VIFAA VYA UCHAWI VYACHOMA MOTO KATIKA MKUTANO WA INJILI TANGA.



Na Mtumishi Gasper Madumla

Bwana Yesu asifiwe...
Blessed be the name of Jesus...
Say,
Amen...

Leo ninakuandikia kwa ufupi sana,juu ya matendo na miujiza aliyoifanya Bwana Mungu kupitia watumishi wake pamoja nami katika mkutano wa nje,mkutano wa injili uliofanyika tarehe 11 July to 13 July 2014,pamoja na siku ya kufunguliwa na kukata minyororo ya kiuchawi tarehe 14 July 2014 hapo mkoani Tanga eneo la Amani,Bulwa. Mahali ambapo wanalima chai,sehemu za milimani.


Photo: Vifaa vya uchawi vikiwa tayari kwa kuchomwa moto,katika mkutano Tanga
Vifaa vya uchawi vikiwa tayari kwa kuchomwa moto,katika mkutano Tanga


Dhima kubwa ya kukuandikia siku ya leo,ni kumwinua Bwana Mungu kwa ushuhuda huu na kumgandamiza marehemu shetani,maana ameshindwa kabisa. Yaani kama ingelikuwa ndio ni mechi tumeicheza basi sisi tungelikuwa ni Ujerumani shetani angelikuwa ni Brazil magoli ni saba moja.KWA BWANA YESU NI USHINDI TU.
Nafikiri unanielewa,ni kwamba upo ushindi usioelezeka ndani ya Yesu Kristo.

Photo: Bibi aliyefungwa kwa nguvu ya mapepo,awa huru
Bibi aliyefungwa kwa nguvu ya mapepo,awa huru , hapa akiombewa na Mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla huko Tanga.
Tulipowasili tu na timu yangu yote ya kutoka Dar,tulishangaa kuona watu waliokuwa wana njaa ya kusikia neno la Mungu maana watu wengi wa AMANI-Bulwa walikuwa wapo chini ya migandamizo ya nguvu za giza kwa kujijua na hata kwa kutojijua sababu wapo watu waliokuwa wakijihisi kuonewa na ibilisi kwa kupigwa na magonjwa mbali mbali ikiwemo UKIMWI pia wapo watu waliokuwa hawajijui kwamba wanateswa na mapepo yenye roho ya magonjwa hasa magonjwa ya tumbo,si wakina mama tu hadi mabinti na wa baba pia.

Hakika Yesu amesikia kilio chao hawa ndugu wa Tanga-Amani Bulwa.
Ndiposa nilipolisoma lile agizo la Bwana Yesu kwetu sisi wanafunzi wake,
Anasema;

" Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. " Marko 16:15

Agizo tulilopewa ni KUIHUBIRI INJILI ULIMWENGUNI MWOTE KWA KILA KIUMBE na wala hatukutumwa tukaihubiri injili kwa wakristo pekee yao,bali kwa kila kiumbe. Maana kila kiumbe kina maskio ya kusikia angali ki hai.
Changamoto tuliyonayo makanisani siku hizi za leo ni kwamba tunahubiriana sana sisi kwa sisi pasipo kuwaendea wale wahitaji haswa wahitaji
wa injili,na sio kubaki makanisani tu,hilo sio agizo la Kristo.

01. MCHAWI ATUJARIBU.

Tulipoanza huduma siku ya kwanza,akatokea mama mmoja mchawi ( jina nimelihifadhi) akaja kwa njia ya kuombewa lakini gafla Roho wa Bwana akasema nami ya kwamba yeye ni mchawi,akatoka gafla-wasi wasi ukamtanda na tukamwambia " usipotubu na kuacha uchawi wako,basi utakufa" kesho yake huyu mchawi akapatwa na msiba wa mwenzake,sasa sijui alikuwa ni ndugu yake,au la!Hivyo basi msiba ukaanzia kwa ndugu yake.

Haleluya...
Bwana Yesu asifiwe...
Bwana Mungu hadhiakiwi,wala hapimiki,
Yeye ni amini na Kweli.

02.ROHO MTAKATIFU KAZINI.

Roho mtakatifu alinishangaza mimi kiongozi wa msafala pamoja na watumishi wa Mungu wote tuliokuwa nao,akiwemo Mch.&mwinjilisti Musa Gwau. Maana Roho mtakatifu alikuwa kazini kuponya,kuokoa,kukomboa,kuangamiza kazi zote za uchawi.

