MWINJILISTI JOHN CHINYULI AFUNGA NDOA.

Hapo vipi? hapo poa sana, tena hilo pozi limekaa poa sana.
Ilikuwa ni shangwe na furaha kuu kwa watumishi wa MUNGU Mwinjilisti John Richard Chinyuli pamoja na dada Sehewa Joseph Wilison baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la Anglican Ukonga Mazizini.
Maisha ya ushindi tulikuwepo na hakika ilikuwa ni moja ya harusi za kuvutia sana ambazo mimi nimewahi kushiriki, Watu walikuwa wengi na kila mtu alikuwa na furaha kuu, Neno lenye nguvu za Roho mtakatifu lilitolewa na pia waimbaji wakali wa nyimbo za injili walikuwepo.
Baada ya ndoa kufungwa kanisani, kulifuatiwa na zoezi la upigaji picha za kumbukumbu na baadae kulikuwa na sherehe kubwa sana katika ukumbi wa Moshi. Kama unasikiaga watoto wa mjini wakisema ''Tumekula na kusaza'' ndivyo ilivyokuwa katika harusi hiyo ya watumishi wa MUNGU. Maharusi walipendeza, Mandhari ilikuwa nzuri sana, wageni waling'aa na mshereheshaji alikuwa wa ukweli.
MUNGU awabariki sana John Chinyuli na Sehewa Wilson na kwa niaba ya Maisha ya ushindi team, Mimi Peter nawatakia maisha marefu na yenye furaha kuu katika ndoa yao.
ALICHOKIUNGANISHA MUNGU, MWANADAMU ASIKITENGANISHE.
Pia Mwinjilisti John Chinyuli ni mmoja wa wahubiri wa neno la MUNGU katika blog hii.
Kila la heri Mwinjilisti John Chinyuli na Dada Sehewa Wilison.
Zifuatazo ni baadhi tu ya picha katika matukio kadhaa wakati wa ndoa hiyo ikifungwa.
Mwimbaji nyota wa nyimbo za injili akiimba  huku amekaa miguuni kwa maharusi.

Mwinjilist John Chinyuli akisaini cheti cha ndoa.

Sehewa Wilson akisaini cheti cha ndoa.

Mwimbaji wa nyimbo za injili Beatrice mara baada ya kuimba.

Maharusi baada ya kumaliza kusaini vyeti vya ndoa.

Bibi harusi Sehewa Wilson akiwa katika pozi wakati wa Neno

Mchungaji akiwapa vyeti vyao vya ndoa.

Furaha kwa sana tu.

Gari ya maharusi ikiwa tayari kabisa kwa kwenda ukumbuni.

Bi harusi ndani ya gari tayari kwa safari.

Hawa watoto ni wataalamu wa kucheza sijapata kuona, wakisafisha njia kwa kucheza ili maharusi wapite.

Nimekuchagua wewe uwe wangu wa maisha.

Maharusi ndani ya zulia jekundu na kwa nyuma ni vigeregere visivyo na idadi.


Maharusi pamoja na wasimamizi wao.


Maharusi wakimsikiliza MC



Mwinjilisti John Chinyuli akiwatambulisha ndugu zake

Hata ndafu pomba ilikuwepo.


Katikati ni Scholar Mungusa kutoka Maisha ya ushindi akiserebuka kwaito ya YESU pamoja na wageni wengine .

utapenda tu hata kama hutaki.


Maharusi pamoja na wana kamati.

Mwenyekiti wa kamati akitoa shukrani.

Mzee wa kanisa akisema machache.

Maharusi walipewa Zawadi ya Biblia kwa John na Tenzi za Rohoni kwa Sehewa. na kutakiwa John ahubiri kwa dk 2 na Sehewa aimbe tenzi moja . John alisoma 1 Samweli 17:34-36 na Sehewa aliimba Tenzi namba 117 inayosema TUFANI INAPOVUMA. Hakika walifanya vyema kila mmoja .

Mwinjilisti akihubiri.

Sehewa akiimba tenzi.

Comments