA KAZI PIA APELEKWA KUZIMU NA KUONA KILA KITU.(3)



BWANA YESU asifiwe ndugu zangu.

Leo tunaendelea na sehemu ya 3 ya ushuhuda wa mtumishi wa MUNGU Josephat Mwingira, mbeba maono wa huduma ya Efatha yenye makanisa zaidi ya 200 hadi sasa. Kama hukusoma sehemu ya pili ambapo Malaika alikuja kumchukua Duniani na kumpeleka mbinguni FUNGUA HAPA

Leo ni sehemu ya 3 ambapo akiwa mbinguni anapewa kazi na BWANA YESU na baadae anapelekwa kuzimu na baadae anaonyeshwa jinsi mapepo yanavyofanya kazi .
Karibu
 
KUSUDI LA WITO WANGU
1.  Kuwafungua waliofungwa
2.  Kuponya wagojwa na wenye misiba mbalimbali
3.  Kuwafunulia watu siri za uzima wa milele
4.  Kuwatayarisha watu tayari kwa kunyakuliwa. Katika kuwatayarisha watu, kuna mambo ambayo alinieleza kufanya
5.  Kuwaweka watu kwenye nafasi zao za utumishi. Yaani, kumpanga kila mtumishi kulingana na wito uliopo ndani yake, kuanzia wito wa juu mpaka wa chini, ili kila huduma isaidie kufikia kusudi la wito wake. 

                     Napewa KUSUDI nililoitiwa

Akaanza kunieleza KUSUDI aliloniitia. Akaniambia kuwa KUSUDI kubwa aliloniitia lilikuwa kunionyesha mambo yote yanayohusiana a UUmbaji yalivyo. 

                        Mambo ya Uumbaji yalivyo

Akanionyesha mambo ya Uumbaji yalivyo kuanzia mwanzo, kama kitabu cha Mwanzo kinavyosema. Halafu akanionyesha mwisho, kama kitabu cha Ufunuo kinavyosema. Akanieleza juu ya Kitabu cha Ezekiel na Kitabu cha Daniel kinachozungumzia mambo ya kwanza na mambo ya mwisho. Akanieleza jinsi mwanadamu alivyokuwa. Akanieleza habari za Luciferi na jeshi lake linavyofanya kazi. Akanieleza mabo mengi mazito ambayo alitaka mimi niyajue.
Nilipomuuliza kwa nini alikuwa ananijulisha mambo yale mazito, akasema, “wewe utakwenda kuyafanya haya kwa ajili ya ndugu zako!” na akaongeza kuniambia, “Wewe umejaliwa haya ili ukayafunue huko, maana umejaliwa kuzijua siri za MUNGU, na umeamriwa kuzijua. Sio wote waliojaliwa haya; lakini wewe umejaliwa kuzijua”. Halafu akaniambia jinsi mwanadamu ambaye hajaokoka alivyo: hali kadhalika aliyeokoka anavyokuwa. Yaani, akanionyesha moyo wa mwanadamu na mawazo yake – yaani mambo anayowaza. Akanifundisha vitu vingi mno. Kitu kingine ambacho nakumbuka, alisema, “Kila atayekusikia”, sasa haya aliyasema mwisho, “na atakayefanya utakachosema, atajaliwa thawabu”. 

