MWIMBAJI MKONGWE WA NEW LIFE BAND YA ARUSHA AFARIKI DUNIA

Eglah Bavuma enzi za uhai wake.
Mwimbaji na mpigaji wa bendi maarufu ya injili nchini ya New Life Band Eglah Bavuma hatunaye tena duniani baada ya kufariki asubuhi ya leo majira ya saa kumi na mbili katika hospitali ya Mount Meru jijini Arusha alikokuwa amerejeshwa kupewa matibabu.

Egla pamoja na wenzake wamekuwa waimbaji wa muda mrefu wa bendi hiyo toka alipotokea kwenye bendi ya Amana Vijana Centre iliyokuwa chini ya kanisa la Pentecoste City Center likiongozwa na mchungaji Abel Orgenes. Licha ya kushiriki katika matukio mbalimbali ya kihuduma na bendi hiyo, pia marehemu ni mmoja kati ya waimbaji waliofanikisha kutoka kwa kanda mpya ya bendi hiyo iitwayo 'Nimejenga Mwambani'.

Taarifa za awali kutoka kwa mchungaji Abel Orgenes zinasema wale wote waliowahi kumfahamu Egla jijini Dar es salaam, wanatakiwa kufika Amana Vijana Centre Ilala majira ya saa 10 jioni.

Hapa unaweza kumuona Eglah akiwapa tafu Tumaini Choir Arusha kuwapigia drums ndani ya studio za New life Band. habari ni ni kwa niaba ya Gospel kitaa blog







Comments