YESU ANAKUITA LEO.

BWANA YESU Asifiwe.
Karibu tushiriki upendo wa MUNGU kwa watu wote.
- Moyoni mwako ni heri kuwa na neno la MUNGU na sio maneno ya watu.
Leo tunajifunza kuhusu jinsi ya kuingia uzima wa milele.
 
Yohana 3:16-21 inasema  ''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu. 

Ndugu yangu  Siku Ukifa Hakuna Awezaye Kukuamsha, Ndugu Na Jamaa Zako Watalia Sana Lakini Hata Hivyo Hutawasikia. Swali kwako ni hili,  Ndugu Yangu Ukifa Utapenda Uwe Mgeni Wa Nani? Je Ungependa Uwe Mgeni Wa MUNGU Au Mgeni Wa shetani? Najua Kila Mtu Anataka Akifa Awe Mgeni Wa BWANA, Lakini Je Umeukubali Kabla Hujafa Huo Mwaliko Wa MUNGU, Je Umempokea YESU Ili Akupe Tiketi Ya Kwenda Mbinguni? Je Umempa BWANA YESU Maisha Yako Ili Siku Ya Kufa Kwako Amtume Malaika Wake Aje Akuchukue Na Kukupeleka Mbinguni? 

Kwanini Unataka Kusafiri Kwenda Mbinguni Huku Humtaki YESU Ambaye Ndiye Pekee Anayeweza Kukupeleka Uzimani? Ndugu Chunguza Njia Zako, Okoka Leo Na Hakikisha Hushirikiani Tena Na Majini, Mizimu, Usoma Nyota, Uzinzi Wala Dhambi Yeyote. Katika Waebrania 3:15 ''Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha. ''  

MUNGU Anasema Kama Ukiisikia Sauti Yake Leo Geuka Na Acha Njia Mbaya Na Mgeukie BWANA YESU Naye Atakurehemu, Kataa Leo Kuwa Wa shetani Na Amua Kuwa Wa MUNGU Kwa Kumpokea BWANA YESU Kama BWANA Na MWOKOZI Wa Maisha Yako ( Yohana 1:12-13 Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. ). 

-Ndugu kuokoka ni sasa na nakuomba  Ondoa Wazo La Kutubu Ukifa, Wokovu Ni Sasa Tu yaani ukiwa hai.

 Ndugu Yangu, Usiishi Kwa Sababu Tu Unaishi Bali Ishi Kwa -Sababu KRISTO Anaishi Ndani Yako.

 -Dhambi Ni Mbaya, Uongo Ni Mbaya, Uzinzi Ni Mbaya Sana, Uasherati Haufai, Rushwa Haistahili, Masengenyo Ni Machukizo. Tusiishi Kwa Sababu Uongo Na Utapeli Umekaa Ndani Yetu Bali Tuishi Kwa Sababu YESU KRISTO Mwana Wa MUNGU Aliye Hai Anaishi Ndani Yetu.

 Ndugu Njoo Kwa YESU Ujisalimishe Maana Dunia Imeharibika Tena ina Wayawaya. Kwa Miaka Mingi Sana Umeyawaza Ya Dunia Lakini Bado Hujayapata, Nakuomba Waza Uzima Kuanzia Leo, Waza Kukombolewa Na Damu Ya YESU, Waza Mbinguni, Kwa Sasa Fanya Hivi 
''MAMBO KWA YESU, STAREHE MBINGUNI.''

 Je Unaweza Ukafaidika Nini Ukipata Vya Dunia Vyote Harafu Ukafa Na Kuenda Kuteseka Motoni Milele?

 BWANA YESU Hajawahi Kuchoka Kukualika Wewe Kwenda Uzima Wa Milele, Hata Muda Huu Kupitia Ujumbe Huu Anakualika Kwenye Sherehe Za Uzima Milele. YESU Leo Anasema " Njooni Kwangu Ninyi Nyote Msumbukao Na Wenye Kulemewa Na Mizigo, Nami Nitawapumzisha- Mathayo 11:28" 

 Ndugu Peleka Kwa YESU Hiyo Mizigo Ya Magonjwa Inayokusumbua, Peleka Kwa YESU Hizo Roho Za Uzinzi Na Uongo Zinazokusumbua, Ataziondoa Na Kuzitupa Kuzimu, Ndugu Usione Fashion Kutoa Mimba Na Wala Usione Ujanja Kuitwa Changudoa, Dhambi Ni Mbaya Na BWANA YESU Hataki Dhambi Hizo Zikupeleke Motoni, Mkimbilie Leo Na Utakaa Salama. 

 Tumtafute BWANA YESU Maadamu Anapatikana, Tumwite Yeye Maadamu Yu Karibu, Mtu Mbaya Na Aache Njia Zake Mbaya, Na Arejee Kwa MUNGU Wetu Naye Atamrehemu, Na Arejee Kwa MUNGU Wetu Naye Atamsamehe Kabisa. Ndugu Acha Kutangatanga Kwa Shetani, Mara Leo Kwa Mganga Wa Kienyeji, Kesho Kwenye Uzinzi, Kesho Kutwa Uko Bar Kwenye Pombe. Kataa Leo Na kimbilia Kwa BWANA YESU Anayeokoa. MUNGU Akubariki,Na Ukikubali Na Kutii, Utakula Mema Ya Nchi.
Isaya 55:6-7 ''Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa. '' 
 

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292 
                     mabula1986@gmail.com
                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
 MUNGU Akubariki.

Comments