Makundi makubwa ya watu hasa waislamu walimiminika na kuombewa,kisha wakaokoka na kufunguliwa na kila aina ya udhaifu uliowakamata hapo awali.
Tazama;
Mtu mmoja muislamu safi,baba mmoja,alitujia ofisini mwetu mara baada ya mkutano. Huyu alikuwa akisumbuliwa na roho za upasuaji wa tumbo lake,( Opareshi za tumbo) maana kila mara hufanyiwa opareshi ya tumbo,hivyo alikwisha zoea visu katika tumbo lake mara kwa mara. Halipotufikia ofisini mwetu mara baada ya mkutano,Roho mtakatifu akashuka na kuanza kushughulika naye,hakika maroho yote ya visu yakamtoka,na akapokea nguvu juu ya mishono yote aliyoshonwa katika tumbo lake saa ile ile,HAKIKA YESU YUPO.

03.UCHAWI KUCHOMWA MOTO.

Injili yoyote ile pasipo kuchoma moto vifaa vya kichawi bado itakuwa imekosa kitu kikubwa sana. Mama mmoja aliyekuwa amelogwa na watu tisa tofauti tofauti,aliweza kuombewa kwa muda mlefu kidogo,hadi mapepo yaliyotumwa kumuangamiza afe,yalilipuka na kutaja siri zote zilizofichika ndani ya mama huyo.

Mapepo yakatuambia " .... Ooh,.. Twendeni bandarini,twendeni bandarini,
( Bandarini ni eneo la mapepo yalipo na uchawi wao ulipo.)
Hatimaye tukawasili hadi eneo hilo,na kuanza maombi rasmi,kwa maombi tukayapiga mapepo kwa jina la Yesu Kristo,yakasalenda- tena sasa;

Mapepo yakatambaa kwa magoti mpaka chumbani mwa huyu mama,na kuleta shuka la kichawi pamoja na shanga nyeupe mfano wa uzi wa kutuliza mapepo machafu.Hayo yote tukayachoma moto.

Mama huyu aliyelogwa ili afe,akawa na uzima tele baada ya kujisalimisha kwa Bwana Yesu na kuokoka,ndipo nikalikumbuka lile andiko;

".... Kila goti litapigwa,...na kila ulimi utakili ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA,.." Wafilipi 2:10-11

Tazama mapepo yalivyokuwa yakimtesa mama huyu muislamu yeye na mumewe pamoja na familia yake yote,maana mapepo na uchawi ulimzulia asipate haja kubwa kabisa,hivyo akawa akiumwa na tumbo si mchezo,LAKINI ALIPOMSIKIA MWANAMUME YESU KRISTO,AKAOKOKA INGAWA ALIKUWA NI MUISLAMU MWENYE KUPINGA IMANI YA KRISTO,AKAFUNGULIWA NA KUPOKEA MUUJIZA MKUU.

Haleluya...
Bwana Yesu asifiwe...

Imefika wakati sasa wa kufunguliwa na kuwekwa huru mbali na nguvu za giza maana YESU KRISTO yu hai halisi.
Yapo mengi ya kuandika kutoka mkutanoni,lakini kwa haya machache sana jina la Bwana Yesu litukuzwe milele na milele..
Sema ,AMEN

Injili iliyokamilika ni injili ya moto wa Roho mtakatifu kwa watu wa nje zaidi kuliko watu wa ndani ya kanisa. Thamani ya injili ni kwa mataifa yote,wala si kwa kikundi fulani kilichokuwa tayari kimeokoka.

Je lipo teso la ibilisi maishani mwako?
Je unateswa na nguvu za uchawi,za giza?
Au,Je ipo roho ya magonjwa,au mauti ndani yako?
Ikiwa jibu ni NDIO,
Basi usisite kunipigia simu yangu hii;
0655-111149.Ubarikiwe.




Photo: Bwana Yesu asifiwe....

Nalikuwa Tanga-Amani bulwa,kwa mkutano wa nje pamoja na hii timu iliyopo hapa pichani. HAKIKA TULIKUTANA NA YESU MTENDA MIUJIZA MKUBWA,MAANA WENGI WALIOKOKA NA KUFUNGULIWA NA MAGONJWA SUGU,WACHAWI WAKAJISALIMISHA.

Kwa uhondo kamili endelea kuperuzi katika wall hii,maadamu nimerudi salama.
Namshukuru MUNGU kwa timu hii,maana ni BWANA tu hata mambo yote haya.

UBARIKIWE.
Mtumishi Gasper Madumla katikati na timu yake waliokuwa katika kuhubiri neno la MUNGU Tanga


Comments