               Naonyeshwa kuzimu na BWANA YESU

Kutoka pale, akanipeleka kwenye eneo linguine, akanipleka kuzimu ili nione kulivyo. Hilo lango la kuzimu lilifinguka lenyewe. Akanionyesha, na mimi mwenyewe nikaona mafunza mkubwa kama ngumi. Makubwa, halfu yana uwezo wa kuruka. Nikawasikia watu wanapiga kelele na nikawaona wanalia kweli. Kuna giza kubwa sana huko, unawaona funza wanatoka upande mmoja kwena ubande mwingine, wakiendea hao watu wanaolia. Wanapofika, hata kama ni mgongoni, basi wanatoboa na kuingia kwenye migongo ya wale watu. Baada ya hapo, unasikia wale watu wanapiga kelele sana kwa uchungu. Funza hao wantoboa toboa kila sehemu za miili, na kila wanapotoboa, unasikia kelele za hao watu wakilia.
Nikamuuliza BWANA YESU, “Hii ni nini?” Akasema, “Ni mateso wanayoyapata watu huku kuzimu”. Nikauliza tena, “Je, ina maana hii ndiyo itakavyokuwa adhabu yao mmilele?” Akasema, watakapopelekwa katika Jehanamu ya moto, huko ndiko watakaa milele na milele”.
BWANA YESU ana ‘Nguvu’ isiyo ya kawaida. Hakuna mahali ambapo hawezi kuingia. Usifanye mchezo, YESU ana nguvu! Yaani hata kama ni mlango, mnapokaribia, kule kusogelea tu, mlango huo unafunguka wenyewe. Yaani YESU ana Nguvu, hana cha mchezo. YESU ana Nguvu! Yaani hata na mimi niliyashangaa sana niliyoyaona kule kuzimu kuhusu Nguvu zake. Wakati tulipokuwa tunatembea kule kuzimu, tulipofika mahali na tulitaka kukaa kidogo, tulikuwa tunaona kiti chake YEYE kimekwesha kufika na amekwesha kukaa, hakuna mtu aliyekuwa anakileta. Na mimi nikaangalia kwa makini kile ambacho BWANA YESU alikuwa anakifanya. Kumbe, nikaonyesha hali ya kutaka kukaa, nikona kiti kimekwisha kufika, nikakaa!.
Baada ya hapo, tukaondoka na kuelekea upande wa pili wa kuzimu, yaani katika eneo la lango la Jehanamu ya moto. Huko nikaonyeshwa moto mkali unaowaka, ingawa hakukuwa na watu, kwa sababu moto unasubiri siku ya mwisho. Katikati ya Jehanamu, kulikuw ana barabara kubwa sana ambayo tuliivuka. Tukaondoka kutoka eneo hilo, na BWANA YESU akanirudisha tena karibu na eneo la kuzimu. Hapo akalifungua lile lango, akanionyesha Lucifer. Ndipo nilipomuona Luciferi akiwa anafanana nap aka mkubwa. Kichwa chake kilikuwa kimepasuka mfano wa alama ya msalaba. Nikamuuliza BWANA YESU, “Kwa nini kichwa cha Luciferi kimepasuka?” Naye akanijibu, “Hali hii ilitokea saa tisa alasiri, siku ile pale msalabani, wakati lile pazia lilipasuka. Tukio hilo, liliharibu kabisa mawazo ya Lucifari (shetani)” . ukisoma katika kitabu cha wokorintho (2Kor. 10:4-5), Mtume Paulo anasema maneno ya ajabu sana. “Silaha za vita vyetu si vya mwili, bali zinauwezo katika MUNGU hata kuangusha ngome. Tukiangusha fikra na mawazo”.
Kuanzia siku ile, pazia lilipopasuka pale msalabani, BWANA YESUalimshinda kabisa setani katika mamlaka yake na ufalme wake. Ndiyo maana anatuambia alitupa mamlaka na ufalme. Yaani alimunyang’anya shetani mamlaka yake na ufalme wake na kutupatia sisi. BWANA YESU akaniambia, “Shetani hana kitu chochote anachoweza kumshindia mwanadamu. Anachofanya shetani, ni kuwahi mawazo ya mwanadamu, na fikra zake, na nia ya moyo wake. Akishafanikiwa kukamata mawazo, fikra na nia ya moyo wa mwanadamu, hana uwezo wa kutenda jabo jingine lolote kwa mwanadamu kinyume na mapenzi ya MUNGU. 

