UTAMLAUMU NANI?

MUNGU alisema nami wiki iliyopita Kwamba " Roho Yangu Haitashindana Na Mwanadamu Milele- Mwanzo 6:3. Hiyo Ni Tahadhari Muhimu Zaidi Kwa Wanadamu Wote, Ee Mwanadamu Unayefanya Uovu Ukisema Hakuna Mwisho, Pole Sana Na MUNGU Ameniambia Hatashindana Na Mwanadamu, Chunga Ndugu Usije Kulala Duniani Ukaamkia Jehanamu. 

BWANA YESU Leo Amesema Hivi " Yeye Anikataaye Mimi, Asiyekubali Maneno , Anaye Amhukumuye ; Neno Lile Nililolisema Ndilo Litakalomhukumu Siku Ya Mwisho." Ndugu Yangu Wokovu Ni Sasa Na BWANA Ameniambia Kuna Watu Zaidi Ya 100 Hawajaingia Internet Bure leo, Bali Wameingia Ili Wakutane Na Neno Lake, Wakipenda Watampokea YESU Wasipopenda Watapotelea Kwenye Uzushi Wao

 Ukienda Motoni Utamlaumu Nani? Kwa Maana Jinsi Hii MUNGU Aliupenda Ulimwengu, Hata Akamtoa Mwanawe Pekee, Ili Kila Amwaminiye Asipotee, Bali Awe Na Uzima Wa Milele- Yohana 3:16.

 Ukienda Jehanamu Utamlaumu Nani? Maana " Ni Neno La Kuaminiwa, Tena Lastahili Kukubalika Kabisa, Ya Kwamba YESU KRISTO Alikuja Ulimwenguni Awaokoe Wenye Dhambi' 1 Timotheo 1:15. Ndugu Saa Ya Wokovu Ni Sasa. BWANA YESU Muda Huu Anazungumza Na Wewe Kwamba " Mimi Nalikuja Ili Wawe Na Uzima, Kisha Wawe Nao Tele- Yohana 10:10." Tena Anaendelea Kusema " Wala Yeyote Ajaye Kwangu Sitamtupa Nje Kamwe- Yohana 6:37." Ndugu Unasubiri Nini Kuokoka? Yatosha Kwa shetani Sasa Ni Kwa YESU.

 Ni Wakati Wa Kufua Mavazi Yetu Ili Yawe Safi Kwa Ajili Ya Harusi Ya Siku Ile Kuu Ya BWANA. Dunia Itakunjwa Kama Karatasi, Kutakua Na Mbingu Mpya Kwa Ajili Ya Wateule.

 Na Kama Vile Watu Wanavyowekewa Kufa Mara Moja, Na Baada Ya Kufa Ni Hukumu -waebrania 9:27. Ndugu Yangu YESU Anakuhitaji Leo Tena Kabla Kabisa Hujafa Ili Tu Usiende Motoni. Hakuna Upendo Zaidi Ya Huu Wa BWANA YESU. Amua Moja Ndugu, Amua Kumpokea YESU Au Kupotelea Motoni Milele. Tusiwe Wa Kuzoelea Neno, Mengine Huwa Ni Maagizo Ya MUNGU Ya Moja Kwa Moja, Ujumbe Huu ROHO Wa MUNGU Amenipa wiki iliyopita , Ni Ujumbe Kwa Ajili Watu Wote Na Hata Mimi Nikiwemo. Kuokoka Ni Sasa Ndugu Zangu. Tuamue Tu Kumpokea BWANA YESU Mwenye Uzima Wetu Wa Milele. BWANA YESU Okoa Roho Yangu Na Mwili Wangu, Okoa Ndugu Zangu Na Marafiki Zangu Wote, Watakao Tii BWANA Naomba ROHO MTAKATIFU Uwafuatilie Ili Waifikie Toba Ya Kweli Wakiwa Wateule Wa BWANA YESU Na Warithi Wa Uzima Wa Milele, Hata Mimi Usinipite BWANA, Nikamilishe MUNGU Wangu Ili Niupendeze Moyo Wako, Kusiwepo Na Kuanguka Wala Kusitasita, Nipe Roho Zako Saba Zilizo Katika Isaya 11:2 Na ROHO Wako Awe Juu Yangu Siku Zote Kama Ilivyo Leo. 

 Ndugu Yangu Hakuna Wakati Mwingine Wa Kutengeneza Maisha Yako, Ila Ni Sasa. MUNGU BABA Anasema " Tazama Wakati Uliokubalika Ndio Sasa; Siku Ya Wokovu Ndio Sasa 2 Kor 6:2" Ndugu Yangu Sikia Onyo La MUNGU " Kwa Kuwa Nimeita, Nanyi Mkakataa; Nimeuonyosha Mkono Wangu, Asiangalie Mtu. Mimi Nami Nitacheka Siku Ya Msiba Wenu. Nitadhihaki Hofu Yenu Ifikapo, Ndipo Watakaponiita, Lakini Sitaitika- Mithali 1:24-28. Ndugu Uko Wapi Wewe? Na Unafanya Nini? Kimbilia Kwa YESU Ndugu Yangu.

 Ndugu Zangu Hakuna Kizuizi Chochote Kinachoweza Kumzuia Mtu Kufika Kwa KRISTO Ikiwa Anahitaji Wokovu, BWANA YESU ipo siku atasema  " Wala Hamtaki Kuja Kwangu ....... Yohana 5:40.

 Pole Sana Wewe Unayesema "SIAMINI KAMA KUNA MOTO WA MILELE". Rafiki Yangu Dakika 2 Tu Ukiwa Motoni Zitabadili Mawazo Yako, Hapo Utatambua Kama Waliopo Kuzimu Leo Wanavyotambua Leo. Wakati Huo Utajua Kwamba Biblia Ni Neno La MUNGU, Tena Muda Huo Utatambua Kwamba Wewe Ni Mwenye Dhambi Na Utajua Kwamba KRISTO Alikufa Kwa Ajili Ya Wenye Dhambi, Tena Muda Huo Utatambua Kwamba Ungeliokoka Kama Ungetubu Ukiwa Duniani, Na Wakati Huo Utajua Ukweli Jinsi Roho Yako Inavyopotea, Utalia Na Kusaga Meno, Utasema "mimi Ni Mjinga, Nimechelewa Sana" Hakuna Asiyeamini Huko Motoni Lakini Wameamini Hali Wamechelewa Na Hakuna Neema Tena. Ndugu Unayesoma Ujumbe Huu Unaweza Ukasema Kuwa Huamini Yote Haya, Lakini Kutokuamini Kwako Hakuwezi Kubadili Ukweli, Na Je Ni Nani Wewe Unayepingana Na MUNGU? Yule Asiyeamini Anamfanya MUNGU Kuwa Mwongo, Madaraka Ya Kuwa Motoni Ni Yako Peke Yako Tu. Ikiwa Wewe Hujali Roho Yako Wala Hutaki Kuokolewa Na Na BWANA YESU Nakupa Pole.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292 
                     mabula1986@gmail.com
                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
 MUNGU Akubariki.

Comments