VIUNGO VYA BINADAMU VYAOKOTWA KWENYE MIFUKO JIJINI DAR ES SALAAM

Mojawapo ya baki la mguu ulioko ndani ya mfuko wa plastiki
Jioni nikiwa narejea nyumbani, na katika pitapita kwenye mitandao ya kijamii, nakutana na habari ambayo wengine wanaiita uzushi na kuipinga vikali. Hata mimi nachelea kuamini kutokana na maelezo yake, ya kwamba kuna viungo vya takribani watu mia moja vimeokotwa kwenye machimbo ya . Napuuzia, huku nikisubiri nione hatua stahiki zikichukuliwa kutkana na kuleta taarifa nyeti kama hizo kwa uongo.

Dakika kadhaa baadae kwenye taarifa ya habari ITV, nasikia hicho kitu, Godwin Gondwe akitangaza kuokotwa kwa viungo vya binadamu kwenye machimbo ya Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Inashangaza, napatwa na mstuko nisijue cha kufanya, zaidi ya kuita Jesus, Jesus... Naanza kutafakari mwenyewe (what could possibly happen?) tena  hapahapa nchini Tanzania? Ni kitu gani? Ni wale waizi ambao huiba watoto? Ni wale waganga wa jadi wenye vibao kila kona jijini Dar es Salaam? Ni baadhi ya wanasiasa wanahusika kuelekea uchaguzi mkuu? Yaanis ikupata jibu (hata sasa bado ningali kupata).

Majukumu yananishika hadi pale ninapojiegesha... Usiku mkali ninaamka, na kazi zinaendelea, lakini kueleka alfajiri nafungua mtandao kuona mapya, hao ndipo nikapigwa na bumbuwazi, akili kuchanganyikiwa na hofu kunijaa. Ninahamaki kuona mabaki ya miili ya binadamu, zama hizi -wamefichwa kwenye mifuko, kama mizoga ya wanyama. Hapo ndipo nakumbuka ya kwamba sio kila unayemuona njiani ni binadamu. Naendelea kuwaza, wakazi wa maeneo ya karibu na tukio wamefichwa hili jambo kwa muda gani, na ni nani anayefanya hivyo?

Taarifa za kwenye habari zilieleza kwamba Jeshi la Polisi limefanikiwa kutambua uwepo wa mabaki hayo (iwe kwa taarifa za wasamaria wema ama kwenye doria yao tu), ninapongeza hatua hiyo, lakini pia ninalaani vikali kila muhusika.

Maneno yananiishia, sijui hata niseme nini zaidi, Taifa zima linasubiri kusikia kutoka kwa viongozi wake kuhusiana na tukio hili, ambalo linaweza kubadilisha tawira ya namna tunavyoyaona maisha. Lakini bado naombea isiwe sahihi, naombea nisikie kwamba ni mifano tu ya midoli na 'experiment' iliyofeli, na si binadamu. Kilichopo mbele yetu, BWANA Yesu na atuepushie mbali.

TAHADHARI!
Tafadhali, endelea tu kutazama picha kwa hiyari yako, tumeamua kuziweka kutokana na ukubwa wa jambo lenyewe. Picha zote kwa hisani ya Dar es Salaam yetu blog.




Baadhi ya wananchi waliojitokeza usiku baada ya kufahamu kuhusiana na jambo hilo
Mabaki yakiwa kando ya mifuko inayosadikiwa kuwa na viungo zaidi.

Gari ikiwa imepakiwa mifuko hiyo, kwa ajili ya uchunguzi zaidi, ambapo tayari Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni umeshaanza upelelezi.

Comments