Naelezwa jinsi mapepo yanavyofanya kazi

Tukatoka sehemu ya Luciferi na kwenda sehemu ya mapepo. Akanionyesha jinsi mapepo yanavyofanya kazi. Huyu Luciferi, naye, anajeshi lake, lenye makundi mengi. Katika kuyahesabu, nikakuta kuna makundi kama mia mbii na hamsini hivi. Kila kundi lina mamlaka yake, lina utendaji wake, na lina nguvu zake.
Luciferi hakusema kitu. Nilichoshangaa. BWANA YESU allinipeleka kwenye eneo lingine ambalo pia yako mapepo. Yaliponion mimi na BWANA YESU, yakasujudu. Yaani, yaliinana kabisa. BWANA YESU akaniambia, “Ndiyo yatakavyokwenda kutenda mbele yako! Yaani, yataslimu amri mbele zako. Yatakuinamia”.
Nikaw anavishangaa vitu hivi na mambo haya. Wakati tunamsogelea Luciferi, alikuwa mbali lakini katika ulimwengu wa kiroho hakuwa mbali, alionyesha hali ya unyenyekevu, kama mtu ambaye anaonyesha heshima ya kupita ‘Bwana Mkuwa’. BWANA YESU akanikumbusha Neno lililoko kitabu cha Efeso (Efes. 6:11-14) linalosema, “Vita vyetu si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya ‘flme’ na ‘mamlaka’…”. Ukisoma pale utaona kuna pointi za msingi tano. Zile pointi, ndizo zimegawanyika katika lile jeshi la kipepo. Yamegawanywa katika makundi hayo mia mbili hamsini yenye majukumu tofauti. Mengine yanapambana juu ya ndoa, mengine yanapambana juu ya watoto, mengine yanapambana juu ya makabila ya watu, mengine yanapambana juu ya uchumi, mengine yanapambana juu ya Watakatifu, na kadhalika. Kwa hiyo, usipoelewa unapambana na mapepo ya aina gani, inakuwa taabu kuyashughulikia. 

                               Mamlaka tatu

Tulipotoka pale, kwenye sehemu ya mapepo, akanipeleka katika eneo ambalo linamazingira Fulani – kitu cha msingi cha kufahamu ni kwamba shetani hatawali eneo linguine zaidi ya eneo la giza. Hii dunia unavyoiona, imegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza ni ‘Utawala wa MUNGU’ ambayo unamilikiwa dunia nzima, na hata utawala wa ‘Mamlaka yashetani’ uko chini ya hiyo mamlaka. Sehemu hii, tunaiita ‘Ufalme wa MUNGU’. maana, pia, ili shetani afanye kazi vizuri, ni lazima aombe kibali kutoka mamlaka hiyo. Halafu, kuna mamlaka ya Kishetani ambayo tunaiita ‘mamlaka ya giza’ kasha, kuna ‘mamalaka ya wanadamu’ ambayo iko chini ya mamalaka ya Uumbaji. Mamalaka hii tunaiita ‘Ulimwengu wa asili’. Mamlaka hii nayo, ina utendaji wake na nguvu zake.
Lakini mamalaka zote ni za MUNGU. Kati ya hizi, ni mamalaka mbili tu, mmlaka ya asili na ile mamalaka ya giza, ndizo zinazoshindana. Mamalaka hizi zinashindana kwa sababu mamalaka ya giza, yaani Lucifer, alinyang’anywa mamlaka yake, akapewa huyu mwanadamu. Sasa Luciferi anapambana ili kumnyang’anya huyu mwanadamu mamlaka hiyo, akifanikiwa kumlaghai. Luciferi anaweza tu kumteka mwanadamu pale anapofanikiwa kushika mawazo, fikra na nia ya mouo wake. Hivyo, akishakamata mawazo ya mwanadamu, anaweza kumfanya huyu mwanadamu afanye dhambi, yaani mambo ya giza. Kwa hiyo, ikishafika hapo, mwanadamu anakuw akatika hali hiyo ya uovu na katika mazingira hayo. Lakini asipokuballi kukamatwa katika yale mawazo, mwanadamu anabaki katika mazingira yake, anatakiwa akubali kuenenda sawasawa na maandiko ya Bibilia yanavyosema. Kwa kufanyahivyo, nia yake inakuwa ni nia ya MUNGU. Mwanadamu, kwa ujumla, kabla hajakubali hilo, anaweza akawa hamjui MUNGU kabisa, lakini nia ya moyo wake ikawa ya kutenda mema. Kwa hiyo anakuwa hajakamatwa na huyu mfalme wa giza, ambaye ni Luciferi. 

 ITAENDELEAAAAA.....................
Usikose sehemu inayofuata hapa hapa Maisha ya ushindi blog pia unaweza kwenda Efatha na ukanunua kitabu hicho hapo chini ambacho ndio kina ushuhuda hu wote. MUNGU akubariki sana na endelea kutembelea hapa
 
WAKATI WA MKESHA EFATHA KIBAHA.

Comments