MTU ANAYEKUPENDA ATAKUJALI KWA KADIRI YA UWEZO WAKE, ATAKUTHAMINI KWA KADIRI YA UWEZO WAKE, ATAKULINDA KWA KADIRI YA UWEZO WAKE!


Hii alama iko wazi sana tukiihusisha na maisha yetu katika kujua ukweli wa hiki nikisemacho! Na mambo haya hayakwepeki kufundishana na kukumbushana! Kwasababu, upendo unatenda kazi sehemu zote; kwa marafiki, ndugu na kwa sehemu tulizozizoea!
Kitu unachokipenda huwezi kukiweka ovyoovyo, huwezi kukiweka mahali popote, wakati mwingine huwezi kumruhusu mtu yeyote tu akitumie au hata kukishika! Na zaidi sana utakuwa muangalifu wakati wote kwa kukijali na kukitunza, utakuwa makini sana katika kukilinda!
Photo
Na Marko Bashiri
Ndivyo inavyokuwa kwa mtu unayempenda au anayekupenda, atakujali sana kwa kadiri ya uwezo wake! Nasema tena " Atakujali na kukutunza na kukulinda kwa KADIRI YA UWEZO WAKE.." Kujali kunaambatana na mambo mengi! Kunaambatana na kusikiliza na kutii! Kama mtu anaongea halafu wewe unakuwa unafanya mambo yako; huko sio kumjali mtu! Hizo ni dalili za dharau, ndio maana ni rahisi kusikia " Mi naongea yeye wal hata ajali anafanya mambo yake..." Ile hali ya kusikiliza kwa kile mwingine anachosema au kuzungumza, huko kunaonyesha kujali na ndio moja ya alama muhimu ya upendo! Kumjali mtu sio lazima uwe na pesa! Ni kwa kadiri ya uwezo wa mtu! Maana wako watu wanatoa pesa na hawapendi wala hawajali! Ni kwasababu pesa zipo na hana choyo au amezoea kuhonga anatoa tu! Ili apate anachokitaka au aendeleza anayoyataka lakini ndani mwake hakuna upendo wowote ule! Anayekupenda atakuthamini, atakuweka katika daraja la juu sana na kukutunza na kukulinda! Yote hayo atayafanya kwa kadiri ya uwezo wake, atakutunza kwa kadiri ya uwezo wake! Haitowezekana yeye avae vizuri huku anakuangalia wewe huna chochote, labda kama mwingine hapendi anapenda kuwa kawaida! Haiwezekani yeye ale vizuri huko kwenye mizunguko yake halafu wewe huku unakula chakula cha shida au unakula chakula cha siku iishe wakati yeye anakula vinono! Anakulia hotelini akija huko anajifanya hali sana, kumbe ameshakula vinono!
Mtu anayekupenda kweli! Atakuthamini, atakutunza na kukulinda katika vipindi vyoote kwa kadiri ya uwezo wake, ukiwa kitandani hujiwezi kwasababu ya kuugua, atakujali, atakuthamini, atakutunza na kukulinda pamoja na kutapika kwako yeye haoni kinyaa, ndio kwanza atahakikisha unakuwa msafi! Upendo ndivyo ulivyo, haihitaji kulazimisha! Upendo ndivyo ulivyo!
SHARE na marafiki zako!
By Marco Bashiri

Comments